Isanga family
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 17,080
- 33,076
Kujenga sio kugumu Mkuu watu wasingejenga...hicho kibanda sio cha kukijadili..Hakuna anaye mtisha mtu bali tunaongea uhalisia nyumba hiyo kwa milion 6, ni hakuna hata mtoto hawezi kubaliana na uongo huo labda kama aliijenga mwaka 2008 au 2010.
Ni bora kuwaambia watu ukweli ili wajue ugumu wa kitu ili akiamuwa kukianza awe amejipanga kuliko kumpotosha alafu aingie kichwa kichwa imtoe barabarani.
Kwa makadirio ya chini hii nyumba mpaka sasa imesha kula si chini ya million 11mpaka 13.
Uongo mtupu! hakuna kitu kama hiki labda ni nyumba ya tope umeweka plasta tu
Duu hivo vyumba vyote vinaenea kwenye hiyo nyumba?Haifiki tofali 2000 hio. Labda 1,400 hivi. Nyumba inaonekana ni ya vyumba viwili vya kulala,sebule,jiko dogo na Choo. 6m kiugumu anaweza kutoboa.
Jiko dogo,Choo vina ukubwa gani? Hata vyumba hivyo viwili vidogo 3*3Duu hivo vyumba vyote vinaenea kwenye hiyo nyumba?
Aiseee 3*3.... hongera zake.Jiko dogo,Choo vina ukubwa gani? Hata vyumba hivyo viwili vidogo 3*3
Haijaanza kuongea kiingereza hapo
Hiyo nyumba ni ndogo, na pia haijaisha kwa 100%. Ila kuijenga mpaka hapo ilipofikia kwa milioni 6 pekee, aisee inahitaji uwe na moyo mwepesi sana kuamini.
Haijaanza kuongea kiingereza hapo
Kwani huyo jamaa wa insta alitumia sh ngapi?Ukiwa unafanya kitu na huna hela ya kutosha kisimamie vizur utajua tatizo wewe unapga gharama mpaka za mtu kukusimamia jitambue broo usibishe kwenye vitu hujawahi fanya
Ngoja tuongeze;Tofali ngapi?
Bati ngapi?
Saruji mifuko mingapi?
Mchanga je?
Ebu weka mchanganuo
1 | Tofali laini 1100, kwa shs @900 | 990,000.00 |
2 | Sement shs | 1,000,000.00 |
3 | Mabati | 1,200,000.00 |
4 | Mbao | 600,000.00 |
5 | Nondo | 400,000.00 |
6 | Kokoto za lenta | 210,000.00 |
7 | Ufundi na kibarua ni yeye mwenyewe | 800,000.00 |
8 | Mengineyo | 800,000.00 |
| Jumla | 6000,000.00 |
Nyumba ya milioni 13+ yeye anasema milioni 6Iga ufe mkuu🤣
Afu kiwanja ni sehemu ya hiyo 6M au?Hahaha........... Mkuu Glenn kwahiyo jamaa anatupiga fix hapa tuingie kujenga kichwa kichwa kwa milioni 6 aliyosema alafu tuje tufe kwa Presha ya nyumba kuishia kwenye lantor 😂😂