Mkuu, consensus ya kumaliza mgogoro inafanyikaje wakati mipaka yenye mgogoro haijapimwa bado? Kinachogombaniwa kati ya mwekezaji na wananchi ni mipaka.... Wananchi wanadai mwekezaji kajitanulia mipaka na kuchukua hadi eneo la vijiji vyao; Mwekezaji anadai mipaka yenye usahihi ndio hiyo; Hatua ya kwanza ni wataalamu wa ardhi kwenda na ramani za ardhi eneo husika, kisha kufanya upimaji na kulinganisha kilichopo kwenye makaratasi ya ardhi na kilichopo kwa ground ili kuweza kutambua mipaka sahihi ili haki itendeke sasa wakiwa mezani wakati consensus inatafutwa.
Sasa hilo litafanyikaje ikiwa wananchi hawa hawaruhusu? Ulinzi wa polisi ni ili kuwalinda wataalamu wakati wanafanya kazi yao, wasipate madhila na wala sio kumnyang'anya mtu ardhi yake.