YALIYOKUWAKO NDIYO YATAKAYOKUWAKO
28Ndivyo ilivyokuwa katika siku za Lutu: Watu walikuwa wakila na kuinywa, wakinunua na kuuza, wakilima na kujenga. 29Lakini siku ile Lutu alipoondoka Sodoma, ikanyesha mvua ya moto na kiberiti kutoka mbinguni ukawaangamiza wote. 30Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile Mwana wa Adamu atakapofunuliwa(Luka 17:28-30). Hii ni mojawapo miongoni mwa kauli ambazo Bwana Yesu Kristo alitoa wakati akiwa hapa duniani, alikufananisha kurejea kwake na kipindi kile cha Sodoma. Sasa tuone ni kwa nini Yesu alifananisha kuja kwake sawa na kipindi cha Sodoma.
MIJI YA SODOMA NA GOMORA
13Basi watu wa Sodoma walikuwa waovu, wakifanya sana dhambi dhidi ya BWANA(Mwanzo 13:13), Miji ya Sodoma na Gomora ambamo alikaa Lutu mtu wa Mungu, ilijaa kila aina ya uovu, hata nabii ezekieli anataja baadhi ya dhambi za Sodoma akisema 49 Sasa hii ilikuwa ndiyo dhambi ya dada yako Sodoma: Yeye na binti zake walikuwa na majivuno, walafi na wazembe, hawakuwasaidia maskini na wahitaji. 50Walijivuna na kufanya mambo ya machukizo sana mbele zangu. Kwa hiyo niliwakatilia mbali nami kama mlivyoona(Ezekeili 16:49,50), kwa hiyo miji hii ilikuwa ni yenye kutenda dhambi nyingi, kumbe kama Yesu alifananisha kuja kwake na miji ya sodoma na Gomora kabla ya kurudi kwake, bila shaka ulimwengu wa kabla ya kurudi kwa Yesu Kristo, lazima utakuwa ni wenye watu watakaokuwa wakitenda dhambi nyingi sana.
MALAIKA WATATU WALIOTEMBELEA SODOMA KABLA YA MOTO KUSHUKA
BWANA akamtokea Abrahamu karibu na mialoni ya Mamre wakati alipokuwa ameketi kwenye ingilio la hema lake wakati wa adhuhuri. 2Abrahamu akainua macho akaona watu watatu wamesimama karibu naye. Alipowaona, aliharakisha kutoka kwenye ingilio la hema lake kuwalaki na kuwasujudia hadi nchi(Mwanzo 18:1,2), Hapa Ibrahimu anapokea wageni watatu ambao hata hakujua walikotokea, na aliwakaribisha kwa chakula, baada ya kula wale malaika wakamuaga Ibrahimu. Hebu tuone baadhi ya mambo waliyofanya wakati na baada ya kuagana na Ibrahimu.
i/. Malaika wawili walielekea Sodoma lakini mmoja alibaki na Ibrahimu na akamweleza yafuatayo
*** 17Ndipo BWANA akasema, Je, nimfiche Abrahamu jambo ninalokusudia
kufanya?(Mwanzo 18:18), Kwa hiyo Bwana akaanza kuandaa wazo la kumtangazia rafiki yake Ibrahimu juu ya jambo lile ambalo alikuwa mbioni kulitenda, Bwana hatendi jambo pasipo kulifunua 7Hakika BWANA hatafanya neno lolote bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake(Amos 3:7), Kwa hiyo akamfunulia/akahubiri kwa Ibrahimu juu ya kusudio lake. Na huyu malaika aliyebaki na Ibrahimu wakati wale malaika wawili wakiwa wameelekea Sodoma anatajwa hivi 25Hilo na liwe mbali nawe, kufanya jambo kama hilo, kuwaua wenye haki pamoja na waovu, kuwatendea wenye haki sawasawa na waovu. Iwe mbali nawe! Je, Mwamuzi wa dunia yote hatafanya lililo sawa? 26BWANA akasema, Kama nikipata watu hamsini wenye haki katika mji wa Sodoma, nitausamehe huo mji wote kwa ajili yao(Mwanzo 18:25,26), kumbe huyu malaika alikuwa ndiye mhukumu wa ulimwengu wote na pia ndiye alikuwa BWANA. Jambo la kwanza hapa, au ujumbe wa kwanza kutoka kwa malaika hawa watatu ilikuwa ni ujumbe wa TANGAZO LA HUKUMU KWA MIJI YA SODOMA NA GOMORA.
Ii/ Wale malaika wawili walioenda sodoma walifika majira ya jioni na ndipo Lutu akawapokea, na mambo waliyomwambia Lutu ni haya yafuatayo.
a/ 12Wale watu wawili wakamwambia Loti, Una mtu mwingine yeyote hapa, wakwe zako, wana au binti, ama yeyote mwingine aliye wako katika mji huu? Waondoe hapa, 13kwa sababu tunapaangamiza mahali hapa. Kilio kwa BWANA dhidi ya watu wa hapa, ni kikubwa kiasi kwamba ametutuma kupaangamiza(Mwanzo 19:12,13), na ndipo Lutu 14Kwa hiyo Loti
alitoka ili kuzungumza na wakwe zake, waliokuwa wamewaposa binti zake.
