Wanafunzi 22 wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Shinyanga kuzuiwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita 2021

Wanafunzi 22 wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Shinyanga kuzuiwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita 2021

Mimi ni mdau katika masuala ya elimu.Najua kwamba mwanafunzi hata akifukuzwa ilimradi alisajiliwa lazima afanye mtihani.Sielewi unaposema kuwa wapo ambao wamefukuzwa halafu wameruhusiwa kuja kufanya mtihani na wapo ambao hawaruhusiwi.Hicho kitu hakipo katika sheria za Necta za sasa hivi.Kwenye shule kuna "suspension" na "expulsion".
Suspension- mwanafunzi anapfukuzwa kwa muda fulani labda wiki 2 au mwezi halafu anarudi shuleni.
Expulsion- mwanafunzi anafukuzwa shule moja kwa moja.Ila kama ni wa darasa la mtihani na amesajiliwa ni lazima arudi kufanya mtihani katika kituo chake.hapo atakuwa anatoka nyumbani anaingia shuleni moja kwa moja kwenye chumba cha mtihani akimaliza anatoka tena nje ya mazingira ya shule.
Hivyo mtoa mada labda hajaelewa vizuri.Inawezekana hao wengine walipewa suspension tu na wengine expulsion, lakini wote wanatakiwa kufanya mitihani.
Brother hawa 22 tunaojadili hapa eti wamezuiwa kabisa kufanya mtihani kwa kile kinaitwa ndiyo waliondaa hizo fujo. Zaidi ya hapo wamepewa jinai polisi Kishapu.
Unajua binafsi imenifikirisha mno,hivi makosa ya watoto shuleni yote yakifuatiliwa ktk misingi ya kijinai si ni lazima yatasomeka jinai tu!!!? Uamuzi wa hasira tu umefanywa.
 
Mwenzetu katoa ushauri katika uelewa wake,pengine saidia kuuboresha ushauri kaka ili tuwasaidie hawa watoto!
Mimi ni Mwalimu ,naunga mkono hoja ya hao watoto kufukuzwa,tena ikibidi wapelekwe mahakamani wakabiliwe na shitaka la uharibifu Wa Mali za umma.

Waambie pumbavu zao
 
Peer pressure kwa vijana hawa iangaliwe..amsha amsha za advanced zinawachotaga hata vijana wapole kabisa.

Walipe gharama za kumnunulia mwalimu gari na kama kuna miundombinu wameiharibu wafidie.
 
Shule nyingi zinavunja haki za binadamu specifically haki za watoto. Mfano mwingine ni huu. Utakuta hata hawakupewa haki ya kusikilizwa na hii ndio itakuwa pona yao wakienda kudai haki yao.

Mfano mwingine ni ule wa kumchapa mwanafunzi kisa hajalipiwa ada na mzazi wake au mzazi hajaudhuria kikao cha shule, hii nayo huwa sielewi waalimu wanawazaga nini kumudhibu mtoto kwa kosa la mzazi wake.

Tumeishi kwa mazoea hadi tunaona ni sawa. Na taasisi zipo zinakaa kimya.

Hao wanafunzi wachukue hatua kimahakama itasaidia kuweka mambo sawa.
 
Peer pressure kwa vijana hawa iangaliwe..amsha amsha za advanced zinawachotaga hata vijana wapole kabisa.

Walipe gharama za kumnunulia mwalimu gari na kama kuna miundombinu wameiharibu wafidie.
Na hicho ndiyo kilichoombwa na wazazi wakifanye ilimradi watoto wao waruhusiwe kuendelea.
 
ᖴᑌKᑌᘔᗩ KᗩᗷIᔕᗩ ᕼᗩYO ᗰᗩᒍᗩᗰᗷᗩᘔI Kᑌᑎᗩ ᗰIᗩKᗩ Yᗩ ᑎYᑌᗰᗩ ᗰᗩᒍᗩᗰᗷᗩᘔI Kᗩᗰᗩ ᕼᗩYO YᗩᒪIᗯᗩᕼI KᑌᔕᗩᗷᗩᗷIᔕᕼᗩ ᔕᕼᑌᒪE Yᗩ Tᗩᗰᗷᗩᘔᗩ KᑌᖴᑌᑎGᗯᗩ Kᗯᗩ ᐯITEᑎᗪO ᐯYᗩ Kᑌᑌᗩ ᖴOᖇᗰ OᑎE ᗷᗩᗩᗪᕼI YᗩᒪIᖴᑌKᑌᘔᗯᗩ ᑎᗩ ᗷᗩᗩᗪᕼI YᗩᒪIᕼᗩᗰIᔕᕼIᗯᗩ ᔕᕼᑌᒪE ᑎYIᑎGIᑎE ᗰEᑎGI YᗩᒪIKᗯEᑎᗪᗩ KᑌᖴᑌKᑌᘔᗯᗩ
 
Kweli kabisa mkuu...maana kuwakataza wasifanye mtihani ni kuongeza tatizo lingine pasipo kutatua tatizo la awali...
Huu ni uamuzi wa hovyo kabisa!
Gari inayosemekana kuharibiwa tayari ilishalipiwa pesa kwa faini ya tshs. 35,000/= iliyoamriwa na bodi kulipwa kwa kila mtoto wa kidato cha sita isipokuwa hawa ambao eti ndiyo mobilizers!
 
