Wananchi mkoani Arusha waandamana kupinga Ushoga

Papa kuombea Neema kwa maana ya neno ulilotumia (grace) haina tatizo lolote na haina maana ya kuunga mkono ushoga. Tunapowaombea wadhambi neema ya msamaha haimaanishi kuunga mkono dhambi. Ni kuomba Neema ya Mungu iwafikie waweze kuongoka na kuwa watu bora katika maisha.

Pili, pamoja na maandamano ya kupambana na ushoga, pia kunahitaji mikakati mipana zaidi ya hilo ili kuinua nguvu ya kupinga na kufifisha nguvu ya uungaji mkono.

Ushoga uko sponsored na unaendeshwa na watu ambao wanatambua nguvu ya fikra (mind). Hivyo wanatumia akili katika fikra pana sana na uko katika program endelevu iliyosukwa kwa ubora. Hapa panahitaji kufikiria vizuri kunielewa maana ukifikiria katika mipaka ya kihisia, kikanda, kiimani, kitamaduni n.k. utafikiri na mimi nataka kusupport ushoga.

Jiulize, je tangu ushonga umeanza kusikika ukianzia huko ulaya na kwingineko, haukupingwa? Je, ulipoanza kuingia Africa na Tanzania, haukupingwa? Je, sheria hazitungwi kuupinga? Lakini je kati ya tunaopinga na tunaunga mkono, ni upande upi unaoonekana kusonga mbele kila siku? Enzi hizo kwa Tanzania, mtu kujulikana ni shoga tu ilikuwa ni aibu lakini siku hizi tuko nao, tunakula nao, ni rafiki zetu, kwenye kamati za harusi, VIKOBA, kwenye dini zetu, wengine wanatufadhili na kutupa mitaji au kutusaidia kwa njia mbalimbali na tunawajua. Wanatupikia vyakula kwenye mahotel, tunapeana mikono ya jambo nao kila siku, hawa wanazidi kusonga mbele.

Swali ni je, maandamano haya na mengine yataweza kuzuia ushoga na mashoga wasizidi kusonga mbele? Kisaikolojia, kuna mambo ambayo kwa kadiri unavyopaza sauti ya kuyazuia ni kama maji ndivyo unavyoyapa nguvu ya kusikika na kuwafikia na kuvutia wengine zaidi. Hivyo mashoga hawatishwi sana na maandamano, zaidi wanaona hiyo ikiwa fursa kwao kwamba ushoga sasa unasikika na kuzungumzwa kila kona ya dunia kama jambo la kijamii, sio la aibu tena kuzungumzwa. Hii kwao ni mafanikio.

Je, nataka kusema tuache tusiseme au kuupinga ushoga? La hasha, lakini tunauzuiaje, tunaupingaje kwa mbinu zipi na vichocheo vyake ni vipi?

Haya ni ya kujiuliza kwa kina na kuwa na njia bora na mathubuti. Kujipanga wengi bondeni kunaweza kusiwe njia bora sana ya kuzua mkondo wa maji kupita au hata kuwasomba kama kusimama kwenu hakutaungamanishwa na njia nyingine za kimkakati zaidi na zenye kuimarishwa kimifumo katika jamii nzima.

Tusitumie mihemko, tujue mbinu na tutumie mbinu, kwa sauti tu za mihemko hakika hii vita itakuwa ngumu na hata waandamanaji wa leo tusishangae kesho tukiwaona wakiandamana kuomba haki ya upande wa pili.

TUTAFAKARI VYEMA
 
Malezi yalishatetereka leo kinachoonekana ni matokeo ya kutofundisha watoto wetu kuwa na mipaka na kiasi katika kila jambo
 
Zipo kwa PC anguu zimejaa kibao,

Siku nikipoteza PC au kuibiwa, cjui ntaweka wapi uso wangu.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23] kumbe unaogopa tena..
 
Je hayo maandamano yatazuia ushoga?

Mashoga wanaingiliwa na wanawake??? Hao hao waandamanaji ndio mashoga buyers
 
Wanaandamana kwa ajili ya nani,ujumbe wao wamelenga kumfikishia nani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…