Wanadiplomasia Wabobezi wameanza kupotea na ni adimu sana Tanzania miaka hii ya karibuni

Wajanja wamevuruga career pathways ili kuchomeka watu wao. Ubalozi kwa mfano umekuwa kwa kiasi kikubwa ni zawadi au "kaa mbali" badala kupanda ngazi.
Inasikitisha sana.
Siku hizi watu wanateuliwa mabalozi hawajawahi kukanyaga hata Wizara ya mambo ya nje!
 
..Rais wa Tz ndiye mwanadiplomasia namba wani.

..Sasa Rais akipwaya na akiwa hana maono kama mwanadiplomasia basi hawa wa chini yake mwanapwaya.

..Hivi unafikiri Salim Salim angefanya kazi ktk awamu ya Magufuli angejulikana kwa kiwango alichofikia?
Mwalimu wanted the right people to be active in taking decisions and actions. Alimlinda Salim toka akiwa mdogo maana kule kwao, mbabe wa mapinduzi alikuwa na allergy na hawa wasomi wa enzi zile.
Na Salim hakumuangusha Mwalimu. It is sad, baadae wasaka tonge wakamletea mambo ya hovyo kabisa ili asiweze kuwa Rais. Na kwakweli haya yanayoendelea...tunavuna tuliyopanda.
Maana inaweza kutokea siku hata mbumbumbu mzungu wa reli akatwaa jackport bingo kama haya mambo ya kusukuma watoto, marafiki na wapendwa wetu ambao wengine hawana sifa kabisa za uongozi, yataendelea hivi
 
..Rais wa Tz ndiye mwanadiplomasia namba wani.

..Sasa Rais akipwaya na akiwa hana maono kama mwanadiplomasia basi hawa wa chini yake mwanapwaya.

..Hivi unafikiri Salim Salim angefanya kazi ktk awamu ya Magufuli angejulikana kwa kiwango alichofikia?
Mkuu Rais kweli ni diplomat no 1 katika nchi yoyote.
Lakini yeye Rais anapimwa kwa vigezo tofauti kabisa na vingi sana.
Rsis hatachaguliwa kwa vile kawapatanisha A na B, bali mustakabali wa maisha ya waliomchagua kuwa imeboreka na maisha ni mazuri zaidi.
 

..Uko sahihi 100%.

..Na Raisi wa Tz asipokuwa mwanadiplomasia mzuri, na asipoelewa siasa na mahusiano ya kimataifa, anaweza kuitia nchi HASARA kubwa na kuharibu uchumi wa nchi.
 

..Msielekeze lawama zote kwa genge la wanamtandao.

..Yeye Salim Salim alishindwa nini kujitetea ili kulinda hheshima na rekodi yake?

..Kuna taarifa kwamba Mzee Mkapa alimtaka Salim Salim arejee nchini awe Makamu wa Rais baada ya Dr.Omari Ali Juma kufariki.

..Sasa inasemekana Salim Salim alisita kufanya hivyo. Lakini kama angekubali maana yake yeye ndiye angekuwa na nafasi kubwa kumrithi Mzee Mkapa.

..Katika mazingira hayo hivi mnaweza kuwashushia lawama wanamtandao kwa asilimia 100?

NB:

..kule UN wakati aligombea kuwa Katibu Mkuu alipewa nafasi ya kwenda kumshawishi Balozi wa Marekani UN, lakini hakutumia nafasi hiyo. Sasa alipopigiwa kura ya VETO mtawalaumu Wamarekani?

Cc Nguruvi3, Pascal Mayalla
 
Wakati mwingine diplomasia ina mapungufu yake.
Mtu ukiwa too diplomatic, unachukuliwa kama weakness.

Siasa za nchi zetu hizi kuchimbana kwingi sana.
Salim A, Salim hakutegemea kuwa wenzake serikalini wamfitini kwa habari za kumchafua.
Hili vile vile lilitokea kwa Prof Mwandosya kwa kuenezewa habari kuwa amekula rushwa kwa kusomeshewa mtoto wate chuo kikuu South Africa.

