Kuna saga linaendelea sasa hivi. Wanafunzi baadhi wa chuo UDSM waliingiziwa pesa za boom lakini siyo kiasi kinachotakiwa, baadhi wameingiziwa milioni moja, milioni 3, milioni 5, kumi na wengine mpaka milioni 20!
Kwa upande wa Bodi ya Mikopo hakukuwa na shida yoyote, wao waliidhinisha kiwango sahihi, hivyo wao hawajapata hasara yoyote, changamoto imetokea kwa CRDB, wao ndio waliongeza cha juu!
Wanafunzi walivyopokea pesa hizo wapenda starehe wameenda kutumbua, wengine wamenunua mashamba, wengine viwanja, wengine wamenunua magari, wa kuhonga wamehonga, yaani pesa zimetumika, baadhi zimebaki kiasi.
Baada ya jambo limekuwa out of hand wameenda kutafutwa TAKUKURU wawatie upepo watoto wa watu warudishe hizo pesa, maana wakienda mahakamani process ni ndefu, lakini pia hata kama ni mahakama inamaana hii itakuwa ni kesi ya madai! Ila na hapa, TAKUKURU ilitumia sheria gani kuwakamata hao wanafunzi wakati pesa ziliingizwa kwao sio kwamba kuna act ya rushwa ilifanyika?
Maswali yanabaki pesa hizo walizopewa wanafunzi ni za nani? Ni kutoka kwa wateja au kuna pesa zilikuwa ninachepushwa lakini jambo likaharibika baada ya wanafunzi kushtuka na kuzitumia pesa hizo. Lakini pia nimesikia (sina uhakika na hili, wanaojua zaidi watakuja kusema) kuwa account yako inapokuwa kwenye status ya uanafunzi inakuwa inawekewe limit ya kupokea pesa, mpaka umalize na upite muda fulani. Kama hili ni kweli pesa hizo nyingi ziliwezaje kuingia kwa wananfunzi? Ulikuwa mpango wa kusafisha pesa hizo?
Naona moto unaongezeka huko mtandaoni watu wanaendelea kulalamika kuwa kuna pesa zinapigwa sana na CRDB na hakuna majibu yanayoeleweka kutoka kwao. Hivi kwanini haya mambo yanatokea sana CRDB? Nakumbuka hata mwaka jana ilitokea zaga kama hili - na wazuri sana kwenye kuosha hivyo wanatumika sana au shida iko wapi?