JF inakutanisha watu wengi na wengine hufikia kuwa marafiki wa karibu sana.
Mimi nilipojiunga JF wapo watu niliwakuta na wengine wakanikuta.Ila kuna baadhi ya watu wamekuwa kimya kwa miaka bila kuchangia au kuibua mijadala kama ilivyokuwa kawaida yao.
Inawezekana sio wenzetu tena walishatangulia mbele ya haki,Ni vizuri kama unamjua mwana JF alikuwa hapa na sasa ni marehemu utusaidie kumtaja hapa.Ili tujue na tuendelee kumwombea kwa Mungu ampe pumziko huko aliko.
Kumbuka kifo hakina taarifa,Hivyo naamini kunawezetu wameshatangulia ila hatujui.