Wanafunzi Jenipher na Caren wa Iringa girls wanahitaji ushauri wenu,enyi GREAT THINKERS

Wanafunzi Jenipher na Caren wa Iringa girls wanahitaji ushauri wenu,enyi GREAT THINKERS

Afu watoto wa siku hizi uhuru umepitiliza😅😅😅 sisi selection zikitoka tu unaambiwa jiandae unaripoti hata kabla shule yenyewe hawajafungua 😅😅

Tuna safari ndefu ya kwenda
 
Serikali haiajili wenye degree sa hv , private ndo kabisaa hawataki hata kuwaona hao degree taker ....
Ukifuata upepo wa Serikali utakwama .mara iseme tunahitaji walimu wengi wa digrii wanasoma wakimaliza haya tuajirini wanasema tunaajiri certificate na diploma!!

Wewe soma usiangalie tu upepo wa Serikali kama digrii Tafuta ya kueleweka piga shule
 
Wanataka kusoma diploma ya nini?
Mmoja kasema anapenda Sana sanaa ,na mwingine kasema anapenda Sana mifugo ,na wakisoma hata wasipopata kazi watakuwa wamefanya wakipendacho na watamlaumu mtu
 
Tatizo hawasomi mixer 😅😅😅 Kama madam wa part-time usiwafungie sana humo ndani. Mara moja moja watoe nje wakapewe moto
 
Ukifuata upepo wa Serikali utakwama .mara iseme tunahitaji walimu wengi wa digrii wanasoma wakinaliza haya tuajitini wanasema tunaajiri certificate na diploma!!

Wewe soma usiangalie tu upepo wa Serikali kama digrii Tafuta ya kueleweka piga shule
Kwa kikubwa kumbe bora kusoma ukipendacho si ndio?
 
Afu watoto wa siku hizi uhuru umepitiliza😅😅😅 sisi selection zikitoka tu unaambiwa jiandae unaripoti hata kabla shule yenyewe hawajafungua 😅😅

Tuna safari ndefu ya kwenda
Na ndio maana ,umetoka chuo hujui ulichokisomea huko
 
Wanataka kusoma diploma ya nini?
Madogo wengi siku hizi wanaenda kusoma diploma vyuo vya kati. Mfano hao wenye masomo ya sayansi huenda kusoma vyuo vya COTC na kuhitimu kama Medical Assistants.

Na baada ya kupata hizo diploma, hupata vigezo vya kuingia chuo kusomea MD. Hivyo wanakuwa wameokoa muda kwa namna fulani, huku wakiwa tayari na CV ya mganga msaidizi.

Binafsi nimeshangaa kuna watoto fulani vichwa balaa huku niliko. Walipata Division One za single digit, halafu wamechaguliwa COTC! Na wameenda. So elimu ya A Level kwa sasa ni kupoteza tu muda.
 
Wanafunzi Jenipher na Caren wa Iringa girls wanahitaji ushauri wenu,

Wanafunzi Hawa walichaguliwa kujiunga kidato Cha 5 iringa girls mwaka huu,

Wameshareport lakini swala lao kubwa ni kwamba hawataki kusoma A level na hawakuijaza ktk machaguo ,waliopt chuo tu

Lakini wizara ikawatupa Iringa girls masomo ya sayansi.

Nikiwa kama Madam wao wa part-time, wamenifata na kuniambia kwamba hawataki kabisa A level wanataka waende chuo diploma 3 years,na wamejaribu kuongea na wazee wao wamesema Kama wanataka chuo wajisomeshe,

Sasa wamenifata kuniomba ushauri wafanye nn,maana wanaona kukaa huku A level ni kupoteza muda tu,

Hawa Watoto wanafikiria mpaka kutoroka shule,wapo dillema

Ushauri kwenu wakuu GREAT THINKERS
Hongera kwa kuaminika bila hivyo pengine wasingeweza kukuambia wanachokitaka.

Una wajibu wa kuwapatia ufumbuzi aa mgogoro wa nafsi na mgogoro na wazazi wao na hivyo wasipopata utatuzi wa changamoto hizo unaweza kuwaathiri kwenye masomo yao au pengine kuchelewa kuenda sambamba na wengine.

Hebu kaa nao kwa wakati tofauti muulize kila mmoja. Kwanini anadhani kwenda chuo ni bora kuliko kuendelea kidato cha tano? Pili wanadhani kwankni wazazi wanawataka wasome kidato cha tano badala ya chuo?

Kupitia majibu yao utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuwashauri njia sahihi na watakuelewa.

