Mkuu, mbona hadi hapo sasa limekuwa rahisi zaidi? Kumbuka wazazi wa hao wanafunzi marehemu hawapo hapo shuleni na mwl. wa zamu yupo kituoni na ingekuwa ni vizuri zaidi awe amewekwa mahabusu.
Mimi kama mwl. Mkuu cha kwanza ni kuwakaribisha wazazi hao hapa shuleni halafu nahakikisha mm nasimama upande wao kama mzazi mwenzao (ku-sympathize nao) wakati huo ni pamoja na kuisoma hali waliyokuja nayo wazazi (Je, wamekuja kwa shari au amani) halafu nafanya maamuzi: Kama wamekuja kwa Amani nitawaelezea kwa uwazi hali inavyokuwa kwa kawaida shughuli za kilimo hapo shuleni na tulivyokuwa tumezoea kufanya na nitaelezea jinsi shughuli husikailivyofanyika miaka iliyopita na ilivyoanza kufanyika mwaka huu tokea nitataja muda na wahusika na majuzi ilivyokuwa ..... lakini katika hali isiyo kuwa ya kawaida na ambayo hatukuitegemea tar..../05/2024 wanafunzi (nataja idadi ya wote waliohusika nje na ndani) walikwenda kufanya shughuli hiyo hiyo kama walivyofanya wenzao......ila kilichotokea ni kwamba baadhi yao (nataja idadi ya waliofariki) walikutwa wakupoteza maisha.
Nitaeleza.....Kwa kuwa jambo hili ni zito, lilitustua na linasikitisha ilibidi tuweze kutafuta msaada kutoka kwa wakubwa wetu Afisa Elimu (W), Polisi, Madaktari na kwa Wataalam Kilimo na Mifugo. Huko tulikoomba misaada wameonesha ushirikiano wa hali ya juu na kwa sasa Miili imepokelewa Hospitali kwa uchunguzi zaidi, Polisi wamemchukua mwl. aliyekuwa zamu ili kupata maelezo ya jinsi ilivyotokea, Afisa kilimo alifika kukagua kihenge husika na amechukua sampuli ya mazao yaliyokuwa yamehifadhiwa ili kuyachunguza.... na kwa kuwa tukioa hili kwa sasa lipo mikononi mwa wakubwa viongozi wetu na tunasubiri matokeo ya uchunguzi ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa, kwanza natoa pole kwa wazazi, jumuia ya shule na jamii kwa ujumla na tumeshauriwa na Hospitali kwamba kwa sasa wameruhusu wazazi tu kuweza kwenda mochari kuiona miili ya vijana wetu hii imekuwa hivyo ili kuruhusu uchunguzi uendelee.
Nitahitimisha kwamba: Kwakuwa sote tunasubiri matokeo ya uchunguzi kama nilivyoeleza hapo juu, naomba wazazi na jamii ka ujumla tuwe ni wenye subira katika kipindi hiki kigumu lakini pia niwaombe wazazi kwa namna ya pekee tuwe na mawasiliano muda wote huu wa kusuburi ili tuweze kujua ni nini kinaendelea........Hatuwezi kujadili kwa undani tukio hili kwani lipo ngazi za juu na watakapotoa mrejesho ndipo nasi tunaweza kujipanga tuendelee namna gani. Wazazi nitawaomba tukutane Ofisi ya mwl. Mkuu ili tuweze kupanga namna ya kuelekea mochari na mambo mengine.........
Mkuu; cha kuzingatia hapo ni kutoruhusu majadiliano au maswali kwani yanaweza kuibua hoja usizotarajia na zinazoweza kuzua mtafaruku.
(Samahani nimezungumza kirefu mno kwani Hoja ya Uhai wa watu (Kifo) haielezeki kirahisi aisee).