KERO Wanafunzi wa UDSM, tumezuiliwa kufanya mitihani kwa kushindwa kukamilisha Ada

KERO Wanafunzi wa UDSM, tumezuiliwa kufanya mitihani kwa kushindwa kukamilisha Ada

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257

Lecturer anayefundisha kozi ya Research Methodologies akifukuza Wanafunzi ambao hawajakamilisha Ada.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) tumezuiwa kufanya mitihani ya Test One kwa kukosa vitambulisho vilivyo hai (Valid ID) kwa sababu ya kushindwa kumalizia Ada ya Semister ya Pili.

Hii inachagizwa na Wanafunzi wengi kuwa na kawaida ya kutumia fedha za kujikimu (Boom) tunazopata kutoka Bodi ya Mkopo kwa ajili ya kulipa ada, pia mpaka sasa wengi wetu hatujapata Boom la pili na hivyo kushindwa kumalizia ada tunayaotakiwa kuilipa.

Changamoto hii imetokea kwenye Vitivo mbalimbali hasa Wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza na Wapili mbao walilipwa kiasi kidogo.

Wanafunzi tulituma barua ya maombi kwa Mkuu wa Chuo kuomba turuhusiwe kufanya mitihani kwa kuwa malipo ya Bodi yanatarajiwa kutolewa wiki ijayo lakini majibu tuliyopata ni kuwa hilo halitawezekana.

Uongozi wa Chuo umesisitiza Wanafunzi wote wanatakiwa kulipa Ada kwa maelezo kuwa wapo ambao hawategemei Boom kulipa ada ambao hawajapata mkopo na kuwa idadi ya ambao hawajalipa ada ni kubwa, hivyo chuo kina ukwasi.

Majibu ya Bodi ya Mikopo - HESLB: Fedha za kujikimu (Chakula na Malazi), Wanafunzi kuanza kupokea kuanzia Jumatatu, Mei 20, 2024
 
Extended secondary
Hapo ni wote waliolipa na wasiolipa
Vitivo vyote mnaingia road mnakichafua balaa hadi ada inaondolewa sema kwa suruali hizo na miili ya Janabi sioni wa kufanya hivyo
Waache watoto wetu aisee!Wanavaa tuvazi wanatuita"modo".Na ile miili yao chakula chao kikuu ni maandazi mawilimawili kwa chilisosi.
 
Back
Top Bottom