Wananchi mkoani Arusha waandamana kupinga Ushoga

Wananchi mkoani Arusha waandamana kupinga Ushoga

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Maandamano hayo yaliongozwa na viongozi wa dini, na wananchi walijitokeza kwa wingi kupinga matendo ya mapenzi ya jinsia moja.

Hali hii imetokana na baada ya vikundi vya kutetea mapenzi ya jinsia moja duniani kuzidisha kasi na msukumo wa kuhalalisha matendo hayo.

Tuliona presha nchi ya Qatar iliyopigwa wakati wa kombe la dunia.

Tukashuhudia vitabu vinavyofundisha mambo hayo vikisambazwa ktk shule za watoto.

Tumeshihudia shule fulani ambayo watoto wanafundishwa kufanyana kinyume cha maumbile.

Huko Kenya mahakama ya juu ikaruhusu uanzishwaji wa NGOs za kutetea ushoga ktk nchi hiyo.

Na kuna baadhi ya madhehebu ya dini duniani yameanza kurasimisha ndoa za jinsia moja na kuna Mengine yamebaki na msimamo uleule wa toka zamani wa kukataa mambo hayo machafu.

Kwa mfano hapa Tanzania Kanisa la Anglican la Tanzania limekataa katakata kukubaliana na kanisa la Anglican la Uingereza kuruhusu ndoa za mashoga. Katika barua ambayo uongozi wa kanisa la Anglican la Tanzania limeliandikia kanisa mama la Anglican la uingereza, Limegoma kabisa kukubaliana na msimamo wa kanisa hilo la Uingereza kuhusu kuruhusu ubarikio wa ndoa hizo.

Kwa bahati mbaya pia, kanisa la Kikatoliki huko Ujerumani limepiga kura kuruhusu ubarikio wa ndoa za Jinsia moja kuanzia mwaka 2026. Hii inafuatia kauli ya Papa ya kuwatakia "Rehema( Grace)" watu wote hata wale wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Hapa chini ni video ya wananchi huko Arusha kuandamana kupinga mambo ya ushoga.



 
Tumeridhika na utumwa na ufisadi wa CCM ila ushoga tumekuwa wepesi kuu pigia kelele na kuu kataa.

Aisee hili taifa.
Unasemaje vile? Aise! Mi niko tofauti na baadhi ya sera za uongozi wa ccm lakini linapokuja suala la ushoga niko tayari kuanza na kukaripia kwa nguvu zote ushoga ndipo mengine yaendelee.

Hapa usiendelee kabisa vinginevyo utakuwa upande huo.
 
Unasemaje vile? Aise! Mi niko tofauti na baadhi ya sera za uongozi wa ccm lakini linapokuja suala la ushoga niko tayari kuanza na kukaripia kwa nguvu zote ushoga ndipo mengine yaendelee.

Hapa usiendelee kabisa vinginevyo utakuwa upande huo.
Huo ni mtazamo wako, huu ni mtazamo wangu. nawe una uwanja wa kutoa maoni.
 
Back
Top Bottom