Wanafunzi watatu wafariki kwa kukosa hewa wakati wanatoa mahindi kwenye kihenge cha shule, mwalimu aliwaacha na kwenda kunywa chai

Ok boss, Wewe ndo mwalimu unaemsemea mwalimu wa zamu aliekwenda kunywa chai akaacha watoto bahati mbaya wakafa. Wazazi wamefika ofisini kwako, embu waeleze kilichotokea kwa kutumia busara ya kuwawezesha kuganga yajayo na pasiwepo chuki ili nijifunze kitu. Maana nachakata namna ya kuelezea ukweli wa hilo tukio sipati maneno.

Haya twende mkuu, unaanzia wapi?
Mkuu; Anza kwa kuwashirikisha Mwalimu mkuu, Waalimu wote wakiwemo na Watumishi wengine wa hapo shuleni (Kikao cha dharura) hapo utapata namna ya kuliweka hilo suala mbele ya kikao cha Wazazi, wanafunzi na Jamii (watu wengineo - Wadau) ukizingatia kwamba tukio hilo hadi hapo lilipofikia, limeshafikia stage ya kuwa linaihusu Shule na Wazazi wote na sio tena eti ni la kwako peke yako mwl wa zamu na unakomaa nalo kivyako-vyako.
Kumbuka Mwl. Mkuu ndiye msemaji wa shule na sio mwalimu wa zamu.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Ni jambo la kawaida kwa shule zetu, mfano unasoma shule ina mchepuo wa kilimo, unategemea nani aende shambani..?? nani avune..?? nani ahifadhi mahindi..??

Tushalima sana, kuvuna na kuhifadhi mahindi mashuleni... Na nyingi ya shule hizi ni zile za bweni
Kongole mkuu. Huo ndo ukweli halisi.
 
Wanafunzi sita wa shule ya mtakatifu John Paul II ya mkoani Shinyanga walienda kutoa mahindi kwenye kihenge cha shule lakini yalishindwa kutoka wakiwa na mwalimu wa zamu katika usimamizi wa chakula, mwalimu alielekeza wanafunzi watatu waingie ndani kutafuta namna ya kuyafungulia kisha akaenda kunywa chai. Baada ya muda kupita, wanafunzi watatu waliobaki nje wakaona wenzao hawatoki na kutoa taarifa kwa walimu.

Walimu walipofika waliita bila mafanikio, wakavunja kihenge na kukuta wamezirai. Baada ya kufikishwa zahanati ya shule matibabu hayakuleta majibu na kukimbizwa hospitali ya Kahama ikathibitishwa wamefariki kutokana na kukosa hewa safi.

Kaimu kamanda wa Polisi, ACP Kennedy Mgani amesema Mwalimu wa zamu, Morris Sileo anashkiliwa na Jeshi la Polisi kwa kushindwa kusimamia vyema ili kubaini uchunguzi na chanzo cha vifo cha wanafunzi hao.
R.I.P wanafunzi wazuri
 
Somo gani hilo linasababisha vifo.
Mkuu; mbona unajitoa ufahamu na unashangaa zaidi kwa kujikita kwenye hoja ya kifo?? Kumbuka kifo kipo siku zote. Kama kweli unazifahamu hizi shule zetu hapa Tz, suala la kilimo e.g. kulima bustani, mazao na kuyahifadhi, maua, kufyeka, n.k. ni jambo la kawaida sana.
Swali lako hapo juu 👆 👆👆eti ni somo gani linasababisha vifo; Ni sawa na kuhoji kazi ya bodaboda kwamba eti kazi gani hiyo inasababisha vifo :BatChesting:
 
Mkuu; Anza kwa kuwashirikisha Mwalimu mkuu, Waalimu wote wakiwemo na Watumishi wengine wa hapo shuleni (Kikao cha dharura) hapo utapata namna ya kuliweka hilo suala mbele ya kikao cha Wazazi, wanafunzi na Jamii (watu wengineo - Wadau) ukizingatia kwamba tukio hilo hadi hapo lilipofikia, limeshafikia stage ya kuwa linaihusu Shule na Wazazi wote na sio tena eti ni la kwako peke yako mwl wa zamu na unakomaa nalo kivyako-vyako.
Kumbuka Mwl. Mkuu ndiye msemaji wa shule na sio mwalimu wa zamu.
Hujanielewa boss. Hoja ni asibebeshwe lawama mwalimu ili pasiwe na chuki. Sasa twende......

Mwalimu wa zamu yupo polisi kwa tuhuma za mauaji bila kukusudia. Wewe ni mwalimu mkuu, sasa najaribu kuwaza unatakiwa uongee na wazazi wa hao watoto kuwaeleza kilichotokea bila kumpa lawama mwalimu ili pasiwe na chuki. Utatumia maneno gani?

Unajua siku zote lazima awepo wa kubeba lawama, ukitaka tatizo liwe kubwa sana akosekane wa kubeba lawama au asiwepo wa kutolewa kafara, hapo ujue shida itahamia kwa uongozi mzima wa shule, yataibuka mambo unaweza kushindwa kufanya damage control.

