Wana-JF tusiwe wavivu ku-comment na kuishia kutoa likes nk peke yake; reply thread nzuri ili zikae kwenye chat muda mrefu na ujumbe usomwe na wengi

Wana-JF tusiwe wavivu ku-comment na kuishia kutoa likes nk peke yake; reply thread nzuri ili zikae kwenye chat muda mrefu na ujumbe usomwe na wengi

Acha uzwazwa mlugaluga
Nenda Insta na X huko ndio ukipata wengi unatengeneza hela, humu utaka wajae halafu unapata nini
 
Lakini kiuhalisia uzi wa ufugaji wa mbuzi hauwezi kuwa na value sawa na uzi wa uzushi au utani.kwa sababu tu ya entertainment value.

Uzi wa ufugaji utabaki kuwa reference material ya thamani miaka mingi ijayo, hauwezi kulinganisha na uzi wa utani ambao unaweza kupotea ndani ya siku moja.
Ni kweli lakini inategemea na akili ya member anavyoona.
 
Actually ilipata comments nyingi sana, let me be true, lakini kwa msaada wa Maxence Melo. Alisema thread ilikuwa muhimu sana isome akaiweka kwenye holding position ili ibaki juu isipotee
Heshima kwake Maxence Melo .
Nje ya mada: nasubiri siku moja anipe Platinum member sijajua inabidi nifanye Nini au nifikie vigezo gani.
Kila nikikaza kuandika mada za maana bado naona kweupe tu.
Au nichangie mpunga JF? Naogopa kuchangia kwa namba zangu madhalimu wasijeni-target .....😜
 
Mkuu kama utachangia mpunga kwa Max basi atakahkikisha ni kwa namna ambayo haitakuletea matatizo. Anafanya bidii kubwa sana kulinda wana JF. Kumbuka huyu ni mtu alikuwa radhi kuwekwa ndani kwa kutokukubali kuwasaliti members wa JF kwa Polisi
 
Heshima kwake Maxence Melo .
Nje ya mada: nasubiri siku moja anipe Platinum member sijajua inabidi nifanye Nini au nifikie vigezo gani.
Kila nikikaza kuandika mada za maana bado naona kweupe tu.
Au nichangie mpunga JF? Naogopa kuchangia kwa namba zangu madhalimu wasijeni-target .....😜
Sasa hivi kuchangia JF na CHADEMA unaonekana unataka kuwapora tonge wauwaji unakuwa mhaini automatically.
I hope Maxence Melo analijua hili.
Juzi niliwakosoa madhalimu kitu wakanifungia namba husika nikaweka nyingine mtandao mwingine nikarudi hewani.
Mitandao ya simu sijui hawaogopi tutawahama?!
 
Mkuu Kraang, sio kila satisfaction anayofurahia mtu lazima iwe hela. Nikupe mifano?
Ndio toa mifano
Unaweza kuwa na shughuli ya kuu ya kipato, lakini kama una fani unaiweza kama kuleta taarifa au kuandika makala, siku hizi imewezeshwa sio kama zamani, ukiandika vitu watu wanapenda kuchangia na kusoma unajiogezea kipato, sioni shida ukiamua kufanya hivyo, humu hakuna chaa maana zaidi ya kutukanwa
Bora utukanwe kule maana kitendo cha yeye kuamua kuchangia kwa kukutukana kinakuingizia mashiko
 
😂😂 Naam! unajua humu ndani kuna kila aina ya mtu, kwa hiyo kama uwezo wako wa kujidhibiti ni mdogo, unaweza kuishia kuwa unatukanana nao kila siku.
Watu wanatukanana X na Insta huko ndio inaongeza wachangiaji kukukongezea kipato
 
Uzi zenye nondo hua hazina comments nyingi, Njoo kwenye uzi zenye upumbavu
 
😂😂 Naam! unajua humu ndani kuna kila aina ya mtu, kwa hiyo kama uwezo wako wa kujidhibiti ni mdogo, unaweza kuishia kuwa unatukanana nao kila siku.
Kuna Professor mmoja humu aliandika kitu kuhusu mambo aliyosomea akaambiwa hajui lolote poyoyo hana kitu kichwani! Usikute aliemwambia hivyo ni la saba au form four alipata F karibu zote. Yaani hapo ndio utachoka kuwa JF kama una roho nyepesi 😂 😂
 
Sijakuelewa hapa, umemaanisha nini?
Watu wanakuwa engage na post zako ndio unapata hela, hata kama anakuja kukutukana au kukukosoa

1784135875408.png
 
Back
Top Bottom