Akawaambia Fanyeni haraka kuondoka mahali hapa, kwa kuwa BWANA ni karibu
kuangamiza mji huu! Lakini wakwe zake walifikiri kwamba alikuwa akitania(Mwanzo
19:14), Ujumbe waliotoa hapa ni TANGAZO LA UHARIBIFU WA SODOMA NA GOMORA.
b/ 15Kunako mapambazuko, malaika wakawahimiza Loti, wakamwambia, Fanya haraka! Mchukue mke wako na binti zako wawili walioko hapa, vinginevyo utaangamizwa wakati mji utakapoadhibiwa. 16Alipositasita, wale watu wakamshika mkono wake na mikono ya mke wake na binti zake wawili na kuwaongoza salama nje ya mji, kwa kuwa BWANA alikuwa na huruma kwao. 17Mara walipokwisha kuwatoa nje, mmoja wao akawaambia, Mkimbie kwa usalama wenu! Msitazame nyuma, wala msisimame popote katika tambarare! Kimbilieni milimani, ama sivyo mtaangamizwa!(Mwanzo 19:15-17), hapa walitoa ujumbe wa kuwataka Lutu na watu wa nyumbani mwake waondoke katika miji ile iliyokuwa karibu kuteketezwa, ujumbe ni ONDOKA. JE, HAYA YATAFANYIKA KABLA YA YEUS KRISTO KURUDI HAPA ULIMWENGUNI? Hebu tuone manabii walifunuliwa nini kuhusu nyakati za mwisho, 6Kisha nikamwona malaika mwingine akiruka juu angani, naye alikuwa na Injili ya milele ya kuwatangazia wale waishio duniani, yaani, kwa kila taifa, kabila, lugha na jamaa. 7Akasema kwa sauti kubwa, Mcheni Mungu na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imewadia. Mwabuduni Yeye aliyeziumba mbingu, dunia, bahari na chemchemi za maji. 8Malaika wa pili akafuata akisema, Ameanguka! Ameanguka Babeli aliye mkuu, yeye aliyeyafanya mataifa yote kulewa kwa mvinyo wa ghadhabu ya uasherati wake. 9Malaika wa tatu akawafuata hao wawili akisema kwa sauti kubwa, Kama mtu ye yote anamwabudu huyo mnyama na sanamu yake na kutiwa chapa yake kwenye kipaji chake cha uso au kwenye mkono wake, 10yeye naye, atakunywa mvinyo wa hasira kali ya Mungu ambayo imemiminwa katika kikombe cha ghadhabu yake pasipo kuchanganywa na maji. Naye atateswa kwa moto uwakao na kiberiti mbele ya malaika watakatifu na mbele za Mwana-Kondoo. 11Nao Moshi wa mateso yao hupanda juu milele na milele. Hakuna mapumziko, mchana wala usiku, kwa wale wamwabuduo huyo mnyama na sanamu yake, au kwa ye yote anayepokea chapa ya jina lake. 12Hapa ndipo penye subira na uvumilivu wa watakatifu, yaani, wale wanaozishika amri za Mungu na kudumu kuwa waaminifu kwa Yesu(Ufunuo 14:6-12) Malaika hawa nao wanatoa jumbe zilezile tatu kama zilizotolewa Sodoma na Gomora wakati wa Lutu. Soma jumbe hizo sehemu zilizopigiwa mistari kwenye hizo aya za kitabu cha Ufunuo . KINA NANI WATAKAOELEWA JUMBE HIZO Wakwe za Lutu walipuuzia ujumbe wa onyo na mwisho wake waliangamia, Danieli naye anasema hivi 10Wengi watatakaswa na kuondolewa mawaa na kuwa safi, lakini waovu wataendelea kuwa waovu. Hakuna mmoja wa waovu atakayefahamu, lakini wale wenye hekima watafahamu.(Danieli 12:10). Watakaofahamu ni wale wenye hekima ya neon la Mungu, lakini waovu hawataelewa, wakipewa ujumbe wa onyo juu ya mwisho wa dunia watakuja na maneno haya 3Kwanza kabisa ni lazima mfahamu ya kwamba siku za mwisho watakuja watu wenye dhihaka wakidhihaki na kuzifuata tamaa zao mbaya. 4na kusema, Iko wapi ile ahadi ya kuja Kwake? Tangu baba zetu walipokufa, kila kitu kinaendelea kama kilivyokuwa tangu mwanzo wa kuumbwa. 5Wao kwa makusudi hupuza ukweli huu, ya kwamba kwa neno la Mungu mbingu zilikuwepo tangu zamani nayo dunia ilifanyizwa kutoka ndani ya maji na kwa hayo maji(2 Petro 3:3-5),. Nawatakia siku njema, mbarikiwe. NB: Nukuu zote ni kutoka Biblia takatifu, toleo la Kiswahili cha kisasa.