Wananchi wa wilaya ya Mlimba, Morogoro wachoma magari na vifaa vya wapima ardhi

Wananchi wa wilaya ya Mlimba, Morogoro wachoma magari na vifaa vya wapima ardhi

Ningekuwa katika kamati ya kushughulikia hilo tatizo ningeweka ndani wanakijiji wote waliohusika pamoja na hao wapimaji ardhi ili ijulikane mbivu na mbichi

Kwa nini walienda kufanya kazi siku isiyo ya kazi?

Uharibifu huu umechangiwa na pande zote mbili waswekwe ndani wote
 
Huwezijua,mambo ya mulungula hayo,wapimaji watakuwa walisimama kwa mwenye nacho.
Watu wakichoka na uonevu ndio haya ya;
Mulimba
Tunduru
Mimi naona hasira za hao wananchi zimeishia tu sehemu ambayo sio sahihi. Hao wataalam wao wana kosa lipi? Wao walienda tu kupima hiyo mipaka.

Japokua pia nadhani ni muhimu kwenye ishu kama hii, wakienda next time waende na ulinzi wa polisi wenye silaha za kutosha.

Inategemea wataalamu waliingia na lugha gani,unaweza kuta hata mwenyekiti wa kijiji hakujulishwa,wanakijiji wana lugha zao hasa ikizingatiwa kwamba kuna mgogoro,

Kuna mwaka Fulani watafiti kama sikosei kutoka SUA walichomwa moto wote na gari lao waliingia maporini huko bila taarifa
Hata mwaka 2018 kule Dodoma watafiti wa sijui kilimo kwanza walipoteza maisha
 
Uzoefu wangu. Mara nyingine katika issue kama hizi watu wawe makini sana.
Huwa inatokea: Wale wavamizi halisi bila kupepesa macho ndio wanakuwa wachochezi wakuu, halafu mambo yakipamba moto, haooo!!! Wanaenda sehemu na kusikilizia! Halafu..…."kichekoooo!!!"
 
Inategemea wataalamu waliingia na lugha gani,unaweza kuta hata mwenyekiti wa kijiji hakujulishwa,wanakijiji wana lugha zao hasa ikizingatiwa kwamba kuna mgogoro,

Kuna mwaka Fulani watafiti kama sikosei kutoka SUA walichomwa moto wote na gari lao waliingia maporini huko bila taarifa
Hapana, hawakuwa wa SUA bali walikuwa wa kituo cha utafiti Kilimo Selian Arusha. Hawa jamaa wa Melela ni wakorofi tu maana hata viongozi wa kijiji walikuwapo nao wamechezea mfueni!
 
Wananchi wenye hasira wamewashambulia watumishi wa Ardhi kutoka wilaya ya Mlimba na kuchoma magari, pikipiki pamoja na vifaa vyao vingine wakati wakiendelea na zoezi la uhakiki wa mipaka ya mashamba yanayogambaniwa na muwekezaji na wananchi wilaya ya Mlimba, Morogoro.

Watumishi wa ardhi waliokua kwenye hilo zoezi wamejeruhiwa vibaya, japokua hakuna kifo kilichorpotiwa hadi sasa.

View attachment 1885041View attachment 1885043View attachment 1885046View attachment 1885047
Qubbake tatizo nini mpaka kufikia hatua hiyo?
 
Hakuna Mkuu wa Wilaya huko kuwajulisha hali halisi? Au kama kawaida yao waliamua kudharau malalamiko ya Wananchi!? Nawaunga mkono Wananchi dhuluma na udhalimu vyote vinakithiri kwa kasi ya kutisha. Sasa watakamatwa hovyo hovyo na kupewa mkong’oto wa kufa mtu kisha kabambikiwa kesi hata ambao hawakuhusika.
Kosa kubwa sana hili, inaonekana walichukulia poa au hawakuwa wanajua hali halisi.
 
Sehemu yenye mgogoro ilikuaje hao wapima ardhi kwenda bila ya kua na ulinzi?
Wanajikutaga miungu hao watu hasa ukikuta wanataka kufanya dhuluma kwa wananchi, wana majibu ya hovyo, adi wanatukana na unakuta ardhi ni ya wananchi kihalali kabisa kuna mahali nilisumbuana nao miaka 3 adi haki ikatendeka yaan hao wananchi naelewa hasira zao wangetoka na ulemavu kabisa wanakera mnoo
 
Hizo hasira wangezielekeza kwenye kudai katiba mpya wangefanya la maana sana
 
Waende na silaha kwa wananchi?

Halafu unajiita Dr ?
Sasa mkuu hilo si eneo la mgogoro? Unajua migogoro ya ardhi kati ya wawekezaji na wananchi inavyokuaga na balaa...?
Ni muhimu kujihami na ulinzi ili waweze kufanya kazi yao kwa amani kama wataalamu. Unajua kwenye hili tukio walikwepo hadi viongozi wa kijiji ila na wao walidundwa vile vile na hao wananchi?
 
Back
Top Bottom