Kumekuwa na hiyo changamoto kwa vijana wengi sababu ya.
-Mob Psychology/peer groups.
-Kuharakia maisha ya anasa vyuoni.
-Uhuru kufanya watakayo.

Wakati unawashauri pia zingatia umri wao.
 
Thank you very much Don jully GREAT THINKER
 
Na baada ya kupata hizo diploma, hupata vigezo vya kuingia chuo kusomea MD. Hivyo wanakuwa wameokoa muda kwa namna fulani.
Kusomea MD kwa sifa ya Diploma ngumu kupata

Wenye diploma wanaoenda kujiunga na digrii unawamulika kwa torch MD ina ushindani sio mchezo Waliopitia Diploma wengi hawapenyi
Anatakiwa kufaulu sio utani huyo mwenye diploma
Wengi huishia huko huko kwenye diploma
 
Madogo wengi siku hizi wanaenda kusoma diploma vyuo vya kati. Mfano hao wenye masomo ya sayansi huenda kusoma vyuo vya COTC na kuhitimu kama Medical Assistants.

Na baada ya kupata hizo diploma, hupata vigezo vya kuingia chuo kusomea MD. Hivyo wanakuwa wameokoa muda kwa namna fulani, huku wakiwa tayari na CV ya mganga msaidizi.

Binafsi nimeshangaa kuna watoto fulani vichwa balaa huku niliko. Walipata Division One za single digit, halafu wamechaguliwa COTC! Na wameenda. So elimu ya A Level kwa sasa ni kupoteza tu muda.
Tate Mkuu ,Thank u boss
 
Kua na adabu binti sawa. Tunacomment hapa kukufanyia hisani au unataka uzi udode ka ulivododa mpaka kuwa jitu la parttime . Tuliza hilo komwe kubwa ka baruti.

Na uavhege uphaller
Pau Montanna
Kuwa pale Part-time sio kwamba Sina cha kufanya, na ndio maana nimeomba GREAT THINKER wakoment
 
wazazi wao wana nafasi nzuri, wasisitize kusoma kwa bidii wasiwaangushe wazazi!! kwa baadae connection zitakuwepo kutoka kwa wazazi!!
 
Waende wizarani watasikilizwa kulingana na ufaulu wao na masomo waliyofaulu, pia watashauriwa Kama kile wanachotaka kukisoma kitarelate na ufaulu wa masomo yao. Mfano huwezi kusomea afya Kama umefaulu masomo ya Sanaa.
Ada za vyuo vya Kati sio kubwa sana maana na mie nilipitia hivyo hivyo.
NB: Kuna kauli ilitolewa miezi kama 3 na waziri Kama sijakosea kuhusuana na ambao hawapendi kusoma advance.
 
Pau Montanna
Kuwa pale Part-time sio kwamba Sina cha kufanya, na ndio maana nimeomba GREAT THINKER wakoment
Every one is a GREATTHINKER Miss.

The matter of fact is uache kujibu wenzio shombo au unataka tukutumie team la ufundi likutie adabu eheee.?? Maana hatushindwi kitu sisi binadamu.

Take care limadam lisilo jielewa. Umenijibu vibaya sana na sijapenda. Tutaonana
 
Amina68 pole sana kwa maswaibu ya wanafunzi wako , ndugu ni kweli ni haki ya kila mtu kufanya alitakalo hususani kwa hao mabinti maana ni umri wa wao kuwa na mawazo chanya na yenye utegemezi kwao ila sasa...

Ikiwa wazazi wao kweli wapo katika hivyo vyeo na pia ikumbukwe wametishia kusitisha malipo ya ada kwa watoto wao ikiwa hawapo tayari kubaki shule ya upili sasa ni hivi ...

Yawezekana tayari wana sehemu wamewaandalia kuwepo lakini pia ikiwa wanachohitaji kukisomea huko chuo hata baada ya shule ya upili wanaweza kukisoma , Nakushauri uwashauri ya kuwa zama zimebadilika si kuwa wakiwahi chuo basi ndiyo uhakika wa ajira ila inategemea na connections hivyo , waombe na kuwajuza kuwa embu wawasikilize wazazi wao na wabaki shuleni hapo , wakisoma kwa juhudi maana chochote chaweza kutokea huko mbeleni .

Ushauri tu .[emoji120][emoji120]
TEKERI
 
Mfumo wetu wa elimu hapa nchini kuna mahali unachanganya sana.
Kama mtu yuko tayari kwenda chuo, aende tu. Isitoshe form 5 & 6, wakati mwingine ni kupoteza muda tu.
Wapewe nafasi ya kuchagua kinachowafaa
 
Back
Top Bottom