Wananchi wa wilaya ya Mlimba, Morogoro wachoma magari na vifaa vya wapima ardhi

Hii kitu si nzuri kwa raia kujichulia sheria mikononi
Lakini pia huenda lile wimbi la UNANIJUA limerudi, wale wenye nacho wanapora kwa kutumia wale watu wanawalipa mshahara na ile Haki yako anapewa mwenye mrungula , uporaji wa ardhi kwa jina la uwekezaji ndio jina la mchezo wenyewe.

Watauawa
 
Kuwapiga risasi ndiyo kutamaliza mgogoro?
Hapana..lakini wakifanya vurugu katikati ya utatuzi wa huo mgogoro ambazo zina hatarisha uhai wa watu wengine lazima polisi waingilie kati hata kwa kuwavunja miguu.

Maana hao wanakijiji na wao kwa kuharibu mali na kuumiza watu sio kutatua mgogoro huo.
 
washukuru MUNGU hawakuuwawa. Je wangeuwawa?

Mpaka kufikia hatua hii maana yake wananchi waliona upumbavu wanaofanyiwa umevuka mipaka, wakaona namna ya kutuliza ghadhabu na hasira zao na ili kuwepo kuheshimiana ni kutekeleza walichofanya.

Serikali itoe fundisho hapo, yasije yakatokea na ya kuzidi hayo yalotokea.
 
Nyie ndio mtu anaharibu mali za uma mnasema asikilizwe ana tatizo gani.

Umeshahalibu mali,utetezi hauna nafasi kwa wakati huo.
 
Walichofanya wananchi siyo kitendo kizuri, ila waliosababisha huo mgogoro wanapaswa kuwajibishwa zaidi kwa kuwa wao ndio sababu ya wananchi kujichukulia sheria mkononi.
Walichofanya wananchi ni makosa ya wale waliosababisha mgogoro katika eneo hilo, tungeanza kudili na wale waliosababisha haya yote kutokea, wananchi ni sehemu ya matunda ya mgogoro huo, tumalizane kwanza na mizizi ya mgogoro kisha turudi kwa wananchi waliosababisha hasara kwa wataalamu wasio kuwa na hatia.
Wananchi wakichoka kutumia akili basi watatumia nguvu na hakuna nguvu ya wananchi itakayoweza kumalizwa bila uwajibikaji.
 
Kuna watu wenye hasira walichoma kituo cha Polisi - Bunju DSM... kama masihara sasa watumikia kifungo cha maisha
Kuna wale walichoma Gari la Ardhi kule Dodoma na kuua wale wataaalam kwa kisingizio cha Wanyonya damu. Aysee walijuta mpaka leo Kijiji kizima wamebaki na makovu watalipa hizo gari mara tatu yake
 
Trust me , punde si punde kuna majitu yatalia na kusaga meno fasi ya mlimba wamechoma ndinga ya serikali, bodaboda ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania na tripod stand ya serikali pia wamewadunda watumishi wa umma wakiwa wanatimiza majukumu yao
Majukumu gani ya kuwahujumu wananchi na kumpendelea mchina?
Kwanini huyo muwekezaji asikwende kuwekeza kwao? Nyambafu
 
Sawa captain kinjekitile ngwale unaamini utaweza kupambana na mwenye bunduki wewe ukiwa na rungu,
Hapo najua lazima polis wataenda kutembezea jando wakaz wa hilo bushi ili next time wajue nini maana ya mali za serikali na watumishi wake
Wananchi wakiamua hizo bunduki wataziweka chini na kutimua mbio, hapa ni maamuzi tu. Wewe Kama ni mumoja wa hao wenye bunduki usijivune na kujiamini sana tenda haki. Maana usipotenda haki ipo siku bunduki unayoibeba ndiyo itakayokuua. Weka kumbukumbu ya maneno yangu dogo.
 
Kuna watu wenye hasira walichoma kituo cha Polisi - Bunju DSM... kama masihara sasa watumikia kifungo cha maisha
Walipangiwa hivyo pindi tu walipozaliwa. Kwa iyo huko kwenda kuchoma kituo cha polisi ni forces of nature iliwasukumiza hili jinsi walivyopangiwa watumike vifungo vya maisha itimie na itiki.

Jiulize wangapi wamechoma vituo vya polisi na hawatumikii vifungo vyovyote? Ni kwasababu hawakupangiwa.
 
Zingine Zimeshindikana wakaamua watumie hiyo nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…