Wewe mleta uzi pamoja na wachangiaji wengine wenye mrengo wa kuwatetea wanafunzi wanaofail LAW SCHOOL OF TANZANIA(LST) wote mnaonekana ni wajinga na hamjui LST inaendeshwaje na mitihani yake inafanyikaje ila kwa ujinga mlionao mnaweza kujivika unguli wa kujadili hoja ya law school of Tanzania huku mkidhihaki walimu wa shule hiyo ya Sheria kwa msiofahamu napenda kuwapa taarifa za shule hio jins inavyofanya kazi hasa kwenye kipengere cha mitihani yake na jins mwanafunz anaweza kufauli mitihani yake.
1. Law school hufundishwa kwa categories mbili;
a) Theories kidogo huku kukiwa na practical training kiasi na mafunzo hayo hufundishwa na walimu wa shule hio na wakati mwingine majaji mfani, Judge Twaib na Judge Dr.Luhangisa na hii hufanyika MULTI-PURPOSE HALL kwa waliofika au kupitapita pale law school watakuwa wanalifahamu hili jenge mahala lilipo.
b)SEMINARS, hapa ndipo mafunzo kwa vitendo hutawala yakiambatana na scenarios mbalimbali za masomo husika yanayofundishwa kwenye shule hiyo na husimamiwa na walimu wa shule hio pamoja na mahakimu au waendesha mashtaka kutoka sehemu tofauti tofauti
2. Mitihani ya law school imegawanyika kwenye vipengele vinne(Four components) kwa zile core subjects,
a) Individual Contineous Assessment(ICA).
b)Written Practical Exercise(WPE).
c) Final Exercise(FE).
d) Oral Practical Exercise(OPE).
3. Mitihani hii yote ina marks 100% kila component na hugawanywa kwa nne ili kuletea uwiano wa marks mia kwa kila somo kwenye masoma ambayo ni core subjects kama, commercial aspects,civil procedure,criminal procedure,probate and administration, ethics na conveyancing(kwenye masomo haya kila component kama nilivyosema hapo juu ina 100% hivyo somo moja huwa na 400% kugawa kwa 4=100%)
4. Pia kuna masomo matatu ambayo mtihani wake ni mmoja tu nayo ni, Legal drafting, Human Rights and Accounting for lawyers.
5. kwenye yale masomo ya components nne kuna mtihani wa WPE wanafunz huingia na kila kitu hata kama una tela la trekta la vitabu unavyofikiria vitakusaidia unaruhusiwa kuingia navyo kuanza asubuhi saa tatu hadi saa saba kisha mnatoka nje kula baada ya hapo unaenda sasa kuufanya huo mtihani maana hio asubuhi unapewa maswali unajisomea huku ukiwa na material yako kama nilivyosema hapo juu.
4. Mtihani wa OPE ni wa mahojiano kama enterview unaingia kwenye pannel ya watu watatu unahojiwa maswali mbalimbali ya kisheria kisha unatoka na mtihani huu husimamiwa na mwalimu mmoja wa law school na hakimu mmoja pamoja na wakili wa serikali mmoja kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini,
HAPA SWALI LA KUJIULIZA nani atakufelisha maana hakimu na wakili wa serikali hawana favour wala kuonea mtu hata kama utasema yule mwalimu wa law school anaweza kufanya makusudi kukufelisha.
KWENYE HOJA ya mitihani mwisho kabisa ile ya components hugawanywa kama nilivyosema na yale masomo matatu huwa na mtihani mmoja tu ukishindwa unaenda kufanya supplementary examination maarufu kama sup.
POINT TO NOTE ili usidisco unatakiwa ufaulu angalau masomo manne ya core subjects SASA ukiwa mwanafunz serious unashindwaje kufaulu hapo law school, wanafunzi wengi wanaenda law school wakiwa na akili za kukariri kama walivyozoea kwenye degree zao huko vyuon na hicho ndio wengi huwaponza maana law school haitoi mitihani ya kujibiwa kwa kukariri inatoa practical examinations as if wewe ni wakili uko mahakamani kupambania kesi yako na maswalu yake ni very technical ukicheza kidogo tu swali lote kama linamarks 40% unazikosa na walimu hawana huruma unawekewa sifuri bila hiyana.
USHAURI; wanafunzi wa law school wasome waache kulialia mitandaon maana walizoea kuhonga ngono na kujipendekeza kule vyuoni hapo law school ni uelewa wako ndio utakuokoa vinginevyo NCHI HII tutajikuta tunakuwa na majaji,mahakimu,waendesha mashtaka na mawakili vipanga jambo ambalo ni hatari.