Wanaochanganya Damu mbichi ya n'gombe kwenye vyakula vya kuku wana nia ya kutufarakanisha na Mungu

Wanaochanganya Damu mbichi ya n'gombe kwenye vyakula vya kuku wana nia ya kutufarakanisha na Mungu

Walokole mfuge kuku zenu msichanganye na damu , ni nyie mmekatazwa sio kila mtu.
Kumbe Adam alikuwa mlokole ☑️🤣

Sasa wewe kumbe ulitokea wapi ikiwa Adam Si Babu Yako?
 
Salaam, shalom!

Baada ya Mungu kuruhusu mtu kula nyama, alimkataza Kula Damu ya mnyama. Yaani ukichinja myama au ndege, Damu yake hupasi kuitumia Kwa matumizi ya chakula, ni machukizo maana ndani ya Damu ya m yama, mna uhai. ( Mwanzo 9:4).

Sasa Kwa kuwa shetani ni baba wa Hila, baada ya kuona wengi wameacha kula Damu ya mnyama, amegeuza Mpango, hivi sasa vyakula vya kuku vinachanganywa na damu wakileta sababu uchwara za kuwa Damu inaongeza Kasi ya ukuaji nk nk kumbe lao Moja, ni kutulisha Damu indirect, tukila kuku aliyekula Damu nasi tupatwe na adhabu ya Mungu Kwa kutotii.

Ushauri: Wafugaji tengenezeni vyakula vya kuku ninyi wenyewe mkiepuka kuweka au kuchanganya Damu kwenye vyakula vitumikavyo Kwa kuwapa mifugo kama kuku nk nk.

Karibuni 🙏
Kuku akila mavi ukija kumla huyo kuku kwani unakuwa umekula mavi?
Tafakari mtu wangu.
 
Kumbe Adam alikuwa mlokole ☑️🤣

Sasa wewe kumbe ulitokea wapi ikiwa Adam Si Babu Yako?
Ndio maana kila siku nakuambia hata hiyo ya adamu ni hadithi wala haina uthibitisho wowote , tena imekopiwa kwenye hadithi za kale zaidi za wasumerian , ndio maana wewe unaeeza kuamini vyovyote utakavyo wala sio tatizo
 
Kwa hiyo ukila kuku wa kupikwa huwa wala damu yake?
HOJA hapo ni ,hakuna faida yoyote apatayo kuku Kwa kulishwa Damu ya n'gombe mbichi zaidi ya kutaka kutufarakanisha na Mungu wetu sie walaji.
 
HOJA hapo ni ,hakuna faida yoyote apatayo kuku Kwa kulishwa Damu ya n'gombe mbichi zaidi ya kutaka kutufarakanisha na Mungu wetu sie walaji.

Hakuna faraka yeyote na Mungu mkuu...

Walichokatazwa wanadamu wa wakati huo kula/kunywa ni damu ya mnyama (kwenye damu kuna uhai) lakini si kwa vyakula walavyo wanyama...
 
Back
Top Bottom