Wanafunzi wachoma moto pikipiki ya mwalimu, wafyeka shamba kisa adhabu ya kukutwa na simu shuleni

Hatujasikia tamko la Mkuu wa Shule
 
Mwenge Secondary kuna O Level? Huyo mwanafunzi aliyeadhibiwa n wa kidato cha 6.

Ila walimu wengine waache unoko na ukuda, japo sitetei kitendo kilichofanywa na wanafunzi hao. Msieeew
Unoko na ukuda ndio kitu fani hicho?
 
Hapo ukifuatilia kwa undani, utagundua chanzo ni malezi. Wazazi wengi hawana muda wa kulea watoto wao. Jamii nayo ina mafundisho yake yaliyo mema na mabaya. Kwahiyo vijana wengi wanakosa muelekeo na hatimaye kuwa na tabia hatarishi
 
Ningependa kukuita mjinga tu kwa sababu unataka kujiona unaujua uzungu wakati huna ulijualo zaid ya uongo na upotoshaji sorry! Lakini.

Hebu soma hapa
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
ni afadhari kama hujui kitu ukae kimya kuliko kujifabya unajua wakati hu a lolote ulijualo Kuhusu hiyo china unayo sema haizuii simu kwa wanafunzi
 
Pia soma hapa kuhusu philipines
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Siku nyingine acha uongo na kujifanya unayajua sana maisha ya kizungu wakati umejaa uongo na uzushi mkubwa na huna ulijualo kutoka huko isitimbi kijijini kwenuπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Ukisoma hii habari utahisi wanafunzi ndio wakorofi, mimi mpwa wangu anasoma pale form six na alinielezea A to Z ya nini kilichotokea.

Mimi mvivu sana kuandika lakini kifupi ni kwamba huyo mwanafunzi aliyesemekana kakutwa na simu, haikuwa ya kwake... Huyo mwalimu aliyechomewa pikipiki ndio alikuwa anamuadhibu kijana ili aseme simu iko wapi... Kifupi ni kwamba Mwalimu alimchapa vibaya mwanafunzi mpaka akazidiwa. Walimu wakaogopa kumpeleka hospitali kwa sababu hakukuwa na pf3.

Kituoni waliogopa maana wangetoa maelezo gani ili waeleweke. Ndipo ikabidi wamrudushe shule wakampa dawa ili atulize maumivu. Jioni mwanafunzi hali yake ikawa mbaya zaidi ndipo wanafunzi wengine wakaanza kushinikiza apelekwe hospitalini. Kukawa na mvutano kati ya waalimu na wanafunzi.

Yule mwalimu aliyetoa adhabu akawa anawatukana wanafunzi na kuwajibu jeuri. Wanafunzi wakapandisha hasira na mvutano ukawa mkubwa, Mwalimu mkuu alipata taarifa na kufika eneo la tukio. Akajaribu kuwasihi wanafunzi watawanyike atashughulikia lakini wanafunzi tayari walishapandisha hasira na chuki dhidi ya yule mwalimu, kwani inasemekana yule mwalimu amekuwa na tabia ya kupiga wanafunzi hovyo bila utaratibu na kuwatukana matusi.

Hiki ndio chanzo mpaka huyo mwalimu kuchomewa pikipiki na kufyekewa shamba lake. Haya ni maelezo mafupi tu ya nini hasa kilichotokea.
 
Mwl Frank alimtandika dogo watu wakaja juu hadi Ndalichako akaamuru DUCE wamsimamishe chuo. Sasa tusubiri haki za binadamu wanasemaje kwenye hili.
Kuna changamoto kubwa sana ya malezi kizazi hiki. Mwanafunzi asiguswe tuendelee tutavuna tulichopanda
 
Kwa nini wa wanafunzi wa shule za sekondari hawaruhusiwi kuwa na simu shuleni?!
 
hahahahahah yaani umeokoteza vi link uchwara kuja kunipinga hapa ni kiasi Gani unaonesha wewe ni zuzu first class wenzako Huko shule zimeunganishwa na Mifumo ya IT wewe unaniletea Link za mwaka 2003 Huko na Leo tupo 2022
Kiufupi endelea kujidanganya na kuleta ujuaji!
 
Mobb psychology. watakuja kugundua hayo wakati wanatumikia kifungo, na wakati wazazi wao wanalipa mali zilizoharibika
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Mkuu maujanja tuu
Juzi kuna mwenyekiti wa chama cha walimu(cwt) wilaya nikamsikia anamsimulia mwenzie(kiongozi wa ccm) '' yaani nikamla .... kimasihara....''

Nikajua tayari uzi umeshafanya yake.
 
Hii comment watu hasa walimu wataipita kama hawaioni... Kiufupi huyo mwalimu hajaanza leo, mwalimu huyo anaukatili by nature kabisa na ninahisi ana matatizo kisaikolojia hadi huwa anakuwa hivyo

Wakati tupo sisi kipindi hicho alikua na visa kama hivi vingi na alikuwa ananusurika sana kupata hivi vipigo kutokana na matendo yake haya

hatukatai bylaws zetu za mashuleni zilizopitwa na wakati haziruhusu Wanafunzi kumiliki simu ila mwalimu huyu alikua anatake advantage ya hiyo sheria kwa maslahi yake binafsi.. alikua akipata taarifa kutoka kwa maspy wake ambao aliwaruhusu kumiliki simu ili kumpa taarifa kuhusiana na simu zilizopo mabwenini basi anakuja anachukua then anaenda ziuza kama ni iPhone au simu ambazo ni ngumu kubypass password bas atakupa kipigo hadi utoe password au umpe hela akurudishie simu yako

Hili ni fundisho kwa walimu wengine ambao wanafanya vitendo kama hivi vya Dhulma kwa kujifichia kwenye kivuli cha utaratibu na sheria za shule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…