Jambo ambalo nimegundua watanzania tumekuwa wajinga sana, tukiibiwa, viongozi wakifuja mali zetu, bei za mazao zikiwa chini tunaishia kulalamika.
Hivyo basi nikiwa kiongozi ndani ya CCM ata nikionea wananchi, nikionea wakulima, nikizurumu wakulima wa korosho, pamba bado nitalindwa na vyombo vya dola.
Kipindi nikiwa chuo, na nikiwa kijana mdogo tena kinda kuna Prof ,siyo Prof J ,wala Lipumba aliwahi kuniambia au kuambia hadhara kuwa,,
Nanukuu;BAADA YA MIAKA 20 KUNA KIZAZI KITATAKA MABADILIKO PIA ATA KIZAZI CHENU NI CHA WATU WA MABADILIKO ""mwishi wa kunukuu.
Sasa nikiangalia miaka 20 hiyo imetimia toka nitoke masomoni lakini kizazi kilichosemwa kimegeuka kuwa cha Simba na Yanga na kizazi cha machawa aina ya kina Mwijaku.
Kwanini 2045 ,naamini 2045 watanzania angalau kidogo watakuwa wameanza kuelimika na nitaongoza taifa ambalo vijiweni litakuwa linajadili maendeleo ya nchi yao, katiba yao pia CCM itakuwa imesambaratika na mimi nitafanya kazi ya kuirudisha.
Kwasasa hacha nirudi CCM kimwili kiroho kama JPM ndani alikuwa UPINZANI nje CCM.
POLENI CHADEMA TUKUTANE SERIKALI ZA MITAA