Wanadiplomasia Wabobezi wameanza kupotea na ni adimu sana Tanzania miaka hii ya karibuni

Sasa wakaze fuvu na wakati nafasi zenye stream za maokoto hazihitaji hiyo seriousness. Ukilamba watu miguu unafika mbali hata kama una uwezo hafifu

Na ukitofautiana na wateuzi hata kama umetoa wazo bora lakn liko tofauti nao unakaa kando
 
Mkuu Jidu, Jidu La Mabambasi , naunga mkono hoja, Kumbe watu wa Nyerere bado wapo na wana misimamo kama Nyerere. Hongera MFA, Dr. Mahiga kwa msimamo, tusikubali kuyumbishwa

Ni kweli, naunga mkono hoja, wengine wanateuliwa ubalozi na kupostiwa nje ili tuu kupunguza kelele!, wengine wanapostiwa nje kuondoa kiwingu, wale ma DGIS!.

Hili nimelizungumza hapa Ijue Hadhi ya Ubalozi, its Rights & Privileges. Wajua Kufutwa Ubalozi Dr. Slaa Hakutokani na Ukosoaji wa Bandari na Anaweza Kurejeshewa Ubalozi Wake?

Hatuna!. Labda yule dogo kule Asia

The good one aliyepo ni Balozi Mulamula, ndio hivyo tena, alipoondolewa hatukuelezwa sababu, as if uteuzi wa a carrier diplomats ni hisani ya rais aliyepo madarakani!. It's not!. Mabalozi wa kuteuliwa kwa hisani ya rais, yes waendelee kuteuliwa lakini mabalozi wa carrier diplomats waendelee kupikwa, huwezi kuwatetegea mabalozi hisani tuu na kuwaondoa carrier diplomats kwa majungu majungu!. Nimeuliza hapa Should We Demand More Right to Information Kwenye Teuzi za Key Posts? Ziwe Endorsed na Bunge With Security of Tenure? Mawaziri Wasiwe Wabunge?
P
Umeongea sahihi tunahitaji Bunge kuridhia baadhi ya teuzi za Rais. Lakini shida ya Bunge letu wanajikomba kwa Rais. Bunge la Tanzania halina uwezo wa kukataa anachopendekeza Rais.

Shida inakuja Rais ndo mwenyekiti wa Chama, atakae pinga ataadhibiwa. Hivyo hata Rais ateuwe na kupeleka Bungeni mtu asiyefaa, bunge litasema NDIYOOO!

Tanzania tunatakiwa kuunda mfumo mpwa wa nchi na hata wakitumishi. Nchi sikuhizi haiandai watu kama zamani. Yaani kwasasa ukiwa chawa tu haijalishi unasifa gani basi unateuliwa.

Zamani watu walipikwa. Nakumbuka hata usalama wa Taifa uliweza kufatilia watu toka wanavyokuwa shuleni hadi chuo. Na kisha kuwaandaa hawa watu hata wao bila kujua kama wanaandaliwa.

Taifa limekosa watu ambao ni makini, ukimtazama unaona utofauti, unaona uzalendo, kujituma, upevu wa uongozi, hekima na ujasiri, usikivu na unyenyekevu ndani yake. Hawa watu waweza kuwepo lakini hawapo kwenye system au mfumo.

Nyerere alifanya kazi na hata watu waliompinga, na aliwasikiliza. Lakini leo ukiongea hoja ikaonesha huko kinyume na Rais basi wewe unafurushwa, hata hoja yako iwe na umakini utaondolewa tu.

Utawala wetu unataka chawa, vijana watakao sifia hata ujinga.
 
Bunge ndilo linawajibu na linatakiwa kuisimamia serikali, hivyo serikali inapopeleka madudu Bungeni, Bunge linawajibu wa kuirekebisha serikali. Kama hiki kilichotokea kwenye IGA ya DPW na Bandari zetu, ni aibu kwa Bunge letu Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!
P
 
Mkuu Jidu, Jidu La Mabambasi , naunga mkono hoja, Kumbe watu wa Nyerere bado wapo na wana misimamo kama Nyerere. Hongera MFA, Dr. Mahiga kwa msimamo, tusikubali kuyumbishwa

Ni kweli, naunga mkono hoja, wengine wanateuliwa ubalozi na kupostiwa nje ili tuu kupunguza kelele!, wengine wanapostiwa nje kuondoa kiwingu, wale ma DGIS!.

