Wanaokimbilia Ndoa za Bomani ili kuoa zaidi ya mke moja, uhalisia ni tofauti, sheria zitakubana sana hautaweza kuongeza mke mpaka mkeo akubali

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Kwa watu hasa wakristo ambao ndoa ya dini zao huwaminya kubanana na wake zao mpaka kifo na wanatafuta mbadala wa kufunga ndoa kwa mataraajio ya kuongeza mke hapo mbeleni, huwa wanadhani ndoa ya serikali / bomani ndio mbadala.

Uhalisia ni kwamba, ndoa ya bomani zipo za aina mbili, ya kwanza ni mme moja na mke moja ambayo mkifunga huruhusiwi kuongeza mke, ya pili ni ya mke zaidi ya moja ambayo inabidi mke wako mtarajiwa akubali na aweke sahihi kwamba umeamua kumuoa lakini huko mbele ya safari unaweza kuongeza mke

Ni mwanamke gani asie na wivu na mum wake mtarajiwa atatia sahihi ya aina hii ya ndoa ? Yaani aache kusaini ndoa ya kumlinda yeye aende kusaini ndoa ya kufungulia milango wanawake wengine ?

Hapa ndipo inapokuja shida ya ndoa za bomani, mwanamke atasaini ndoa ya kufugia milango wake wa ziada, ni ngumu sana akubali kuweka sahihi kwenye ndoa ya kukuruhusu kuongeza mke.
 
Ila kama dini zinawafanya watu wabanane mpaka kifo na ndoa ishaanza kuwa chungu ndani ya mwezi moja huwa sipati picha hapo kama nyumba ndogo inakwepeka
 
Umenikatisha tamaa kweli kweli, nikajua na huko ni rahisi mno. Sasa wataalam waliopitia haya watuletee uzi wa kuweza kumfanya mwanamke akubali uke wenza. Ndoa za mitala raha sana, mke mmoja hatoshi.
 
Sheria ya ndoa ya Tanzania inatambua ndoa 3. Ambazo ni

1. ndoa za kidini, ambazo ni ndoa ya kikristo na kiislam

2. Ndoa ya kiserikali

3. Ndoa ya kimila

Ndoa zinazoruhusiwa mitala bila mwanamke kukubali.. ni ndoa ya kiislam na ndoa ya kimila
 
Cheti cha ndoa cha serikali ndio hichohicho hutolewa Bomani, kanisani au msikitini. Cheti ni kimoja na kinatambulika kote huko.

Kile cheti kina sehemu ya ku-tick au kuchagua kuwa ndoa yenu ni ya aina gani. Kuna ya mke mmoja na wake wengi.

Kwa mimi mkristo nilikuta tayari mchungaji ameshatick pale kwenye kibox cha mke mmoja😀😀 nadhani ili kuondoa uwezekano wa mimi kuweka tick kwenye kibox cha wake wengi bila wengine kuona.
 
Hii sheria ya kumwomba mke atoe idhini ili uongeze mke Kenya waliipiga panga bungeni ingawaje wabunge wanawake wali mind sana kwamba inamyanyasa mwanamke......naona wanaume waliwazidi kwenye wingi wa kura. Ni wakati sasa serikali ikarekebishe hii sheria ili mwanaume aweze kuamua kuongeza mke bila idhini ya mke ili kupunguza idadi ya wanawake wanaokosa waume kwa kigezo cha mke aliyetangulia kukaba penati. Hii pia itapunguza nyumba ndogo na watoto wasiojulikana ndani ya ukoo na familia kwani sasa mambo yatakuwa hadharani.​
 
Cheti cha ndoa cha serikali ndio hichohicho hutolewa Bomani, kanisani au msikitini. Cheti ni kimoja na kinatambulika kote huko.

Kile cheti kina sehemu ya ku-tick au kuchagua kuwa ndoa yenu ni ya aina gani. Kuna ya mke mmoja na wake wengi.

Kwa mimi mkristo nilikuta tayari mchungaji ameshatick pale kwenye kibox cha mke mmoja😀😀 nadhani ili kuondoa uwezekano wa mimi kuweka tick kwenye kibox cha wake wengi bila wengine kuona.
Mchungaji alicheza kama pele😂😂😂
 
Kwa watu hasa wakristo ambao ndoa ya dini zao huwaminya kubanana na wake zao mpaka kifo na wanatafuta mbadala wa kufunga ndoa kwa mataraajio ya kuongeza mke hapo mbeleni, huwa wanadhani ndoa ya serikali / bomani ndio mbadala.

Uhalisia ni kwamba, ndoa ya bomani zipo za aina mbili, ya kwanza ni mme moja na mke moja ambayo mkifunga huruhusiwi kuongeza mke, ya pili ni ya mke zaidi ya moja ambayo inabidi mke wako mtarajiwa akubali na aweke sahihi kwamba umeamua kumuoa lakini huko mbele ya safari unaweza kuongeza mke

Ni mwanamke gani asie na wivu na mum wake mtarajiwa atatia sahihi ya aina hii ya ndoa ? Yaani aache kusaini ndoa ya kumlinda yeye aende kusaini ndoa ya kufungulia milango wanawake wengine ?

Hapa ndipo inapokuja shida ya ndoa za bomani, mwanamke atasaini ndoa ya kufugia milango wake wa ziada, ni ngumu sana akubali kuweka sahihi kwenye ndoa ya kukuruhusu kuongeza mke.
Oa kienyeji tu hakuna Cha Cheri Cha ndoa,akizingua vuta mzigo mpya
 
Mimi siombi ruhusa mwanamke nikitaka ongeza mwingine...mapenzi ni hisia sio kupeana miongozo.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom