Wanafunzi Dar na Dharau kwa Wakubwa Wao

Inategemea na malezi , wazazi wengi wa Dar wana lugha chafu yaani mzazi anaongea Lugha chafu mbele ya watoto mwisho wa Siku mtoto anajionea ni lugha ya kawaida tu.
 
Kizazi cha nyakati za mwisho hiki.
 
Mtu mzima ukishapanda kwny usafiri wa umma inabidi nawewe uache kuwaambia watu wakupishe siti ukiona mwanafunzi hataki kusimama achana nae,hawa watoto nao wanachoka jamani
Hata sisi tulikuwa tunachoka hivyo hivyo na bado tuliwapisha, Nini siku hizi daladaal za kumwaga sisi ilikuwa unasimama kituoni kama saa nzima au mawili maana barabara yenyewe ilikuwa ni moja sasa hiyo foleni yake, likifika mnagombea hadi ukiingia kwenye gari inabidi upumzike kidogo ili network irudi mara unaona mzee kasimama inabidi umuite aje akae, mitoto ya siku hizi adabu ni ziro, tena ingekuwa enzi zetu huyo Mtoto angetandikwa vibao vya mdomo humo humo kwenye kwenye daladala na akifika nyumbani hasemi maana atapigwa tena
 
Aisee hizi tabia za wanafunzi wa dar wanazipata kutoka kwa kaka zao wanaume wa dar...nao wanamajibu ya ovyo sana
Hi tabia ipo nchi nzima wala si Dar pekee ndio sababu ya kuharibikiwa kwao maana hata ukimkuta anafanya kosa ambalo labda yeye hajui kama ni kosa hakuna wa kumwambia kwa kuogopa kutukanwa
 
Tatizo ni sisi wazazi, tusimrushie sana mawe huyo kijana/binti. Wazazi tulio wengi tumesahau kulea, tunachojua ni kuzisaka pesa.
 
Kwahiyo uyo mama yupo kwenye siti then anamwambia mwanafunzi ndio apishe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…