Wananchi wa wilaya ya Mlimba, Morogoro wachoma magari na vifaa vya wapima ardhi

Wananchi wa wilaya ya Mlimba, Morogoro wachoma magari na vifaa vya wapima ardhi

Wananchi wenye hasira wamewashambulia watumishi wa Ardhi kutoka wilaya ya Mlimba na kuchoma magari, pikipiki pamoja na vifaa vyao vingine wakati wakiendelea na zoezi la uhakiki wa mipaka ya mashamba yanayogambaniwa na muwekezaji na wananchi wilaya ya Mlimba, Morogoro.
Watumishi wa ardhi waliokua kwenye hilo zoezi wamejeruhiwa vibaya, japokua hakuna kifo kilichorpotiwa hadi sasa.
View attachment 1885041View attachment 1885043View attachment 1885046View attachment 1885047

Pole pole tutafika tu.
 
Watakamatwa wachache. Migomo ya chuo walikua wanaitwa ring leaders.

Ila hii nchi tunachukuliana poa sana.
 
Mimi naona hasira za hao wananchi zimeishia tu sehemu ambayo sio sahihi. Hao wataalam wao wana kosa lipi? Wao walienda tu kupima hiyo mipaka.

Japokua pia nadhani ni muhimu kwenye ishu kama hii, wakienda next time waende na ulinzi wa polisi wenye silaha za kutosha.
Waende na silaha kwa wananchi?

Halafu unajiita Dr ?
 
Sipati picha wananchi walivyojazana huko porini sasa hivi kujificha wasikamatwe😀
 
Mimi naona hasira za hao wananchi zimeishia tu sehemu ambayo sio sahihi. Hao wataalam wao wana kosa lipi? Wao walienda tu kupima hiyo mipaka.

Japokua pia nadhani ni muhimu kwenye ishu kama hii, wakienda next time waende na ulinzi wa polisi wenye silaha za kutosha.
Sip kwenda na ulinzi lazima wananchi washirikishwe na serikali ya Kijiji haya Mambo kufanya bila kushirikisha wananchi madhara yake ndo hayo sasa
 
Sawa captain kinjekitile ngwale unaamini utaweza kupambana na mwenye bunduki wewe ukiwa na rungu,
Hapo najua lazima polis wataenda kutembezea jando wakaz wa hilo bushi ili next time wajue nini maana ya mali za serikali na watumishi wake
Huo ni upumbavu na ujinga wa mtu asiyeenda shule ,anayeamini bunduki pekee ndiyo itakayo msaidia wakati wote .Asilimia kubwa ya polisi na viongozi wa CCM (Including you) wanaamini strength yao Iko kwenye bunduki (Indeed stupidity) .Hakuna marefu yasiyo
Kuwa na nchi uvumilivu wa bunduki unakikomo.Hata kama Elimu yenu duni jifunzeni ya duniani.USA Ilifika sehemu polisi anapiga magoti kwa wananchi(Huku ndiko kuelemika)
Polisi tunaishi nao mitaani ,Polisi tunakunywa nao mitaani,polisi hao hao tunakumbana vikumbo kwa mangi kujikopa unga!..
 
Dah haya mambo sio kabisa nakumbuka vizuri nilimpoteza kijana alikua mwanafunzi wangu kutoka chuo cha madini alikua field kwenye hicho Kituo cha Utafiti was Udongo Selian Arusha

Alifariki mtoto wa wait

Inasikitisha,asante kwa kunikumbusha hii habari,kumbe ilikuwa kutoka Chuo cha Selian
 