Unadhani kwanini kwenye siasa kama kuna tatizo serikali imefanya na haiwezi libeba lazima atafutwe wa kubeba hizo lawama? Atolewe kafara?

Hapo ili uongozi wa shule uwe salama, hatua ya kwanza ni kukubali kuwa mwalimu wa zamu amefanya uzembe wa hali ya juu na watahakikisha wanasaidiana na polisi ili sheria ifate mkondo wake, mpaka hapo utakuwa pamoja na wazazi, mengine yatafata.
 
Ni nature walipangiwa watakufa hivyo Pindi tu walipozaliwa. You cant avoid the forces of nature.

R.I.P madogo
Mkuu; Siiafiki sana nadharia hiyo kwani kama ndo hivo; basi ingelikuwa zimechukuliwa tahadhari zote stahiki lakini bado tukio likatokea- hapo sawa. Lakini tukio hili limeacha maswali mengi sana bila majibu. :AYOOO:
 
Tatizo ni kuendesha mambo locally. Ilipaswa aliyetengeneza hicho kihenge aandike maneno ya tahadhari Kwa hatari zozote zinazoweza kujitokeza kutokana na kihenge hicho. Mf. Ni hatari kuingia ndani ya kihenge, hakuna hewa safi
 
Kuna haja ya walimu kupewa somo la usalama mashuleni hasa shule za bweni.
Ni jambo la kawaida kwa shule zetu, mfano unasoma shule ina mchepuo wa kilimo, unategemea nani aende shambani..?? nani avune..?? nani ahifadhi mahindi..??

Tushalima sana, kuvuna na kuhifadhi mahindi mashuleni... Na nyingi ya shule hizi ni zile za bweni
 
Kuna haja ya walimu kupewa somo la usalama mashuleni hasa shule za bweni.
Hii ndio pointi ya msingi, pamoja na yote hayo kufanyika... Lazima usalama uzingatiwe ili kuepuka ajali kama hizi, kama watu hawana elimu ya usalama.. basi elimu itolewe kwa wasimamizi na wahusika wote
 
Inasikitisha sana jamani
Wapumzike kwa amani!

Kuna shule nyingine walikufa kwa kukosa hewa hivohivo watu wazima kama wanne hivi wakifuatilia maji kwenye kisima fulani cha Zamani sana huko ndani alieanza kuingia hakurudi akaingia mwingine kumuangalia mwenzio na mwingine hadi wa tano ndio alipojaribu tu akakosa hewa fasta akarudi

Cc Smart911
 
Hujanielewa boss. Hoja ni asibebeshwe lawama mwalimu ili pasiwe na chuki. Sasa twende......

Mwalimu wa zamu yupo polisi kwa tuhuma za mauaji bila kukusudia. Wewe ni mwalimu mkuu, sasa najaribu kuwaza unatakiwa uongee na wazazi wa hao watoto kuwaeleza kilichotokea bila kumpa lawama mwalimu ili pasiwe na chuki. Utatumia maneno gani?

Unajua siku zote lazima awepo wa kubeba lawama, ukitaka tatizo liwe kubwa sana akosekane wa kubeba lawama au asiwepo wa kutolewa kafara, hapo ujue shida itahamia kwa uongozi mzima wa shule, yataibuka mambo unaweza kushindwa kufanya damage control.

Unadhani kwanini kwenye siasa kama kuna tatizo na raisi kalifanya na hawezi libeba lazima atafutwe wa kubeba hizo lawama?

