Wananchi wa wilaya ya Mlimba, Morogoro wachoma magari na vifaa vya wapima ardhi

Inategemea wataalamu waliingia na lugha gani,unaweza kuta hata mwenyekiti wa kijiji hakujulishwa,wanakijiji wana lugha zao hasa ikizingatiwa kwamba kuna mgogoro,

Kuna mwaka Fulani watafiti kama sikosei kutoka SUA walichomwa moto wote na gari lao waliingia maporini huko bila taarifa
 
Lazima atakua keshapewa briefing tayari...!
DC yupo, DED yupo, OCD yupo wote wanazingizia wananchi hawana matatizo huko Mlimba. Mlimba Kuna matatizo makubwa,badala ya kwenda kuwasikiliza wananchi watatumwa polisi kuwakamata.

Wananchi ni vichaa kwenda kuchoma magari moto? Iundwe time kuchunguza tukio hilo. Sio kuanza kamata kamata mkifanya hivyo mlimba nyumba zitabakia na yatima wananchi watatimkia mikoani serikali itaanza kupeleka misaada ya kwenda kutunza teza raia.
 
Yaani hapo no DC naanza na madiwani wote , wenyeviti wote wa vijiji halafu kijiji kinakuwa kwenye quarantine kwa mwezi mzima. Kuluh nalah mulluhu
 
Umeongea point za msingi.
 
Wananchi hawawezi kukurupuka from no where na kushambulia maafisa ardhi na kuchoma magari yao bila sababu za msingi. Hapo lazima kuna kitu ni vyema wananchi wakapewa fursa ya kusikilizwa badala ya kuwapiga virugu na kuwakamata
Kweli kabisa. Nakubaliana na wewe.
 
Trust me , punde si punde kuna majitu yatalia na kusaga meno fasi ya mlimba wamechoma ndinga ya serikali, bodaboda ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania na tripod stand ya serikali pia wamewadunda watumishi wa umma wakiwa wanatimiza majukumu yao
Kafie mbele!Uonevu ukizidi serikali kwa wananchi matokeo yake ndiyo haya.
Kwa taarifa yako nchi nzima kituo kinachofuata ni polisi
 
Hawa wanaoitwa wawekezaji hasa uwekezaji wa ardhi wanatakiwa wakati wote wawasikilize wanachokitaka wananchi waliopakana nao,mambo kama haya unakuta muwekezaji kwa sababu anajuana na mkurugenzi wa wilaya au ana vishoka wake kwenye halmashauri anaamua kujikatia pande la ardhi wakilalamika wananchi wanaambiwa watulie hawayajui matumizi ya ardhi mwisho yanatokea haya.
 
Ni kweli kabisa. Wawekezaji wa ardhi inabidi kufanya jitihada za kuwahusisha wanakijiji wanaopakana nao kwenye mipango mbalimbali ya ardhi wanazomiliki, itasaidia kupunguza migogoro ya aina hii.
 
Mungu wangu
 
Duh, wameenda mbali zaidi, akili haikutumika, jela inawasubiri. Ujinga una gharama kubwa
Utakamata wangapi kwa matokeo hayo hiyo ilikuwa ni mob war labda wajitutumue kwa mamlaka yao kukamata yeyote ila kikubwa ni sheria zifuatwe kati ya wawekezaji,maafisa ardhi na wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…