Wanajeshi wa Uingereza wanaacha kazi ya jeshi licha ya malipo bora

Hivi unafahamu miaka ya nyuma ya mwanzoni wa uhuru wahindi walikuwepo jeshini? Na wengine walistaafu kabisa na vyeo vyao vya juu?

Na machotara wengineo walikuwepo jeshini?
Ukianzia comment niliyotoa na swali nililouliza mwishoni, kisha ukaja swali nililoulizwa na jibu nililotoa hapa uliponukuu utaona majibu ya swali lako hili.

Mimi naelezea kwanini Wahindi siku hizi hawajiungi jeshi, wewe unauliza kama najua zamani walijiunga. Sasa comparison ya kujua nowadays hawajiungi jeshi ningeipataje.
 
Sababu kubwa ni kwamba hakuna maisha bora kwa wanajeshi baada ya kuacha jeshi kwani muda wa kukaa jeshini kwa kawaida ni miaka 4 ndo unakuwa discharged.

Sasa utakuta wengi wao wamepigana Afghanistan, Iraq na kwingine lakini baada ya kuwa discharged wanakuwa na shida ya kupata kazi na ndo huangukia kwenye ulevi na wengine wanakuwa na ile hali yaitwa PTSD au post-Traumatic Stress disorder.

Hawa wote wanokumbwa na hali hizi ni wale wa vyeo vya chini khasa wale privates na wengine huishia kuwa madereva wa mabasi na kadhalika.

Pia wengi wao sasa hivi wafanya kitu chaitwa UpSkilling na wapo katika vyuo vikuu wakifanya kozi zinohusiana na masuala ya ulinzi na usalama pamoja na masuala ya aviation.

Na wenzetu wazungu kwa kutambua hali hiyo, vyuo vikuu vingi sasa hivi vyatoa kozi mbalimbali kwa ajili ya ex-army ili kuwapa ujuzi wakiishatoka humo jeshini.

Wakimaliza hapo hufungua makampuni ya ushauri elekezi au kufanya kazi kwenye makampuni na mashirika makubwa duniani kama washauri elekezi ila hawa ni wale wa vyeo vya juu.

Ukitaka kuwatambua angalia makampuni mengi ya risk management na crisis management utawakuta humo.

Na si hao tu hata polisi nao wengi huacha baada ya miaka miwili au mitatu wakilalamika paperwork nyingi ingawa sasa hivi wengi hupewa laptops wazitumie kuandika statements. Hawa polisi huenda kusoma kozi kama policing na cloud management na pia hufanya kazi za ushauri elekezi.

Mimi nazungumzia real situation kwani wengi nimekutana nao katika harakati za hapa na pale duniani, na mkiketi na kuteta huanza kumwaga stories.
 
Kati ya nchi zinachokuliwa kawaida na Uingereza ni Urusi. Are you kidding us?
 
Kwahiyo kwa uelewa wako Western front iliishia Dunkirk mwaka 1940?

Operation Market Garden ya 1944 unaijua ilifanywa na nani na ilikuwa na ukubwa kiasi gani?

D-Day landings unazijua?

Nani alimtoa Hitler Ufaransa, Uholanzi, North Africa, Denmark?

Nani alivunja mabwawa ya umeme, alivunja submarine pens za German u-boats, nani aliweka naval blockade kwa Ujerumani. Nani alilipua Ruhr industrial complexes?
Soviets waliomba misaada kwa Marekani. I have evidence, unabisha?

Na hata wasingeomba, kwanini walipokea kama hawakuhitaji? Umaskini na njaa havina baunsa, walikuwa wachovu.

USSR walikuwa na intel makini alafu mwaka 1939 wakashirikiana na Ujerumani kuivamia Poland, mwaka huo 1939 wakaivamiwa Finland. Alafu wakawa isolated na kila jirani, kisha 1942 wakavamiwa na Ujerumani mpaka Marekani ikatoka mbali uko kuja kuokoa jahazi.
Ndivyo ulivyofundishwa intelijensia kali inakuwa hivyo?😂😂
Soviets walipambana sababu walivamiwa. Marekani na Uingereza hazikuvamiwa.
Unaona tofauti ya mwenye akili na mvivu kichwani, Waingereza walifanya evacuation wanajeshi wao wakawa sehemu ya fighting force. Warusi walikuwa wanatoa mhanga jeshi, sometimes bunduki moja kwa wanajeshi wawili.

