Wana-JF tusiwe wavivu ku-comment na kuishia kutoa likes nk peke yake; reply thread nzuri ili zikae kwenye chat muda mrefu na ujumbe usomwe na wengi

Wana-JF tusiwe wavivu ku-comment na kuishia kutoa likes nk peke yake; reply thread nzuri ili zikae kwenye chat muda mrefu na ujumbe usomwe na wengi

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
15,415
Reaction score
29,584
Kuna watu wanatembelea JF ilikusoma threads za watu wengine na kazi yao ni kutoa likes, laughs, dislikes, fire etc peke yake, Nadhami mnatambua JF wametengeneza system kwa namna mbayo thread isipopata replies au comments basi itazidi kushuka chini na kupotea, ili kutoa nafasi ya juu kwa thread zenye kupata comments nyingi.

Sasa nimeona mara nyingi thread inapata likes na fire nyingi sana, kwa sababu watu wameifurahia sana thread au comment kwenye thread, lakini wanaishia hapo tu, kutoa likes bila comments. Matokeo yake unakuta ni uzi au thread ya maana sana lakini inapotea kwa sababu haipati replies.

Basi nawasihi members wa JF, palae mnapoona kuna thread inaongea mambo ya maana na ya msingi, usiishie kutoa like peke yake. Toa comments zako hata kwa kifupi tu ili hiyo thread iliyokugusa au kifurahia au kuiunga mkono kwa dhati isomwe na watu wengi zaidi. Unapotoa comments kwa kwenda kwenye reply, unaendelea kuipa thread uhai na kuifanya ibaki kwenye chat kwa muda mrefu.

Tusiwe watu wa kufurahia tu yanayosemwa na wengine, tuwaunge mkono wanachosema kwa kutoa maoni yako au maneno mafupi juu ya thread ili kile tulichosoma na wengine wapate kukisoma.
 
1784132758926.png

Tusiishie hapa tu!
 
Labda mada ilikua ngumu sana kuchangia mkuu, hasa akitokea mtu kapost mada ya mambo ya chini ya kitovu na wewe ukaposti mda huo huo mada yako nzuri tu lazima itadorora
Yaani Mkuu min-me umegonga penyewe; ngoja niende mtaani kwetu kutafuta story za jamaa anaitwa Waziri nione kama naweza kupata story ya kuandika "Waziri atembea na mke wa rafiki yake" niilete!
 
Thubutu! Wee ngoja tupate thread ya jinsi ya kuchewelesha mshindo bila kutumia Mkongo uone members watakavyokimbilia kwenye Forum ya Mahusiano ya Jamii kujibu na kuuliza maswali. Si wanawake si wanaume!😂
Watu wanapenda umate umate bwashee 😅
 
Thread nzuri ndio zikoje ?,hapo ndio shida.Members wana umri,elimu na majukumu tofauti, hivyo wengine wanaona uzi wa kula kimasihara ni bora kuliko uzi wa ufugaji wa mbuzi.
Lakini kiuhalisia uzi wa ufugaji wa mbuzi hauwezi kuwa na value sawa na uzi wa uzushi au utani.kwa sababu tu ya entertainment value.

Uzi wa ufugaji utabaki kuwa reference material ya thamani miaka mingi ijayo, hauwezi kulinganisha na uzi wa utani ambao unaweza kupotea ndani ya siku moja.
 
Back
Top Bottom