Wanaomiliki Toyota Starlet wanaonekana vituko wakiwa mjini na Vigari vyao

Sasa kama unalielewa hilo mbona uwasimange wenye starlet? Kwamba toyota ilikosea sana kutengeneza aina hiyo ya gari?
Hapo kwenye starlet Aisee hapana kama hela haitoshi jitahidi uendelee kujichanga uvute gari la kueleweka na sio kuharakisha kununua gari mwishowe ni aibu tu mnajitia barabarani
 
Unaweza kua na kichwa kikubwa kumbe ufikiriaji ukawa hafifu ona kama hizi dharau mnawasema Hawa je kwa sisi tulio na vibaiskeli tusemaje
 
Kazi ya gari ni nini,?
 
Acheni ubishi hayo magari yanawatia aibu na mnadharaurika sana huku mtaani.

Ushauri wangu.; Msiharakishe maisha kwa kutaka magari ya bei rahisi kama kipato hakitoshi endelea kujichanga utafute gari bora na sio bora gari.

Daladala zipo ni mara kumi upande daladala huku tunachanganyikana na kila aina ya watu wa hali tofauti tofauti kuliko kupata aibu na masimango ukiwa na hicho starlet
 

Natafuta kazi, nina ujuzi wa kusimamia biashara kwa miaka 5


Huna akili mtoa mada tafut kwanz kazi
 
Daladala ni kero sana
 

Mkuu tuliza akili, Starlet ni moja ya gari ambazo bei iko juu Sana Japan, IST na wenzake wanasubiri.
 
Miliki japo baskeli uone matatizo ya kumiliki chombo cha kueleweka
 
Hakuna anayekosoa hela ya nauli labda mtu mwenyewe apende kwenda sehemu flani kama huna nauli hujalazimishwa kutoka

Kwani anayekosa nauli na mwenye gari anayekosa mafuta wanatofauti gani
Wewe kumbe Bado kula kulala Yani hujui kuwa maisha na utafutaji vinaweza kukulazimisha kwenda sehemu hata kama nauli huna au ndo nyie mnaolala sebureni kwa shemeji zenu hata usipotoka nje ukashinda unachezea remote utakula tu?
 
Wewe kumbe Bado kula kulala Yani hujui kuwa maisha na utafutaji vinaweza kukulazimisha kwenda sehemu hata kama nauli huna au ndo nyie mnaolala sebureni kwa shemeji zenu hata usipotoka nje ukashinda unachezea remote utakula tu?
Mume WA mtu mtarajiwa huyo.... Anongea hizo shiiit kama wakike
Wakati naolewa nilimkuta mume wangu ana Corolla ya zamani....
8 yrs ago....mpaka Leo nakuona mwanaume maana kitu kilikua akina hata ac.....lakin alikua anapambana.....nilibadili mentality from there....chako ni chako.....at least sikupanda madaladala......na ilikua yetu .....period
 

Tunachokosea waswahili ni kuangalia gari bila kujua uhitaji wa mtu!!

Mimi nimejipima, nimeona mahitaji yangu ni Starlet!! Why not?? Na kwa nini wewe ucheke?

Nitatoa mfano na niliwahi kuutoa tena!! Mimi miaka mingi nyuma nilinunua Daihatsu Terios, kwa sababu nyingi moja ikiwa fuel consuption na pili ni mashamba, ninayo kadhaa huko porini sasa habari za kuacha gari mahali upande bodaboda ndiyo nilikataa!! Terios inapasua vichaka na vilima kama haina akili nzuri na mjini najigamba vilevile ukiikuta ni namba AS!! Nilikaagiza mwenyewe!!

Then mtu kama wewe akikaona kachafuu anakurupuka gari gani hii uza nunua hata rumion au gari kubwa!! Hell no! Utakula hasara mafuta utayotumia, mie hata yapande vipi nateleza nayo tu pori kwa pori!!

Kitu cha kwanza tuache utoto wa kujaji watu na wanavyomiliki, hujachangia hata kumi na inawezekana hata babako hana!! Pili; Mtu ananunua chombo kuendana na mahitaji na shughuli anazofanya wakati mwingine unaweza kumuona kwenye starlet inampa urahisi kufanya delivery ya kazi zake mijini wewe unamcheka mwenzio yupo kwenye ofisi!! Nyumbani kapaki ndinga ya maana!!
 
Kwanini uendelee kupata magonjwa mtambuka huko kwenye daladala zisizo jaa. Wakati unaweza miliki huu mtoko na usiwe na wasiwasi wa EWURA Hata waweke bei elekezi lita Kwa 10,000 au vita ya Ukrainia iendelee Hata miaka 10,000.

Practical speaking chuma ni chuma muhimu kiwe na tairi alilogundua Robert William Thomson hapo mwaka 1846.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…