Hili nimelizungumza hapa Ijue Hadhi ya Ubalozi, its Rights & Privileges. Wajua Kufutwa Ubalozi Dr. Slaa Hakutokani na Ukosoaji wa Bandari na Anaweza Kurejeshewa Ubalozi Wake?

Hatuna!. Labda yule dogo kule Asia

The good one aliyepo ni Balozi Mulamula, ndio hivyo tena, alipoondolewa hatukuelezwa sababu, as if uteuzi wa a carrier diplomats ni hisani ya rais aliyepo madarakani!. It's not!. Mabalozi wa kuteuliwa kwa hisani ya rais, yes waendelee kuteuliwa lakini mabalozi wa carrier diplomats waendelee kupikwa, huwezi kuwatetegea mabalozi hisani tuu na kuwaondoa carrier diplomats kwa majungu majungu!. Nimeuliza hapa Should We Demand More Right to Information Kwenye Teuzi za Key Posts? Ziwe Endorsed na Bunge With Security of Tenure? Mawaziri Wasiwe Wabunge?
P
Mkuu P, umechambua kisawasawa.
 
Pamoja na yote zama nazo zimebadilika.....

Mathalani komredi El Commandante Salim A.Salim ni kizazi cha wapigania UHURU wa Zanzibar/Tanganyika.....

Kilikuwa ni kipindi cha mapambano ya kusimama kama TAIFA.....akakutana na siasa za KIJAMAA zenye upande mkubwa tu duniani.....

Akajitupa "miguuni" mwa siasa hizo.......

Upande wa pili ,China ikataka kuondolewa UANACHAMA wa baraza la usalama la umoja wa mataifa.....El Commandante Salim A.Salim akapambana kuhakikisha kiti cha CHINA hakipokwi hiyo nafasi.....

Leo hii ni yeye pekee aliye mshindi wa tuzo ya HESHIMA YA MARAFIKI WA CHINA BARANI AFRIKA....

Hakuna mwafrika mwingine aliyetunukiwa hivyo[emoji2956][emoji7][emoji7]

#Siempre Mwanadiplomasia El Commandante Salim Ahmed Salim[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Kidiplomasia, Salim Amed Salim alifikia viwango ambavyo ni vya juu sana kufikiwa na mtanzania yeyote so far.
 
..kuna Prof.Anna Tibaijuka aliongoza UN-Habitat sijui kwanini hamjamtaja.

..pia Dr.Stergomena Tax aliongoza SADC naye hamjamtaja.

..Balozi Anthony Nyaki muwakilishi maalum wa UN Liberia.

..Lt.Gen.Paul Mella Mkuu wa vikosi umoja wa mataifa vya kulinda amani Darfur.

..Jaji Mohamed Chande Othman muendesha mashtaka mkuu East Timor, muendesha mashtaka Tribunal ya Rwanda, na mjumbe wa tume mbalimbali za uchunguzi za UN.

..Jaji James Kateka aliyehudumu Mahakama ya kimataifa ya masuala ya bahari.

..Jaji William Sekule aliyehudumu un tribunal za Rwanda na Yugoslavia.

..Jaji Steven Bwana alipata kuwa Jaji Mkuu wa mahakama ya Rufani ya Seychelles.
 
Umeongea sahihi tunahitaji Bunge kuridhia baadhi ya teuzi za Rais. Lakini shida ya Bunge letu wanajikomba kwa Rais. Bunge la Tanzania halina uwezo wa kukataa anachopendekeza Rais.

Shida inakuja Rais ndo mwenyekiti wa Chama, atakae pinga ataadhibiwa. Hivyo hata Rais ateuwe na kupeleka Bungeni mtu asiyefaa, bunge litasema NDIYOOO!

