Maandamano hayo yaliongozwa na viongozi wa dini, na wananchi walijitokeza kwa wingi kupinga matendo ya mapenzi ya jinsia moja.
Hali hii imetokana na baada ya vikundi vya kutetea mapenzi ya jinsia moja duniani kuzidisha kasi na msukumo wa kuhalalisha matendo hayo.
Tuliona presha nchi ya Qatar iliyopigwa wakati wa kombe la dunia.
Tukashuhudia vitabu vinavyofundisha mambo hayo vikisambazwa ktk shule za watoto.
Tumeshihudia shule fulani ambayo watoto wanafundishwa kufanyana kinyume cha maumbile.
Huko Kenya mahakama ya juu ikaruhusu uanzishwaji wa NGOs za kutetea ushoga ktk nchi hiyo.
Na kuna baadhi ya madhehebu ya dini duniani yameanza kurasimisha ndoa za jinsia moja na kuna Mengine yamebaki na msimamo uleule wa toka zamani wa kukataa mambo hayo machafu.
Kwa mfano hapa Tanzania Kanisa la Anglican la Tanzania limekataa katakata kukubaliana na kanisa la Anglican la Uingereza kuruhusu ndoa za mashoga. Katika barua ambayo uongozi wa kanisa la Anglican la Tanzania limeliandikia kanisa mama la Anglican la uingereza, Limegoma kabisa kukubaliana na msimamo wa kanisa hilo la Uingereza kuhusu kuruhusu ubarikio wa ndoa hizo.
Kwa bahati mbaya pia, kanisa la Kikatoliki huko Ujerumani limepiga kura kuruhusu ubarikio wa ndoa za Jinsia moja kuanzia mwaka 2026. Hii inafuatia kauli ya Papa ya kuwatakia "Rehema( Grace)" watu wote hata wale wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Hapa chini ni video ya wananchi huko Arusha kuandamana kupinga mambo ya ushoga.
View attachment 2547164
View attachment 2547165