Wanaofanya mazoezi ya mbio (jogging) hayana faida kiafya, ni matokeo ya matangazo ya biashara ya Nike

Kazi na shughuli za kila siku ni mazoezi ndio ,ila yale mazoezi ya kutenga mda yana umuhimu sana.

Kwa sababu yanaandaa mpaka saikolojia yako ki mazoezi .

Ipo tofauti kubwa sana kati ya mazoezi ya kutenga mda , na shughuli za kazi za kila siku.

Kama ni kazi kila mtu anafanya, na kutembea, ila upo umuhimu wa kutenga mda wa zoezi hata kama ni dakika 15 tu kila siku .
 
I mostly do push ups na nilianza tangu nikiwa o- level na hii ni baada ya siku moja kupewa adhabu ya push ups niliamka na maumivu since that day nikaamua kuendelea na matokeo nimeyaona nina zaidi ya miaka kumi nilipoacha nilikuwa dhaifu sana sana, sasa hivi nipo fit zaid ya fit nayaona matokeo kabisa kabisa pia uwa napenda kutembea kwa miguu mara moja moja jogging inahusika. Yani huwezi nambia nikakuelewa wakati nayaishi unachokipinga nakushauri anza hata wewe mazoezi madogo madogo.
 
Mkuu uyo haelewi anachojaribu kukifikisha yani mimi kwanza nikiacha napata shida sana na matokeo ya mazoezi nayaona nina miaka zaida ya kumi naa nayaishi.
 
Mkuu uyo haelewi anachojaribu kukifikisha yani mimi kwanza nikiacha napata shida sana na matokeo ya mazoezi nayaona nina miaka zaida ya kumi naa nayaishi.
Mimi nipo na Maveterani muda kipindi hiki mara nyingine nachezea Timu ya vijana kuruka koni huko na kucheza sana mpira nina mwezi wa pili nyama za paja zinauma sana nimeamua kupumzika kidogo madhara yake nayaona kabisa harafu pana mtu anakuja kusema tusifanye mazoezi daah...
 
Kazoea kuuweka mwili bila kufanya mazoezi kama mtu umezoea ni mateso angejua hata hasingeongea anacho ongea nimemshangaa sana.
 
Kutembea ni bonge la zoezi

Ova
 
Kukimbia kwa wiki labda mara 2
Unaweza kujikuta unakimbia sana
Mpaka ukajikuta unaunguza carolies zako ,kwenye kukimbia inataka kiasi
Usikumbie kupitiliza

Ova
 
Huyo mzungu ni wa kupuuzwa. Ila ni kweli mazoezi ukizidisha lazima uzeeke. Sura inajikunja. Kukimbia kilometa zisizozidi 3 ni sahihi kiafya. Mazoezi makali ya kukimbia lazima yakuletee shida kwenye magoti. Wanariadha wengi wakifika uzeeni hupambana sana na goti. Na kama unapenda kukimbia jitahidi kula vitu vinavyosaidia kuongeza lubricants kwenye magoti na sehemu zingine mifupa inapoungana. Mtu kama dronedrake hapaswi kufanya jogging maana kila siku anapoteza lubricants nyingi kupitia nyeto.
 
Mkuu unafuatilia maelezo ya professor janabi kuhusu kula na unamuona yeye muonekano wake alivyo watanzania tunapenda kula ndio tatizo.
 
Hiyo ni kweli mkuu. Hata uki- skip lunch, dinner moja kwa siku si vibaya na ni nzuri kiafya.
Hata professor janabi alishawahi kuelezea siku moja kuhusu kula hovyo na kufanya mazoezi bila kupima heart beat kwasababu kuna uwezekano wa kupata heart attack au cardiac arrest watu wanakimbia kimbia tu ndio maana wachezaji licha ya kufanya mazoezi ila wana dondoka na kufariki wakati mwingine.
 
Hahahahahah anapoteza uloto tu dronedrake
 
Kitu kama hicho hata mimi namuunga mkono ila sio kwenye swala la mazoezi. Chai hata mimi mara nyingi sinywi ila mazoezi nikifanya naona faida zake kwangu na sio kwa kuambiwa.
Kabla haujaanza kufanya jogging lazima kwanza ufanye vipimo vya kucheck moyo kama upo sawa sasa watu wanakimbia kimbia tu it's very dangerous for their health.
 
Hivi mwili hauwezi kuchoma mafuta wenyewe tu kwa hali ya kawaida ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…