KERO Wanafunzi wa UDSM, tumezuiliwa kufanya mitihani kwa kushindwa kukamilisha Ada

KERO Wanafunzi wa UDSM, tumezuiliwa kufanya mitihani kwa kushindwa kukamilisha Ada

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
View attachment 2991530
Lecturer anayefundisha kozi ya Research Methodologies akifukuza Wanafunzi ambao hawajakamilisha Ada.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) tumezuiwa kufanya mitihani ya Test One kwa kukosa vitambulisho vilivyo hai (Valid ID) kwa sababu ya kushindwa kumalizia Ada ya Semister ya Pili.

Hii inachagizwa na Wanafunzi wengi kuwa na kawaida ya kutumia fedha za kujikimu (Boom) tunazopata kutoka Bodi ya Mkopo kwa ajili ya kulipa ada, pia mpaka sasa wengi wetu hatujapata Boom la pili na hivyo kushindwa kumalizia ada tunayaotakiwa kuilipa.

Changamoto hii imetokea kwenye Vitivo mbalimbali hasa Wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza na Wapili mbao walilipwa kiasi kidogo.

Wanafunzi tulituma barua ya maombi kwa Mkuu wa Chuo kuomba turuhusiwe kufanya mitihani kwa kuwa malipo ya Bodi yanatarajiwa kutolewa wiki ijayo lakini majibu tuliyopata ni kuwa hilo halitawezekana.

Uongozi wa Chuo umesisitiza Wanafunzi wote wanatakiwa kulipa Ada kwa maelezo kuwa wapo ambao hawategemei Boom kulipa ada ambao hawajapata mkopo na kuwa idadi ya ambao hawajalipa ada ni kubwa, hivyo chuo kina ukwasi.
ingekuwa miaka iyo uyo lecture muda huu hapo angebebwa kichwa chini miguu juu,ofisi ya makamu wa chuo Ffu washafika mlangoni wanamtoa kwa mlango wa dharura
 
Nikiwa IFM mwaka 2014 sem ya pili sikuwa nimelipa ada pia nikazuiwa kufanya test one ikanibid nipostpone sababu hali ilizidi kuwa tight ikanibidi nidrop chuo. Sikuwahi kurudi mpaka leo
 
Iv ukijiajiajir wanakukataje loan ya board ya mkopo.
Mfano ukisajiri kampuni au ukitoka katika ujasiriamali na kuwa mfanya biashara kuna TIN number ambayo inataarifa zako kama mzalishaji na katka ulipaji wa kodi kama mfanya biashara lazima ukatwe chao kupitia hiyo TIN number yako...usishangae watu wanasajiri hizo mbaga kwa majina ya watoto wao
 
Back
Top Bottom