Wanafunzi 22 wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Shinyanga kuzuiwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita 2021

Wanafunzi 22 wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Shinyanga kuzuiwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita 2021

Naifahamu sana shybush,ni moja Kati ya shule za wanafunzi wavuta bhangi, yaani kuna kipindi walivunjavunja thamani za shule,wenzao wakakamatwa na polisi,walikwenda kuvamia kituo cha polisi maganzo,ufupi hatutakiwi kuwatetea
Kwahiyo shule ndio inawafundisha utukutu na walimu wameshindwa kuwabadili tabia... Maana kila Mwaka Wanafunzi wanagraduate inakuwaje shule imaendelea kuitwa ya wakorofi au wao wanapangiwa walioshindikana?
 
Mahakaman hawajafikishwa but wamekaa mahabusu siku 3
Baada ya kutoka mahabusu wameambiwa nini polisi.
Mana huku niliko kuna wanafunzi wawili wa kidato cha sita wamefukuzwa shule baada ya kumfungia mwanafunzi wa kidato cha tano mmoja ndani na kumpa kipigo cha kutosha.
Wamepelekwa polisi na kukutwa na kosa la jinai ivyo wamefukuzwa shule na wapo hapa mtaani tangu wiki iliyopita.
 
Chanzo cha hizo fujo hapo ni nini?

Kwanini mliharibu Gari la mwalimu?

Enzi zangu nilikuaga mkorofi Shuleni ila sikua na huu upuuzi wakuharibu mali za Uma.
 
Duh! Mbona hatari hii jamani. Peer pressure kuideal sometime panahitajika matumizi ya hekima na busara zaidi kuliko sheria. Coz utaona kwene case hii wazazi ndiyo wanabaki na vilio zaidi.

Mpaka kikao cha bodi kinakaa ujue walishakanywa zaidi ya mara moja lakini bado wakarudia. Kuna wanafunzi ni wakorofi sana hata wasamehewe mara 100 bado hawabadiliki.
 
Kisheria mwanafunzi akishasajiliwa ni lazima afanye mtihani awe mahabusu/magereza,hospitali au hajalipa Ada ya shule.Kama ni watovu wanidhamu na wamefukuzwa Shule wana haki ya kufanya mtihani.Awamu ya JPM ilibadili mambo mengi ngoja tuone.
na mimba jpm alisema au unasema wewe
 
Kuna taarifa kuwa wanafunzi 22 wa kidato cha sita wa Shule ya Sekondari ya Shinyanga maarufu kama Shybush,wamefukuzwa shule na kuzuiwa kufanya mtihani wa kidato cha sita unaotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao wa tano.

Taarifa zaidi zinadai kuwa sababu kubwa ni fujo iliyotokea shuleni hapo mwezi March ambapo wanafunzi waliharibu gari la Mwalimu,na hivyo kupelekea bodi ya shule hiyo kukutana na kuamua wanafunzi hao wachukuliwe hatua hiyo.
Sambamba na hao,pia wapo wengine zaidi ya 30 ambao walirejeshwa makwao na wataruhusiwa kufanya mitihani yao wakitokea makwao.

Binafsi niwaombe wataalamu wa sheria wanisaidie ufafanuzi wa juu ya "Waraka wa Elimu No. 13" uliotumiwa na bodi ya shule hiyo kuondoa haki ya vijana hao kufanya mtihani na kupelekea vilio na majonzi kwa wazazi na walezi.

Kwa hiyo wewe unaona wana haki bila kuangalia utovu wa nidhamu na uharibifu walioufanya! Haki ywa mwanafunzi ni kifanya fujo shuleni! Wewe ni mpumbavu kabisa na si ajabu ni mmoja wa hao wajinga na majuha waliotimuliwa pale shuleni!
 
Kwahiyo shule ndio inawafundisha utukutu na walimu wameshindwa kuwabadili tabia... Maana kila Mwaka Wanafunzi wanagraduate inakuwaje shule imaendelea kuitwa ya wakorofi au wao wanapangiwa walioshindikana?
Hapana,haina ukweli kuwa wote wanaopangiwa kusoma pale ni wakorofi. Shule yenyewe inatengeneza ukorofi wa watoto,na ndiyo maana unasikia hapa kila mmoja anayeielewa anaisemea hilo. Brother,ktk fikra za kawaida kabisa,inatokeaje watoto waandamane usiku wa manane na had vipofu wakokotwe na wenzao pasipo staff kujua??? Na zaidi watembee km 15 shule bila taarifa...kweli!!!!?????
Niliuliza ulinzi nikaambiwa wapo walinzi 8. How it happen lightly like that??? Kuna tatizo serikali iiangalie hiyo shule!
 
Shida mleta mada kuna vitu hajaeleza.
Je Ilo kosa limefikishwa polisi na mahakamani Mana kufukuzwa shule ukishasajiliwa ni mpaka uwe na kosa la jinai.