Tanzania tunatakiwa kuunda mfumo mpwa wa nchi na hata wakitumishi. Nchi sikuhizi haiandai watu kama zamani. Yaani kwasasa ukiwa chawa tu haijalishi unasifa gani basi unateuliwa.

Zamani watu walipikwa. Nakumbuka hata usalama wa Taifa uliweza kufatilia watu toka wanavyokuwa shuleni hadi chuo. Na kisha kuwaandaa hawa watu hata wao bila kujua kama wanaandaliwa.

Taifa limekosa watu ambao ni makini, ukimtazama unaona utofauti, unaona uzalendo, kujituma, upevu wa uongozi, hekima na ujasiri, usikivu na unyenyekevu ndani yake. Hawa watu waweza kuwepo lakini hawapo kwenye system au mfumo.

Nyerere alifanya kazi na hata watu waliompinga, na aliwasikiliza. Lakini leo ukiongea hoja ikaonesha huko kinyume na Rais basi wewe unafurushwa, hata hoja yako iwe na umakini utaondolewa tu.

Utawala wetu unataka chawa, vijana watakao sifia hata ujinga.
Unachokisema ni kweli kabisa! Kwa mtazamo wangu, ili kumaliza tatizo hili ni muhimu kuelewa chanzo chake ni nini.

Kwanza naheshimu sana ndugu Paskal Mayalla kwa hili, siku ndugu Paskal Mayalla aliyomuuliza mwendazake kuwa katoa wapi mamlaka kuingilia mihimili mingine, akajibiwa kwa kejeli kuwa serikali imejichimbia zaidi. Pale ndio ulikuwa mwanzo wa kudhoofisha mihimili mwili ya dola.

Pili, ilikuwa ni hatua ya kuwapa wakuu wa mihimili hiyo Kinga ya kutokushtakiwa. Baada ya pale mihimili ikaanza kutetea na kula sahani moja serikali badala ya kuisimamia.

Tusiporudi nyuma na kuangalia tulipo jikwaa, na tukarekebisha, tukang'ang'ania kuangalia tulipoangukia, tutabaki kulalama daima.
 
..kuna Prof.Anna Tibaijuka aliongoza UN-Habitat sijui kwanini hamjamtaja.

..pia Dr.Stergomena Tax aliongoza SADC naye hamjamtaja.

..Balozi Anthony Nyaki muwakilishi maalum wa UN Liberia.

..Lt.Gen.Paul Mella Mkuu wa vikosi umoja wa mataifa vya kulinda amani Darfur.

..Jaji Mohamed Chande Othman muendesha mashtaka mkuu East Timor, muendesha mashtaka Tribunal ya Rwanda, na mjumbe wa tume mbalimbali za uchunguzi za UN.

..Jaji James Kateka aliyehudumu Mahakama ya kimataifa ya masuala ya bahari.

..Jaji William Sekule aliyehudumu un tribunal za Rwanda na Yugoslavia.

..Jaji Steven Bwana alipata kuwa Jaji Mkuu wa mahakama ya Rufani ya Seychelles.
Mkuu asante, hapo nitamchukua Prof Anna Tibaijuka kati ya hao wote.
Aniwie radhi kwa kutomtaja lakini tunaona the fine tuned calibre ya wanadiplomasia tuliokuwa nao.
 
..hawakuwa wakibebwa na Mwalimu Nyerere?

..Watanzania wanaoweza kuwa Katibu Mkuu UN ni wale waliolelewa kitaaluma ndani ya mashirika ya kimataifa kama UN, WB, IMF, Commonwealth Secretariat, etc.
Mkuu kubebwa kwa vipi tena?
Kuwa trained ,yes.
Mwanadiplomasia mbonevu anapikwa na kupikika.
Wainhereza wanasema a diplomat is a foreign service officer sent to lie gracefully for his country.
In so doing anaiokoa nchi yake kimahusiano na nchi nyingine.
 
Back
Top Bottom