Matokeo yake Uingereza ilipata casualties kama 500k wakati Urusi 27 million. Mjanja nani hapo?
Ndio maana nikakuambia Hitler alijimaliza alipofahamu Soviets wanakaribia Berlin na si France wala Britain au baba yao US....
Uingereza na Marekani walikuwa busy kuikomboa Ufaransa kisha Uholanzi, kisha kuingia Ujerumani. USSR na Ujerumani zilikuwa zimeiteka Poland pamoja hivyo technically USSR ilikuwa inapakana na Ujerumani.

Sasa kilichofanya USSR wafe kama kuku ni nini kama sio upuuzi.
Wajerumani walikufa 5 million wakipigana fronts mbili, Warusi wakafa 27 million front moja alafu eti Soviets roho ya paka 😭
Soviets wanapigana kama vibaka, wanakufa kwa sifa. Hawataki akili bali nguvu tu, sasa ona ulivyo mshamba unawasifia hawana air superiority. Sasa hilo jeshi la superpower au mgambo.
Uingereza, Ujerumani zinapigana kama watu wenye akili timamu.
Soviets sio waoga elewa hilo kwanza, Germany ilidhani ingewatisha kwa kuwaua wengi pale Kursk lakini kila wanapokufa jamaa wengine wanakuja na mzuka wanaanza moja , m@mae... Germans wakaona hawa ni alien ama watu, wakaanza kurudi nyuma wenyewe....
Na Soviets wakafa kama kuku, hata Wajerumani wenyewe waliovamia hawakufa hata 25% ya idadi ya Warusi. Bado huoni nani alikuwa boya vitani?
Britain walikuwa wanakimbia vita, vita ya ujanja ujanja, ndio maana France shoga yake alipigwa akafuatwa hadi kwake Paris huku Britain yupo hoi akitizama shoga yake anaolewa ndoa ya mkeka na mjerumanj na jamaa kaufyata....
Aliyeikomboa Ufaransa nani kama sio Uingereza na Marekani, Urusi iliikomboa nchi gani ukiachana na yenyewe tu?
Wakati Ufaransa inavamiwa, USSR si ilikuwa inalamba viatu vya Ujerumani mwaka huo.
Hitler ujanja wake na nguvu zake ziliishia kwa Soviets...

Ndio maana hadi leo hakuna mpuuzi na NATO yote atajitoa akili mbele yao.
Soviets ndio walivamiwa na Ujerumani.

Inashangaza wewe kutaka Uingereza na Marekani ndio iwapige Soviets. Ni wanajeshi sifuri wa Ujerumani walikanyaga ardhi ya Uingereza. Ni wanajeshi sifuri Wajerumani walikanyaga ardhi ya Marekani. Ni mamia ya maelfu ya Wajerumani waliivamia USSR.

Kitendo cha kuitaka Marekani ipigane na Ujerumani ndio unarudi palepale kudhibitisha kuwa USSR haikuwa na nguvu hizo unazoipa. Vita ya Kagera ila unawalaumu Wakenya kutokufa sana, walivamiwa wao?
 
Mkuu, kuhusu hapo mwisho kwa majeshi ya kisovieti.

Majeshi ya kisovieti (pamoja na vifo vyao vingi) ndo yaloingia mjini Berlin mwezi April 1945 na Adolf Hilter kutafuta kitanzi cha kujinyongea.

Hiyo ilitokea baada ya vita kali iloitwa "Battle of Berlin" iloendeshwa na majeshi ya umoja wa Kisovieti na ndo ilopelekea kutokea kwa kiloitwa "The Fall of Berlin" ambapo serikali ya kinazi ya Karl Donitz ilijisalimisha.

Majeshi ya umoja wa kisovieti yalikuwa yamelenga kuingia Berlin tangia mwezi January 1945 kutokea Kusini na Mashariki mwa mji wa Berlin kuwasaka manazi.

Yaaminika Hitler alijinyonga terehe 30 April 1945 na baadhi ya majeshi yake yakendelea kupigana huku yakikimbia kuelekea upande wa kaskazini magharibi ambako tarehe 8 Mei 1945 yalijisalimisha kwa majeshi ya Ulaya Magharibi au Western Allies.

Kama hufahamu ni kwamba historia ya hizi vita kuu ya kwanza na ya pili imekuwa ikichakachuliwa kidogokidogo ili kupindisha ukweli halisi wa kilichotokea khasa pale vita kuu ya pili ilipoishia, ndo maana Russia tarehe yao huwa ni tarehe 9 Mei na Ulaya Magharibi ni tarehe 8 Mei.

