Wanafunzi Jenipher na Caren wa Iringa girls wanahitaji ushauri wenu,enyi GREAT THINKERS

Hao watoto ni wajinga na wewe mwalimu wao ni mjinga
 
Kama wana umri wa miaka 18 na kuendelea wako huru kuamua chochote watakacho (kwenda chuo na kujilipia ada wao wenyewe), lakini kama wako under 18 years, hawana uhuru wa kuamua moja kwa moja, itabidi wakubali maamuzi ya wazazi wao.

Note
Inaonekana hao mabinti wana kiburi kimtindo, na huenda future yao itakuwa mbaya tu. Sio rahisi kwa binti wa kitanzania kuwa na ujasiri huo wa kupingana na baba yake kwa kiwango cha kuleta mambo hayo mpaka mtandaoni.
 
sababu yao haina msingi kama wanataka slope wambie waache ujinga wapiga kitabu kikali waje wasome bachelor ya hicho wanataka kusoma
 
Ama kweli kueleweka ni kugumu kweli
 
Naona Madam kama una kiwango kikubwa cha HEKIMA
Yuko zero

Usicheze na ku compromise masomo ya advanced sayansi unachezea maisha ya mtoto mwache aende

Advance sio ya kutania kisa mtu anaenda Viajira vya ngazi za chini vya diploma na certificate anajiriwa afanye vikazi vya low cadre vya mradi mkono uende kichwani
Dunia imebadilika usiangalie Tanzania tu ohh mimi nilikuwa na ki certificate na ki diploma nikajiendeleza miwazo ya kimaskini dunia ya sasa huko imehama

Mtoto atakuwa maskini.Mpeleke mtoto high level ndio maana inaitwa high school.
 
Afu watoto wa siku hizi uhuru umepitiliza[emoji28][emoji28][emoji28] sisi selection zikitoka tu unaambiwa jiandae unaripoti hata kabla shule yenyewe hawajafungua [emoji28][emoji28]

Tuna safari ndefu ya kwenda
Haya maisha haya na hasa ukitoka

Familia duni lazima upite A level maana hakuna wa kukusomesha chuo

Lengo lako ufaulu upewe mkopo



Kama wazazi zipo kama mtoa mada alivyosema waende chuo tu

Advance ni kama shortcut tu
 
Kweli nimeamini unaweza ukakatwa kichwa ukabakiza mgongo na kiuno tu na bado ukawaza.... case study ni wewe!!

Hebu niambie Wright brothers wa marekani walichimbua notes za nani (theory) ndipo wakabuni ndege ya kwanza?

Mbunifu mbobezi wa umeme unaouzungumzia bwana tesla alimeza lini hizo theory unazozihusudu wewe?

Ni aibu nzito kudhani kwamba ehiyo historia ya sayansi tunayofundishwa mashuleni ndio sayansi yenyewe....!

Mara mia wanangu wa VETA na SIDO wanaweza kua kwenye right track, kuliko hizo takataka unazozipigia debe humu

Ni aibu lukuki kijana kama wewe kuusifia mfumo wa elimu ulioasisiwa na wakoloni tena kwa lengo la kutudumaza fikra zetu

Mfumo ambao viongozi wako wa fisiemu wameurithi na kuwabrainwash watoto wetu, matokeo yake nafasi moja ya ajira inagombaniwa na vijana "wasomi" 500

Na mimi nasema acha wagombanie kwa kua mfumo umewaandaa kugo.bania "white collar jobs" kwa kumezeshwa mi theory ya watu waliokufa
 
Unachanganya madesa mazee! You are talking about unrelated things!
 
kwangu mm ,naona wamefanya maamuzi sahh kabisaa, wakipiga 3 yrs wanapata professional zao ,wakati wenzao watakua wanakipiga chuo mwaka wa kwanza ,baada ya hapo Wana join degree wakiwa hawana kikwazo Cha matokeo ya six,wakat hao wenzao walikiunga alevel watakuwa bado hawana uhakika wa ku join degree maana matokeo Yao ya six ndo hatma Yao ya kuvhonyoosha moja kwa moja au kurudi nyuma kuaoma diploma. So to me they're correct,and wise girls, they're after time .
 
Si waende chuo tu,? Parents can pay even in private colleges,so far wamefaulu vizuri!
 
Waende chuo waachane na advance maana wanaweza poteza muda kama wakizingua, watu wengi wamepoteza muda wa miaka mi 2 advance mwisho wa siku wakaanza diploma chuo, dunia imebadilika zamani watu walikuwa wanaenda advance ili kupata sifa za mtaa
 
Waende chuo waachane na advance maana wanaweza poteza muda kama wakizingua, watu wengi wamepoteza muda wa miaka mi 2 advance mwisho wa siku wakaanza diploma chuo, dunia imebadilika zamani watu walikuwa wanaenda advance ili kupata sifa za mtaa
Nashukuru Sana great thinker RoadLofa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…