Huo ni upumbavu na ujinga wa mtu asiyeenda shule ,anayeamini bunduki pekee ndiyo itakayo msaidia wakati wote .Asilimia kubwa ya polisi na viongozi wa CCM (Including you) wanaamini strength yao Iko kwenye bunduki (Indeed stupidity) .Hakuna marefu yasiyo
Kuwa na nchi uvumilivu wa bunduki unakikomo.Hata kama Elimu yenu duni jifunzeni ya duniani.USA Ilifika sehemu polisi anapiga magoti kwa wananchi(Huku ndiko kuelemika)
Polisi tunaishi nao mitaani ,Polisi tunakunywa nao mitaani,polisi hao hao tunakumbana vikumbo kwa mangi kujikopa unga!..
Hili ni tatizo mtu yeyote akitumia akitumia akili anaonekana ccm, kwa taarifa yako mimi sina chama na sijawahi kuipigia kura ccm katika chuguzi zote ukicha 1985 tulivyompigia mwinyi kura ya ndio nadhani kipindi hicho wewe ulikua bado ume kwenye karanga mimi ni free thinker boko likitolewa lazima niseme polis wakitendewa uovu lazima niwasemee, diwan wa ccm akionewa na lazima niseme mwananchi akitoa boko lazima niseme maana hatupo kwa mashindano
 
Sip kwenda na ulinzi lazima wananchi washirikishwe na serikali ya Kijiji haya Mambo kufanya bila kushirikisha wananchi madhara yake ndo hayo sasa
Dr anashauri waende na polisi wenye silaha, sasa sijui hizo silaha za nini kwa wananchi ?

Inasikitisha sana
 
Kijiji gani kimehusika na tukio hili?je ni Idete,Namawala,Mbingu,Mngeta,Ikule,Mkangawalo,Chita ,Mpanga,ama wapi hasa?
Mwekezaji anaitwa nani je ni KVTC,KPL ama nani ?
 
DC yupo, DED yupo, OCD yupo wote wanazingizia wananchi hawana matatizo huko Mlimba. Mlimba Kuna matatizo makubwa,badala ya kwenda kuwasikiliza wananchi watatumwa polisi kuwakamata.

Wananchi ni vichaa kwenda kuchoma magari moto? Iundwe time kuchunguza tukio hilo. Sio kuanza kamata kamata mkifanya hivyo mlimba nyumba zitabakia na yatima wananchi watatimkia mikoani serikali itaanza kupeleka misaada ya kwenda kutunza teza raia.
Tatizo la nchi hii ni viongozi kuona kuwa matatizo ya wananchi ndio mtaji wao wa kisiasa!!wanakuja wanawadanganya hivi wanaondoka, hali ikifikia hivi ndio unaona serikali yote inahamia hapo, na kujifanya kuwa tatizo hilo ni jipya?!!wanalitatua ndani ya wiki moja tu baada ya maafa kuwa yametokea!!ndio unajiuliza mgogoro wa miaka zaidi ya 10, unakuja kumalizwa ndani ya wiki moja tu.walikuwa wapi muda wote huo?!!
 
Thamani ya Vifaa vyote hapo pamoja na Gali si chini ya milioni 250. Hasara yote hii atagharamia nani?

Hakukuwa na njia sahihi ya wao kuwasilisha malalamiko yao hadi kufikia hatua hii?

Nashauri Viongozi muwe mnatembelea site kutatua migogoro mapema kabla hatujafika huku, Wakuu wa Idara za Serikali na Wakuu wa Wilaya msikae maofisini. Andaeni ratiba ya angalau kila wiki mnapita Vijijini huko kusikiliza kero na malalamiko ya Wananchi mnao waongoza.

Wananchi si kila mgogoro unatatuliwa kwa mabavu, kuna hatua za kufanya kuwasilisha malalamiko yenu. Kuna Serikali za Mitaa/Vijiji, Diwani, Mbunge, Mkurugenzi, Mkuu wa Wilaya n.k

Serikali ione namna sahihi ya kuziba ombwe hili mapema kabla mambo hayajawa mabaya zaidi.
 
Wananchi wakiwa hawajakubaliana na serikali haina hata haja ya kuwaambia nini cha kufanya
 
Back
Top Bottom