Ila ukweli wabakia kuwa ni majeshi ya Russia (pamoja na idadi kubwa ya vifo vya wanajeshi wake) ndo walotia timu mjini Berlin kuumaliza unazi na kupandisha bendera juu ya Reichtag mwezi Mei mwaka 1945.

Yapo mengi kuna manazi walozaliwa baada ya hawa walojisalimisha na wapo walokimbia barani Ulaya na kusambaa Duniani kote na leo ukisikia kuna wazungu wenye misimamo mikali wasopenda wageni katika nchi zao basi ufahamu kuwa huenda wana vinasaba vya manazi.

Vinasaba vya unazi vikimaanisha kuwa wao ni super race na ndo wenye haki miliki ya Dunia hii.
 
Wanawaza watatumwa Iran au Yemen kwa wanaojua kujilipua.
 
Wamenusa shughuli pevu in the near future!
Uingereza inapenda vita, na wanatamani kinuke kule kwa Putin ili ipeleleke askari kibao. Wanajeshi wamestukia kuwa wanataka kupelekwa kwenye vita isiyo na masilahi ya kitaifa, bora kuchomoa sasa hivi.

NB: ni hisia zangu.
 
Ni kweli mmarekani alimkodisha vifaa vya kijeshi Ila urusi alipigana akakomboa inchi nyingi ndio akaunda USSR ndio maana walikufa wengi.Hata nchi za magharibi zinakili urusi alitumika Sana na inasemekana Hitler alifanyia makosa kuvamia Urusi
 
Duh!!!! Wacha-mbuzi wengine bhana!!!!
It's comical.
 
Ni kweli mmarekani alimkodisha vifaa vya kijeshi Ila urusi alipigana akakomboa inchi nyingi ndio akaunda USSR ndio maana walikufa wengi.Hata nchi za magharibi zinakili urusi alitumika Sana na inasemekana Hitler alifanyia makosa kuvamia Urusi
Soviet Union ilizikomboa nchi gani vita ya pili ya dunia mkuu?
 
Tupe darasa mkuu.
 
Jamaa mahaba yanampofusha...
 
Hizi zilizojiunga na NATO kama Estonia na zingine
Estonia ilikuwa ni sehemu ya Soviet Union. Ni sawa na useme USSR iliikomboa Russia.

Siijui nchi iliyokombolewa na Soviet Union ila nazijua nchi zilizovamiwa na Soviets kwenye hiyo WW2.
 
Umetisha mkuu kwa hii simulizi...
 
USSR ilikuwa kubwa hivyo kusema Russia ndio iliipiga Ujerumani ni kauli za pro-Russians kutaka kuikuza. Peke yake ni jeshi la kawaida mbele ya Uingereza au Ujerumani kwenye rekodi za vita zote.

Ukraine somehow sio wepesi kwenye battle na kwenye WW2 akili za USSR ziliamini defensive lines zilizopo Ukraine zitatosha kabisa kumsimamisha adui. Hata kwenye doctrine za Cold War, Ukraine ilikuwa na defensive lines nyingi na concentration kubwa ya jeshi.

Urusi iliwahi pigwa na Japan wakasuruhishwa na Marekani, iliwahi wekewa naval blockade na Uingereza kwenye bahari yake yenyewe.
Poland baada ya WW1 waliipiga Urusi ikiwa yenyewe. Sasa eti nchi ilipigwa na Poland inalinganishwa na mababa wa vita.
Nchi iliyokuwa inapigana na vi-Georgia na Latvia ingeishinda vipi nchi kama Uingereza wakiwa peke yao. Wakati Uingereza ilizoea kupigana na wababe kina Ufaransa, Hispania.

Imperial Russia ilikuwa inaambulia kuwapiga Waturuki na baadae Ottomans ila wazungu wenzake inateseka kasoro Napoleon aliyeshindwa na hali ya hewa.
 
Huelewi nini hapo?, France alivamiwa shoga yake Britain kajipeleka kuokoa jahazi, wakapigwa wote ,askari wakapitia Dunkirk kwa misaada ya mitumbwi ya wananchi wenye huruma 🤣

Nitabaki na jibu moja tu, Soviets ndio walimmaliza Hitler, hata hapo juu umeambiwa lakini bado umekaza fuvu unataka kurefusha mjadala...