Hizi ni dhambi za mtandao zilizoharibu moja ndani ya chama na kwa watu kama Salim Ahmed Salim alijiondoa kabisa kutoka local politics.
 

..kuchafuana ni utamaduni wa siasa za Tanzania, nadhani toka enzi za Tanganyika na Tanu.

..Salim Salim na Mwandosya ni wahanga wa juzijuzi wa siasa za kuzushiana na kuchafuana.

..Unaweza kurudi nyuma mpaka kwa wakina Chifu Marealle, Sheikh Takadiri, Oscar Kambona, ..wote hao walizushiwa mambo ya uongo ili aonekane wabaya na wachafu mbele ya jamii.

..Kwa mfano, Marealle alizushiwa kwamba alitaka uhuru kwa Wachagga tu, na sio Watanganyika. Habari hiyo ilienezwa na kwasababu Watanzania sio watu waasisi wakaikubali. Na kuna chuki dhidi ya Wachagga kutokana na uongo huo.

..Kuna ushahidi wa nyaraka za kumbukumbu za vikao vya Umoja wa Mataifa ambavyo Chifu Marealle alishiriki na zinathibitisha kwamba alidai uhuru wa WATANGANYIKA wote. Marealle hakubagua.

..Mambo hayo ya kuchafuana na kuzushiana yaliasisiwa na Tanu na yameendelezwa na Ccm na yapo mpaka leo hii yakielekezwa kwa wapinzani.
 

..Mimi naiona kama ni weakness kwa upande wa Salim Salim kushindwa kuwashughulikia kwa hoja watu waliokuwa wakimchafua.

..Kwa maoni yangu amezidiwa na watu wadogo kama Tundu Lissu, Mdude Nyagali, na wengine ambao wamefanyiwa mambo mabaya sana lakini hawakujikunyata na kusalimu amri kwa watesi wao.
 
Watu wengine yaani mtu anakurupuka kujibu hata aelewi hivi ni wapi nimeandika au kuhusianisha na nchi za nje au Kenya.
Nadhani uelewi kinachoongelewa. Kama umezaliwa miaka ya 2000 hutojua kakae darasani ufundishwe. Vijana wa siku hizi shida sana katika kufikiri na kujibu hoja.
 

..unaweza kupata Rais anayetuma wanadiplomasia kuzodoa na kufokea mataifa mengine na marafiki zetu huko nje kama Tz ilivyokuwa kati ya 2015 na 2020.
 
Mimi nitaliweka tofauti.
Salim Ahmed Salim alikuwa na bado ni mtu wa intergrity.
Ame sustain moral high ground na hakushuka kuwa level moja na waliomchafua.
Leo hata akikaa meza moja na waliomchafua , Salim anajitokeza kama mtu muungwana sana.

Heshima ya Balozi Salim Ahmed Salim haijawahi kutetereka, he is a living legend.
 
Anao sasa huo uwezo wa kuelewa!!??
 
Tuimne sifa za watu waliolitumikia Taifa kabla hawajspotea.
Salim ni mfano mzuri.
Kuna vijana kina Balozi Kairuki sasa hivi wanafanya vizuri.
 

Napenda maarifa yako. Inasemekana aligoma pia kwa Nyerere kabla ya Nyerere kuwekeza kwa Mkapa. Inasemekana pia kulikuwa na kivuli fulani cha nguvu za Maalimu ambazo wakati ule ilikuwa ngumu kujua nani ni nani.

Shida ya sisi watanzania tunapenda sana umbea. Sijui kama haya yana ukweli au ni hadithi noo utamu kolea
 

..Salim Salim ameshindwa hata na kijana mdogo Mdude Nyagali ambaye hakukubali kusalimu amri kwa wahuni waliokuwa wakimtesa.
 


Hawa hata kuitwa diplomats hawafai

1: Mulamula ❌❌❌❌❌❌❌
2: Anna Tibaijuka ❌❌❌❌❌❌❌
 
Tukusaidie vipi, maana ulivyo andika ni umbeya wenyewe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…