Wanafunzi 22 wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Shinyanga kuzuiwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita 2021

Brother hawa 22 tunaojadili hapa eti wamezuiwa kabisa kufanya mtihani kwa kile kinaitwa ndiyo waliondaa hizo fujo. Zaidi ya hapo wamepewa jinai polisi Kishapu.
Unajua binafsi imenifikirisha mno,hivi makosa ya watoto shuleni yote yakifuatiliwa ktk misingi ya kijinai si ni lazima yatasomeka jinai tu!!!? Uamuzi wa hasira tu umefanywa.
 
Mwenzetu katoa ushauri katika uelewa wake,pengine saidia kuuboresha ushauri kaka ili tuwasaidie hawa watoto!
Mimi ni Mwalimu ,naunga mkono hoja ya hao watoto kufukuzwa,tena ikibidi wapelekwe mahakamani wakabiliwe na shitaka la uharibifu Wa Mali za umma.

Waambie pumbavu zao
 
Peer pressure kwa vijana hawa iangaliwe..amsha amsha za advanced zinawachotaga hata vijana wapole kabisa.

Walipe gharama za kumnunulia mwalimu gari na kama kuna miundombinu wameiharibu wafidie.
 
Shule nyingi zinavunja haki za binadamu specifically haki za watoto. Mfano mwingine ni huu. Utakuta hata hawakupewa haki ya kusikilizwa na hii ndio itakuwa pona yao wakienda kudai haki yao.

Mfano mwingine ni ule wa kumchapa mwanafunzi kisa hajalipiwa ada na mzazi wake au mzazi hajaudhuria kikao cha shule, hii nayo huwa sielewi waalimu wanawazaga nini kumudhibu mtoto kwa kosa la mzazi wake.

Tumeishi kwa mazoea hadi tunaona ni sawa. Na taasisi zipo zinakaa kimya.

Hao wanafunzi wachukue hatua kimahakama itasaidia kuweka mambo sawa.
 
Peer pressure kwa vijana hawa iangaliwe..amsha amsha za advanced zinawachotaga hata vijana wapole kabisa.

Walipe gharama za kumnunulia mwalimu gari na kama kuna miundombinu wameiharibu wafidie.
Na hicho ndiyo kilichoombwa na wazazi wakifanye ilimradi watoto wao waruhusiwe kuendelea.
 
ᖴᑌKᑌᘔᗩ KᗩᗷIᔕᗩ ᕼᗩYO ᗰᗩᒍᗩᗰᗷᗩᘔI Kᑌᑎᗩ ᗰIᗩKᗩ Yᗩ ᑎYᑌᗰᗩ ᗰᗩᒍᗩᗰᗷᗩᘔI Kᗩᗰᗩ ᕼᗩYO YᗩᒪIᗯᗩᕼI KᑌᔕᗩᗷᗩᗷIᔕᕼᗩ ᔕᕼᑌᒪE Yᗩ Tᗩᗰᗷᗩᘔᗩ KᑌᖴᑌᑎGᗯᗩ Kᗯᗩ ᐯITEᑎᗪO ᐯYᗩ Kᑌᑌᗩ ᖴOᖇᗰ OᑎE ᗷᗩᗩᗪᕼI YᗩᒪIᖴᑌKᑌᘔᗯᗩ ᑎᗩ ᗷᗩᗩᗪᕼI YᗩᒪIᕼᗩᗰIᔕᕼIᗯᗩ ᔕᕼᑌᒪE ᑎYIᑎGIᑎE ᗰEᑎGI YᗩᒪIKᗯEᑎᗪᗩ KᑌᖴᑌKᑌᘔᗯᗩ
 
Kweli kabisa mkuu...maana kuwakataza wasifanye mtihani ni kuongeza tatizo lingine pasipo kutatua tatizo la awali...
Huu ni uamuzi wa hovyo kabisa!
Gari inayosemekana kuharibiwa tayari ilishalipiwa pesa kwa faini ya tshs. 35,000/= iliyoamriwa na bodi kulipwa kwa kila mtoto wa kidato cha sita isipokuwa hawa ambao eti ndiyo mobilizers!
 
Hongera,but siku yakikutokea ndiyo utajua unless uwe maksai
 
Peer pressure kwa vijana hawa iangaliwe..amsha amsha za advanced zinawachotaga hata vijana wapole kabisa.

Walipe gharama za kumnunulia mwalimu gari na kama kuna miundombinu wameiharibu wafidie.
Ni bro,lkn utashangaa uamuzi uliochukuliwa hapo!!
 
Huzuiwi kuutumia ulimi wako brother as long as MUNGU alishaijua hasara aliyoiingia ya kuukupa!

Hao kwanza walitakiwa kula fimbo kabla ya kufurushwa kwenda vijijini kwao wakalime!
 
HEKIMA ZITUMIKE
 
Waongee na baraza la mitihani. Yaani, waulize baraza la mitihani kama wanaweza fanya mitihani. Kama jibu ni ndio, basi baraza litawapa maelekezo. Yaani mchakato huu uanze sasa badala ya kuendelea kuongea humu.
 
Mkuu tunasimamia sheria tumechelewa mnooo na mshirika mkubwa wa kufeli ni ukosefu wa nidhamu kama kweli ni wakosaji naunga mkono hoja

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…