Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kizazi cha nyakati za mwisho hiki.Leo kwenye daladala kuna mama alimwambia mwanafunzi ampishe mzee akae. Yule mwanafunzi badala ya kujibu kistaarabu labda mama nimechoka au nnitalipa nauli ya mtu mzima ila alichokifanya ni kujibishana na yule mama. Akaanza kumwambia simpishi mtu angetaka angewahi. Mama kujibiwa vile akapata moto. Akamwambia nyie watoto wa siku hizi hamna adabu mzee kasimama wewe umekaa halafu unajibu vibaya. Mwanafunzi akamwambia mama "usitafutie kik kwangu kama una stress mshahara hujatoka achana na mimi." "Kwanza nakushangaa unavyoniambia nimpishe si ungempisha wewe". Mama akamwambia "we mtoto nina mtoto kama wewe nyumbani usinijibu vibaya". Mwanafunzi akamjibu "mama kama mtoto yuko kwako ungekua na mtoto kama mimi ungemleta kwenye garia saa hizi mbona hayupo kwanza achana na mimi na stress zako za kutolipwa mshahara".
Haki nilijisikia vibaya yule binti kumjibu vile mama wa watu. Sawa sio jambo zuri kumsimamisha mwanafunzi ili mtu mzima akae lakini yule binti ana mdomo mchafu sanaa. Kwa style hii hawa wanafunzi wa Dar wataendelea kufeli kwa sababu hawana adabu kwa mkubwa wala mdogo. Nimewazia walimu wake atakua anawajibu dharau kiasi gani wakiwa wanamgombeza.
Hata sisi tulikuwa tunachoka hivyo hivyo na bado tuliwapisha, Nini siku hizi daladaal za kumwaga sisi ilikuwa unasimama kituoni kama saa nzima au mawili maana barabara yenyewe ilikuwa ni moja sasa hiyo foleni yake, likifika mnagombea hadi ukiingia kwenye gari inabidi upumzike kidogo ili network irudi mara unaona mzee kasimama inabidi umuite aje akae, mitoto ya siku hizi adabu ni ziro, tena ingekuwa enzi zetu huyo Mtoto angetandikwa vibao vya mdomo humo humo kwenye kwenye daladala na akifika nyumbani hasemi maana atapigwa tenaMtu mzima ukishapanda kwny usafiri wa umma inabidi nawewe uache kuwaambia watu wakupishe siti ukiona mwanafunzi hataki kusimama achana nae,hawa watoto nao wanachoka jamani
Enzi za mwalimu unaenda nae hadi shuleni kwao kumshtakiaAisee...ni tabia mbaya sana mtoto kujibizana na mtu mzima.
Hi tabia ipo nchi nzima wala si Dar pekee ndio sababu ya kuharibikiwa kwao maana hata ukimkuta anafanya kosa ambalo labda yeye hajui kama ni kosa hakuna wa kumwambia kwa kuogopa kutukanwaAisee hizi tabia za wanafunzi wa dar wanazipata kutoka kwa kaka zao wanaume wa dar...nao wanamajibu ya ovyo sana
Hakika ziro zitawaadhibu!Ndio maana zero zinawaandama hazitawaacha salama
[emoji122] hakika hukumu ni hapahapa dunianiimeniumiza sana
Tena kabla ya kufika shule unakua umeshampa mbata tatu nne hivi...watoto hawana adabu kabisaEnzi za mwalimu unaenda nae hadi shuleni kwao kumshtakia
Aliekupeleka polisi hakua timamu..Nina wasiwasi katika hiloNilishachukuliwa rb kwa kosa lakumpiga kofi mtoto wa mtu..
Zama zimebadilika na zinaendelea kubadilika kwa kasi sanaTena kabla ya kufika shule unakua umeshampa mbata tatu nne hivi...watoto hawana adabu kabisa
Inahuzunisha sanaZama zimebadilika na zinaendelea kubadilika kwa kasi sana
Chanzo ni nyie wazazi lakiniInahuzunisha sana