Nyie hamjui tu, huyo mleta mada ni mmojawao wa hao wanafunzi waliotimliwa pale Shinyanga! Anatafuta huruma hapa!
 
Kwa hiyo wewe unaona wana haki bila kuangalia utovu wa nidhamu na uharibifu walioufanya! Haki ywa mwanafunzi ni kifanya fujo shuleni! Wewe ni mpumbavu kabisa na si ajabu ni mmoja wa hao wajinga na majuha waliotimuliwa pale shuleni!
Huzuiwi kuutumia ulimi wako brother as long as MUNGU alishaijua hasara aliyoiingia ya kuukupa!
 
Nyie hamjui tu, huyo mleta mada ni mmojawao wa hao wanafunzi waliotimliwa pale Shinyanga! Anatafuta huruma hapa!
Nishasemea hili,kuwa walikaa mahabusu siku 4 na upelelezi unaendelea.
 
Baada ya kutoka mahabusu wameambiwa nini polisi.
Mana huku niliko kuna wanafunzi wawili wa kidato cha sita wamefukuzwa shule baada ya kumfungia mwanafunzi wa kidato cha tano mmoja ndani na kumpa kipigo cha kutosha.
Wamepelekwa polisi na kukutwa na kosa la jinai ivyo wamefukuzwa shule na wapo hapa mtaani tangu wiki iliyopita.
Upelelezi unaendelea
 
Nyie hamjui tu, huyo mleta mada ni mmojawao wa hao wanafunzi waliotimliwa pale Shinyanga! Anatafuta huruma hapa!
Si lazima wote tuwe na uelewa mmoja,naheshimu ulichokisema lakini si kweli hivyo
 
Mpaka kikao cha bodi kinakaa ujue walishakanywa zaidi ya mara moja lakini bado wakarudia. Kuna wanafunzi ni wakorofi sana hata wasamehewe mara 100 bado hawabadiliki.
Huenda uko sahihi,lkn hebu wazia mzazi ambaye hajawahi kujulishwa utovu wa nidhamu wowote unaitiwa mtoto kufukuzwa tu....inauma sn
 
Huenda uko sahihi,lkn hebu wazia mzazi ambaye hajawahi kujulishwa utovu wa nidhamu wowote unaitiwa mtoto kufukuzwa tu....inauma sn

Inauma sana lakini naamini hakuna mzazi asiejua kuwa shuleni kuna sheria na kanuni za kufuata na endapo zikikiukwa zinaweza mfukuzisha mwanae shule.
 
Kuna taarifa kuwa wanafunzi 22 wa kidato cha sita wa Shule ya Sekondari ya Shinyanga maarufu kama Shybush,wamefukuzwa shule na kuzuiwa kufanya mtihani wa kidato cha sita unaotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao wa tano. Taarifa zaidi zinadai kuwa sababu kubwa ni fujo iliyotokea shuleni hapo mwezi March ambapo wanafunzi waliharibu gari la Mwalimu,na hivyo kupelekea bodi ya shule hiyo kukutana na kuamua wanafunzi hao wachukuliwe hatua hiyo. Sambamba na hao,pia wapo wengine zaidi ya 30 ambao walirejeshwa makwao na wataruhusiwa kufanya mitihani yao wakitokea makwao. Binafsi niwaombe wataalamu wa sheria wanisaidie ufafanuzi wa juu ya "Waraka wa Elimu No. 13" uliotumiwa na bodi ya shule hiyo kuondoa haki ya vijana hao kufanya mtihani na kupelekea vilio na majonzi kwa wazazi na walezi.
 
Mimi ni mdau katika masuala ya elimu.Najua kwamba mwanafunzi hata akifukuzwa ilimradi alisajiliwa lazima afanye mtihani.Sielewi unaposema kuwa wapo ambao wamefukuzwa halafu wameruhusiwa kuja kufanya mtihani na wapo ambao hawaruhusiwi.Hicho kitu hakipo katika sheria za Necta za sasa hivi.Kwenye shule kuna "suspension" na "expulsion".
Suspension- mwanafunzi anapfukuzwa kwa muda fulani labda wiki 2 au mwezi halafu anarudi shuleni.
Expulsion- mwanafunzi anafukuzwa shule moja kwa moja.Ila kama ni wa darasa la mtihani na amesajiliwa ni lazima arudi kufanya mtihani katika kituo chake.hapo atakuwa anatoka nyumbani anaingia shuleni moja kwa moja kwenye chumba cha mtihani akimaliza anatoka tena nje ya mazingira ya shule.
Hivyo mtoa mada labda hajaelewa vizuri.Inawezekana hao wengine walipewa suspension tu na wengine expulsion, lakini wote wanatakiwa kufanya mitihani.
 
Mwanafunzi aliyefanya kosa la jinai haruhusiwi kufanya mtihani
 
Back
Top Bottom