Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Julai 3, 2026, Mdau aliandika “Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) tuliingiziwa Boom (fedha za mkopo) mara 2 kimakosa, wametumia TAKUKURU kutuweka mahabusu, kwani hayo ni makosa yetu? Hii si sawa”. Ufafanuzi umetolewa kutoka pande husika.
Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano katika Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Amani Kakana amesema “Bodi hatukupata hasara yoyote wala hakuna Mwanafunzi tuliyeelekeza akamatwe, changamoto ya malipo inahusu Benki husika (CRDB), waulize wao, sisi hatuna shida yoyote na hatuhusiki.”
Upande wa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – TAKUKURU, Doreen Kapwani amesema “Tumepata taarifa hizo na tunazifanyia kazi, tutatoa taarifa kamili itakapokuwa tayari.”
Alipoulizwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano Benki ya CRDB, Emmanuel Kiondo amesema “Kwa sasa tunasubiri kwanza taarifa ya Bodi ya Mikopo (HESLB) kisha tutatoa ufafanuzi."
ILIKOANZIA ~ Wanafunzi wa UDSM tuliingiziwa Boom mara 2 kimakosa, kutudai wanatuletea TAKUKURU kutukamata, kwani hayo ni makosa yetu?