Wana JF narudia tena, haribu kabisa tiketi au karatasi yenye taarifa zako kamili

Polisi nao huwa hawaeleweki. Wengine nao ni vibaka tu. Na kuna wengine uwezo wa kiakili na kielimu ni duni. Wameajiriwa na div 4-30. na kila kitu wanataka kusolve kinguvu badala ya kufikiria kwa weledi mkubwa. Ifike mahali jeshi liwe linapima uwezo wa mtu kabla ya kumpa jukumu la upelelezi.

Aliyekamatwa kwenye hii story, kazi yake ya uwakala inawezekana pia imemhusisha na tukio fulani la dhuluma na sasa wameamua kumbambika hiyo kesi. Na pia inawezekana naye ni criminal na alihusika kwenye tukio la Kimara. Lolote linawezekana.
 
Tukio lilitokea lini? Muda gani? Kukuta tiketi yake sio uthibitisho kuwa alikuwa eneo la tukio. Bado polisi wanatakiwa kuthibitisha kuwa alikuwepo eneo la tukio. Tiketi inawezekana iliachwa hapo n mhalifu makusudi ili kuwapoteza polisi.
Mtuhumiwa awaambie alikuwa wapi siku na muda ambao tukio linatokea. Na anaweza kutafuta ALIBI...wapo watu alikuwa nao,alikuwa kazini(miamala aliofanya itaonekana) na simu yake inaweza kutumika kuonesha alikuwa wapi siku hio.
Yeye ni mtuhumiwa tu na polisi inabidi wathibitishe,watansumbua tu ila kama hakupiga tukio itajulikana.
 
Kumbe mjeda😂
 
Katika mambo ya investigation kitu chochote kinachokuwa eneo la tukio.lazima kifanyiwe kazi,iwe,leso kipande cha chupa hata kipisi cha sigara,humo zitapatikana alama za vidole,au chochote kile iwe nywele,mate nakadhalika

Kuna tukio moja la mauji nadhan mwanza kuna mwanadada maarufu sana aliuwawa,bahati mbaya muuaji aliacha chupa ya soda eneo la tukio,basi ikapimwa DNA ikasoma,ikasaidia uchunguzi
 
Tatizo ni kwamba you're not a logical thinker kama hao polisi tu, naona umeshindwa kuelewa comment yangu kwamba polisi hawajawaza nje ya boksi wametumia shortcut kama kawaida yao...
Haya, wewe na u-logical thinker wako utanisaidia nini kwenye hii ishu bhana?
Acheni kujifanya mnajua kila kitu katika maisha ya watu wengine.
Halafu sikukuita wala kukuambia ni lazima uchangie post yangu.
Majukwaa yako mengi bro na unaweza kwenda jukwaa lolote mkuu.
 
Yes, na ndio manaa leo tunasubiri kukuche vizuri ili tukajue kinachoendelea.
 
Yaani mkuu, kuna watu humu ndani sijui wanajikutaga wao nani.
Yaani ni pointless kabisa.
Kasoma mada kuu bila kuichambua kaja kukimbilia ku-comment bila kufikiri.
Yote tuwaachie jeshi la police wa dili na mtu wao.
Wanaleta sana ujuaji wakati kichwani ni sifuri.
 
Tatizo kubwa vyombo vyetu vya usalama vinafanya kazi kwa ramli, mazoea na kwa kuwanyanyasa watu wa Hali ya chini.....kwa kuwa hakuna Askari aliyewahi kuwajibishwa kwa uonevu wao dhidi ya wanyonge wenyewe wanaona kawaida.......

Hiyo issue ingemhusisha mtoto au ndugu wa kigogo wa serikali asingemkamata kama kuku hivyo na pengine angemuomba kumkamata......

Imagine unakamatwa ndio uchunguzi unafanyika ukionekana huna hatia unaachiliwa kama kuku......
 
Penye wengi pana mengi my dear,tuwavumilie tu wasije wakakuharibia siku yako

Stay strong
 
Katika nchi zenye tawala Bora na za kisheria sambamba na kuwa na Jeshi la Polisi lenye uadilifu, suala hili lingeweza kuwa rahisi sana. Lakini kwa kuwa Jeshi la Polisi lililopo halina sifa hizo za Uadilifu, basi huyo mtu anatakiwa ajipange sawa sawa, he should expect the worse to come. Namuonea huruma sana huyo mtu, tayari ameshaingia kwenye mtego mbaya wa hawa jamaa, huyo Sasa amegeuzwa kuwa fursa na hao Polisi waliomkamata.
 
Shida ipo Kwa hao polisi hapo pia, unaokotaje tu kikaratasi kinachoweza kusafiri hata na upepo ukaanza kufanya ndio ushahidi wa kumuweka mtu ndani?
Tiketi isafiri na upepo kutoka Mbezi hadi ndani ya duka ulikotokea uhalifu?
Ndio maana nasema tuwaachie jeshi la police lifanye yao.
Ukweli utajulikana tu mkuu
Ndio maana nikasema pale 'binadamu hubadilika' huenda kahusika au hajahusika.
Ushahidi utajionesha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…