Hapa sasa umenipa mwanga kumbe ni Waalimu!, maana nilikua nasoma comments huku nimebaki kinywa wazi, utumwa wa fikra hauwezi kuisha Tanzania halafu ndio tuna ndoto za kufika Dunia ya kwanza,
Mawazo finyu sana hawaangalii vitu kwa jicho la tatu,
Mtoto akifanya kosa ukamwambia alete Tofali na yeye hataki nyumbani wajue si ndio mwanzo wa kua mwizi au afanye uhuni ili apate pesa ya kununua hizo tofali,
Haya kosa la Mtoto kwanini Mzazi wake atoleshwe Pesa za kununua Tofali? Huyo Mzazi ana mangapi yanayomsibu na Tofali tena!!
Hiyo Tabia yapaswa kukemewa haijalishi ipo Shule nyingi (Shule nilizosoma sikuwahi kukumbana na hayo mauza uza) na haijalishi kwa kua wewe Mtu mzima uliwahi kupitia hayo basi kila kizazi kipitie,
Tubadilike.