PAsipo SOviet kujitoa kiume kupambana ana kwa ana na Germans, West na wao wangekufa tena wengi sana, damu ya wasoviet ndio ikawa pona ya hao west....
Britain ilikuwa imemalizwa wamebaki wanachechemea, ndio maana baada ya hitler kuahirisha, hakuw na hofu sana kuichukua Britain, historia inasema hakuwa na wasi wasi kama amepoteza hilo eneo lakini alijua atarudi ndipo akaenda akamalizwa na Soviets...
Wajerumani walikufa 5 million wakipigana fronts mbili, Warusi wakafa 27 million front moja alafu eti Soviets roho ya paka 😭
Germany ilipeleka vifaru elfu kumi na askari milioni 3, halafu wakarusha na ndege , waliingia na hio mbinu yao waliita blitzkrieg..

Halafu kasome historia vyema na uache uongo, askari wa Soviet walikufa inakisiwa kati ya 8 millions hadi 10 Miliions, ukichanganya na vifo vya raia wa Soviet ndipo inafika around 24 Mils, ho askari milioni 27 umetolea wapi?

Soviets wanapigana kama vibaka, wanakufa kwa sifa. Hawataki akili bali nguvu tu, sasa ona ulivyo mshamba unawasifia hawana air superiority. Sasa hilo jeshi la superpower au mgambo.
Uingereza, Ujerumani zinapigana kama watu wenye akili timamu.
Nilishatizama vita kwenye documentary, askari wa USA wanavamia Afghanistan, ni kituko cha karne, nikasema kama jeshini ndio hivi ndio maana na mashoga wanapatikana kwenye majeshi yao, wale jamaa ni walaini sana, kidogo tu wanaita air support, unaona A10 hio inapita kushambulia, Taliban walikuwa wakiwagusa kidogo tu jamaa hao wana radio wanalia hadi machozi wanabubujikwa wanataka air support, ukiangalia umbali walipo na ha Taliban utacheka, karibia km 5, yaani machine guns mtu ana shoot ana shoot miti na ile kuwa fukuza jamaa wasisogee....

Hao vita hawawezi na ni waoga, anayepigana man to man ni Russians tu...
Ukiwaweka Taliban 500 na askari wa US 1000 kwenye uwanja wa mapambano hakuna air support, nakuambia na ninakuhakikishia askari wa US wanamalizwa wote....

Hakuna jeshi la ovyo na vituko kama hao NATO wkiongozwa na US, wana uchumi, wana silaha, wana vifaa lakini vita ni sifuri... Ndio maana unaona Israel inapelekeshwa na kikundi cha Hamas hadi wanatoa mlio....

NATO ni hovyo ..... hakuna cha us3nge wa NAVY SEAL wala ushuzi wa Army Rangers labda kwenye movies, jamaa ni chapati...

Ndio maana hadi sasa NATO wanaogopa na kujitafakari kuingia RUssia, ndio maana unaona askari wa Britain wana left jeshi, ni majitu maoga sana....



Alivamia kweli Soviet lakinisi si ndipo ikawa mwisho wake... tandikwa hadi Berlin, akajua Soviets ni walaini walaini...
 
Hio ya Poland, Poland alikuwa ana ji defend, kingine ile vita Russia waliamua yaishe na si kwamba Poland ina uwezo kupambana na Russia, hata hawakuwa na motivation, Poland walipambana ili kuishi... sio hata vita ya kutolea mfano ni upuuzi tu...
 
Kwa technology ya zamani, lakini sasa hivi vyuma vinakufuata uko uko Uingereza. Makombola yanapiga London kama kawaida. Na wakicheza kisiwa kinazamishwa. Mijamaa ya Russia ilikuwa inasema kwa vile UK wana midomo sana na kimbele mbele ni bora kuzamisha hicho kisiwa kwa kombora moja la nguvu litakalosukuma mawimbi ya maji na kuzamisha kisiwa chote. Dunia ya sasa siyo ya zamani kutumia bunduki kulenga adui. Sasa hivi kuna drones, ballistic missiles inapigwa toka bara kwenda bara. Sasa hivi NATO wanaofia makombola ya kisasa ya Russia yanabeba vichwa 12 kila kichwa kinapiga sehemu yake kilipopangiwa, na hakuna kudunguliwa. Hayo yakipigwa mawili tu Uingereza ni majivu kote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…