Hapo ili uongozi wa shule uwe salama, hatua ya kwanza ni kukubali kuwa mwalimu wa zamu amefanya uzembe wa hali ya juu na watahakikisha wanasaidiana na polisi ili sheria ifate mkondo wake, mpaka hapo utakuwa pamoja na wazazi, mengine yatafata.
Mkuu, mbona hadi hapo sasa limekuwa rahisi zaidi? Kumbuka wazazi wa hao wanafunzi marehemu hawapo hapo shuleni na mwl. wa zamu yupo kituoni na ingekuwa ni vizuri zaidi awe amewekwa mahabusu.
Mimi kama mwl. Mkuu cha kwanza ni kuwakaribisha wazazi hao hapa shuleni halafu nahakikisha mm nasimama upande wao kama mzazi mwenzao (ku-sympathize nao) wakati huo ni pamoja na kuisoma hali waliyokuja nayo wazazi (Je, wamekuja kwa shari au amani) halafu nafanya maamuzi: Kama wamekuja kwa Amani nitawaelezea kwa uwazi hali inavyokuwa kwa kawaida shughuli za kilimo hapo shuleni na tulivyokuwa tumezoea kufanya na nitaelezea jinsi shughuli husikailivyofanyika miaka iliyopita na ilivyoanza kufanyika mwaka huu tokea nitataja muda na wahusika na majuzi ilivyokuwa ..... lakini katika hali isiyo kuwa ya kawaida na ambayo hatukuitegemea tar..../05/2024 wanafunzi (nataja idadi ya wote waliohusika nje na ndani) walikwenda kufanya shughuli hiyo hiyo kama walivyofanya wenzao......ila kilichotokea ni kwamba baadhi yao (nataja idadi ya waliofariki) walikutwa wakupoteza maisha.
Nitaeleza.....Kwa kuwa jambo hili ni zito, lilitustua na linasikitisha ilibidi tuweze kutafuta msaada kutoka kwa wakubwa wetu Afisa Elimu (W), Polisi, Madaktari na kwa Wataalam Kilimo na Mifugo. Huko tulikoomba misaada wameonesha ushirikiano wa hali ya juu na kwa sasa Miili imepokelewa Hospitali kwa uchunguzi zaidi, Polisi wamemchukua mwl. aliyekuwa zamu ili kupata maelezo ya jinsi ilivyotokea, Afisa kilimo alifika kukagua kihenge husika na amechukua sampuli ya mazao yaliyokuwa yamehifadhiwa ili kuyachunguza.... na kwa kuwa tukioa hili kwa sasa lipo mikononi mwa wakubwa viongozi wetu na tunasubiri matokeo ya uchunguzi ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa, kwanza natoa pole kwa wazazi, jumuia ya shule na jamii kwa ujumla na tumeshauriwa na Hospitali kwamba kwa sasa wameruhusu wazazi tu kuweza kwenda mochari kuiona miili ya vijana wetu hii imekuwa hivyo ili kuruhusu uchunguzi uendelee.
Nitahitimisha kwamba: Kwakuwa sote tunasubiri matokeo ya uchunguzi kama nilivyoeleza hapo juu, naomba wazazi na jamii ka ujumla tuwe ni wenye subira katika kipindi hiki kigumu lakini pia niwaombe wazazi kwa namna ya pekee tuwe na mawasiliano muda wote huu wa kusuburi ili tuweze kujua ni nini kinaendelea........Hatuwezi kujadili kwa undani tukio hili kwani lipo ngazi za juu na watakapotoa mrejesho ndipo nasi tunaweza kujipanga tuendelee namna gani. Wazazi nitawaomba tukutane Ofisi ya mwl. Mkuu ili tuweze kupanga namna ya kuelekea mochari na mambo mengine.........
Mkuu; cha kuzingatia hapo ni kutoruhusu majadiliano au maswali kwani yanaweza kuibua hoja usizotarajia na zinazoweza kuzua mtafaruku.
(Samahani nimezungumza kirefu mno kwani Hoja ya Uhai wa watu (Kifo) haielezeki kirahisi aisee).
 
Ok boss. Upo sawa.
 
Wanafunzi sita wa shule ya mtakatifu John Paul II ya mkoani Shinyanga walienda kutoa mahindi kwenye kihenge cha shule lakini yalishindwa kutoka wakiwa na mwalimu wa zamu katika usimamizi wa chakula, mwalimu alielekeza wanafunzi watatu waingie ndani kutafuta namna ya kuyafungulia kisha akaenda kunywa chai. Baada ya muda kupita, wanafunzi watatu waliobaki nje wakaona wenzao hawatoki na kutoa taarifa kwa walimu.

Walimu walipofika waliita bila mafanikio, wakavunja kihenge na kukuta wamezirai. Baada ya kufikishwa zahanati ya shule matibabu hayakuleta majibu na kukimbizwa hospitali ya Kahama ikathibitishwa wamefariki kutokana na kukosa hewa safi.

Kaimu kamanda wa Polisi, ACP Kennedy Mgani amesema Mwalimu wa zamu, Morris Sileo anashkiliwa na Jeshi la Polisi kwa kushindwa kusimamia vyema ili kubaini uchunguzi na chanzo cha vifo cha wanafunzi hao.
Dah!... poleni Sana
 
Probably ni kwasababu mahindi yaliwekwa dawa ya kuyahifadhi yasiharibike... Kuna dawa kama kidonge inawekwa mahali inasambaa kama hewa ndani ya chumba cha kuhifadhia mazao... Sasa ukikaa humo muda mrefu lazima ikuathiri
Zipo taratibu maalumu ambazo zinapasa KUZINGATIWA wakati mtu anapotaka kuingia kwenye kitu chenye 'enclosure' kama vile vihenge, visima au mashimo yafananayo na vitu kama hivyo.
 
Shule haina wafanyakazi? Wapo pengine,ila kwa kuwa mwalimu alikuwa mwalimu wa zamu akaona kuwabebesha wanafunzi mahindi itakuwa pengine adhabu tosha.Walimu watoto tukiwaleta shule hatuwaleti jkt mjitahidi kutoa adhabu zinazoendana na watoto.nadhani muda umefika haki elimu mnishirikishe kutengeneza matangazo yatawakumbusha pia walimu kuwa makini huko mashuleni na watoto wetu
 
Mtihani sana,Mweyezi Mungu wapokee kwa amani
 
Back
Top Bottom