Wanafunzi Jenipher na Caren wa Iringa girls wanahitaji ushauri wenu,enyi GREAT THINKERS

Wanafunzi Jenipher na Caren wa Iringa girls wanahitaji ushauri wenu,enyi GREAT THINKERS

Hao wazazi wanafuata mkumbo tu
Ao wazazi ni vichaa kabisa kwanini wasiwasikilize watoto wao? Ninasfi mtoto wangu akikataa Form five akataka chuo nampeleka haraka maana watoto wakike kuwachelewesha kidogo tu utajuta lakini pia mizazi mingine inadhani mtu asipopipta five na six hawezi kuajiliwa na serkali niujinga kumwazia mtoto ajira bada umwandae ajitegemee.
Nimetoa ushauri kama mzazi mwenye watoto wa umri zaidi ya 25 kwaiyo najua madhara watakayokutana nayo ao watoto na wazazi watajutabila watakuwa wamechelewa.
 
swali wewe ndie mazazi kwa hao vijana
Swali jingine je unao ujamaa nao hao vijana
Majibu hapana
Sasa wewe ni Nani ? Ushauri acha nao hao vijana watakuumiza kichwa
 
Ukijibiwa ni tag!!?

Nina lundo la visichana vimerudi mtaani viko kama vikichaakichaa..

Vilienda vyuo baada ya kidato cha nne...sijui mipango...sheria..procurement...maji...ifm...na takataka nyingine nyiingii..

Vipo mtaani kazi yao sasa ni kuhudhuria sherehe kucheza singeli na misibani.
Kuna mahali serikali inakosea sana.. chuo laxima kiende maturity ya mtoto. Wengi wanapomaliza form four wanakuwa 17 years, kumpeleka mtoto kama huyu chuo ni kumkatili.

Chuo mtu anakuwa treated as an adult, hakuna sheria kali za malezi ukilinganisha na A level, hivyo basi vitoto vingi huishia kubung'aabung'aa tu na vinakuwa victims vya ngono zembe. Kwani ni vitoto ushamba umevijaa na havina akili.

USHAURI KWA SERIKALI...
Maana hili ni la serikali na haiepuki lawama.. ni vyema watoto waende hivi vyuo baada ya A level..na msiwapangie wazazi.. acheni mzazi apange na mwanae na si kuwaamuru kupitia selection.

Na vyuo vingi mnavyowapeleka hao watoto ni vya hovyoo,havina msaada wowote.
Umemalizaaaaaa, ahsanteee
 
Inawezekana hawawazi Bata, advance imekuwa sio muhimu, pia unaweza kujikuta umepoteza miaka yako 2 Bure tu.
Ila katika Hali hii ya wazazi kushikilia makali basi Hawa wanafunzi hawana namna, wabaki shule tu wamalize then waende chuo. Mipango Yao wataikuta tu, wawe wavumilivu.

Madam Amina68 baadae alasiri tukutane Manyara (karibu na miyomboni pharmacy) tupange namna ya kuwashauri wadogo zetu!
Watajua wao na maisha yao.
 
Wanafunzi Jenipher na Caren wa Iringa girls wanahitaji ushauri wenu,

Wanafunzi Hawa walichaguliwa kujiunga kidato Cha 5 iringa girls mwaka huu,

Wameshareport lakini swala lao kubwa ni kwamba hawataki kusoma A level na hawakuijaza ktk machaguo ,waliopt chuo tu

Lakini wizara ikawatupa Iringa girls masomo ya sayansi.

Nikiwa kama Madam wao wa part-time, wamenifata na kuniambia kwamba hawataki kabisa A level wanataka waende chuo diploma 3 years,na wamejaribu kuongea na wazee wao wamesema Kama wanataka chuo wajisomeshe,

Sasa wamenifata kuniomba ushauri wafanye nn,maana wanaona kukaa huku A level ni kupoteza muda tu,

Hawa Watoto wanafikiria mpaka kutoroka shule,wapo dillema

NB: Jenipher baba ake ni komando JW

Caren mama ake ni Moja ya walinzi cruel ya Hangaya

MATOKEO YAO: Jenipher Ana Div I Pts 16

Caren Ana Div I-14

Ushauri kwenu wakuu GREAT THINKERS
Kwa ushauri wangu ni vyema sana wasome A-Level ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kwa elimu ya juu huko baadae. Wakienda chuo wajue wanenda kusomea taaluma na wakimaliza ikatokea wakapata ajira basi wataajiriwa na kulipwa mshahara wa mtu mwenye elimu ya kidato cha nne. Lakini wajue wao ni watoto wa kike wanakimbizana na muda dhidi ya umri na majukumu wakikosea hapa mwanzo itawawia ngumu sana kurudi shule huko mbeleni wakiwa tayari na majukumu ya kifamilia.
 
Kama wazazi wana fedha A level sio kupoteza muda ila kama makapuku ni heri waende COTC wachukue diploma ya clinical officer wapate ajira.
Ila kwa wadhifa wa wazazi wao ni vyema waendelee advance ili wakitoka hapo wakachukue degree ili baadaye wapachikwe pazuri
 
Back
Top Bottom