ᖴᑌKᑌᘔᗩ KᗩᗷIᔕᗩ ᕼᗩYO ᗰᗩᒍᗩᗰᗷᗩᘔI Kᑌᑎᗩ ᗰIᗩKᗩ Yᗩ ᑎYᑌᗰᗩ ᗰᗩᒍᗩᗰᗷᗩᘔI Kᗩᗰᗩ ᕼᗩYO YᗩᒪIᗯᗩᕼI KᑌᔕᗩᗷᗩᗷIᔕᕼᗩ ᔕᕼᑌᒪE Yᗩ Tᗩᗰᗷᗩᘔᗩ KᑌᖴᑌᑎGᗯᗩ Kᗯᗩ ᐯITEᑎᗪO ᐯYᗩ Kᑌᑌᗩ ᖴOᖇᗰ OᑎE ᗷᗩᗩᗪᕼI YᗩᒪIᖴᑌKᑌᘔᗯᗩ ᑎᗩ ᗷᗩᗩᗪᕼI YᗩᒪIᕼᗩᗰIᔕᕼIᗯᗩ ᔕᕼᑌᒪE ᑎYIᑎGIᑎE ᗰEᑎGI YᗩᒪIKᗯEᑎᗪᗩ KᑌᖴᑌKᑌᘔᗯᗩ
Hongera,but siku yakikutokea ndiyo utajua unless uwe maksai
 
Peer pressure kwa vijana hawa iangaliwe..amsha amsha za advanced zinawachotaga hata vijana wapole kabisa.

Walipe gharama za kumnunulia mwalimu gari na kama kuna miundombinu wameiharibu wafidie.
Ni bro,lkn utashangaa uamuzi uliochukuliwa hapo!!
 
Kuna taarifa kuwa Wanafunzi 22 wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya Shinyanga maarufu kama Shybush, wamefukuzwa shule na kuzuiwa kufanya mtihani wa kidato cha sita unaotarajiwa kuanza mapema mwezi wa tano.

Taarifa zaidi zinadai kuwa sababu kubwa ni fujo iliyotokea shuleni hapo mwezi March ambapo wanafunzi waliharibu gari la Mwalimu,na hivyo kupelekea bodi ya shule hiyo kukutana na kuamua wanafunzi hao wachukuliwe hatua hiyo.

Sambamba na hao,pia wapo wengine zaidi ya 30 ambao walirejeshwa makwao na wataruhusiwa kufanya mitihani yao wakitokea makwao.

Binafsi niwaombe wataalamu wa sheria wanisaidie ufafanuzi wa juu ya "Waraka wa Elimu No. 13" uliotumiwa na bodi ya shule hiyo kuondoa haki ya vijana hao kufanya mtihani na kupelekea vilio na majonzi kwa wazazi na walezi.
HEKIMA ZITUMIKE
 
Sasa ndiyo weshafukuzwa na nasikia hata RC amebariki uamuzi wa bodi ya shule,wataufanyaje huo mtihani. Tuwaelekeze wakimbilie wapi ili wasaidike

Pengine uwe ndiyo msaada pekee jamani. Unajua ukiwawazia vijana wenyewe unaona km wanafanya ujinga ule kwa sabb tu ya peer pressure ambayo always haimpi mhusika nafas ya kuwazia matokeo baada ya tukio wanaloshiriki. Lakini madhara zaidi utayakuta kwa wazazi wa watoto hawa. Wengne wamejichimba mfukoni kuwaandaa kwa gharama kubwa kupitia shule binafsi,leo mtoto kafikia hatua ambayo mzazi anawazia aanze kupumua,ghafla analetewa taarifa ya mtoto kufukuzwa shule na mbaya zaidi hadi aondolewe ktk mfumo rasmi wa elimu!!
NADHANI WAHUSIKA WAONE SABABU YA KUSAIDIA HILI SUALA JAMANI.
Waongee na baraza la mitihani. Yaani, waulize baraza la mitihani kama wanaweza fanya mitihani. Kama jibu ni ndio, basi baraza litawapa maelekezo. Yaani mchakato huu uanze sasa badala ya kuendelea kuongea humu.
 
Kuna taarifa kuwa Wanafunzi 22 wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya Shinyanga maarufu kama Shybush, wamefukuzwa shule na kuzuiwa kufanya mtihani wa kidato cha sita unaotarajiwa kuanza mapema mwezi wa tano.

Taarifa zaidi zinadai kuwa sababu kubwa ni fujo iliyotokea shuleni hapo mwezi March ambapo wanafunzi waliharibu gari la Mwalimu,na hivyo kupelekea bodi ya shule hiyo kukutana na kuamua wanafunzi hao wachukuliwe hatua hiyo.

Sambamba na hao,pia wapo wengine zaidi ya 30 ambao walirejeshwa makwao na wataruhusiwa kufanya mitihani yao wakitokea makwao.

Binafsi niwaombe wataalamu wa sheria wanisaidie ufafanuzi wa juu ya "Waraka wa Elimu No. 13" uliotumiwa na bodi ya shule hiyo kuondoa haki ya vijana hao kufanya mtihani na kupelekea vilio na majonzi kwa wazazi na walezi.
Mkuu tunasimamia sheria tumechelewa mnooo na mshirika mkubwa wa kufeli ni ukosefu wa nidhamu kama kweli ni wakosaji naunga mkono hoja

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom