ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 83,659
- 90,151
Shida Iko wapi? Si mtajengewa nyingine?Sasa tupo mahala si salama kama shule inaweza kufutwa kwa ajili ya mwekezaji.
Inaanza kuwa new normal . Years back mwekezaji binafsi alijipa jukumu la kufanya tathmini ya nyumba za watu binafsi vingunguti jijini ,Lukuvi akiwa ardhi chini ya magufuli zoezi lilifutwa na baada ya awamu hiyo zoezi lilirudi kwa kasi na tathmini ya kuondoa watu kwa ajili ya mwekezaji mmoja ikaendelea . Sijawahi kujua serikali inaondoaje watu kwa matumizi yasiyo na manufaa ya umma .
Sasa leo nimekutana na habari kuwa shule ya public inaweza kuezuliwa ili mwekezaji mmoja aweze kunufaika na eneo kwa maumivu ya public . Video inaonyeasha wananchi wakilalamika kuhusu watoto wao wadogo waliositishwa masomo hasa residents wa eneo husika.
Watanzania kama kuna asset tuliyokuwa nayo ya kujivunia ni ardhi. Kila mmoja alikuwa na uwezo wa kumiliki ardhi in one way or the other . Ni dhahri kwa kipindi hiki tunatawaliwa na watu wabinafsi wasiojali public interests . Ardhi imeanza kuingia sokoni kama bidhaa nyingine zozote ndo maana unaona inaanza kuuzwa kwa billions kwa watu wachache. Nyerere alituheshimisha kwa hilo no wonder ungeweza kumkuta mtu ana kibanda cha nyasi kariakoo . Hii ilikuwa na maana sana kwenye land ownership . Watawala wenye mlengo wa ubepari ukichanganywa na ubinafsi ni hatari sana na tutashuhudia mengi .
kwa hili la kuuza public property kwa individual watanzania tuamke kwanza tupewe majibu na ila pia beneficially ni nani , ni kwa manufaa ya nani na nani yuko nyuma yake ila pia ardhi kama asset pekee iliyobaki baada ya kila tulichokuwabnacho kugawiwa tuipiganie kwa hali na mali kabla hatujawa kama wakenya.
Ruksa kutoa povu.
Wewe ukigundua Madini kwenye nyumba Yako utaivunja au utaiacha 😁😁