GE2025 Wanaopinga uteuzi wa Samia wataje wagombea wao ili tumpime

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kwa nini hawakupinga siku ya uchaguzi na walimchagua kwa kura 100%? Kwa nini hawakupinga siku hiyo ya uchaguzi kuwa huo siyo utaratibu? Why now? Mwezi January hawakujua kuwa huo siyo utaratibu?
Haiondoi uharamu huo
 
Usiingize ukristo kwenye hii issue. Ni heri ungesema wanambagua kwenye suala la jinsia kwa sababu wengine wametamka wazi kuwa hawataki kuongozwa na mwanamke. Unataka kusema wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM waliomchagua kuwa mgombea uRais wote ni waislam?
 
Wananchi: Tunataka tupate rais wa kuchaguliwa sio kurithi tu

Chawa: hata huyu alchuguliwa, si alikuwepo kwenye karatasi ya kupiga kura.

Wannchi: awamu yake imeisha tayari, aachie ngazi.
Chawa: Ndo anaanza sasa, pale alikuwa anatuvusha. Tunae hadi 2035.

Wananchi: huyu si awamu ya 5?
Chawa: hii ni awamu ya sita🤣.
 
Sisi tunamtaka Luhaga Mpina, mgombea mwenza awe Fatuma.
 

1.Mzee mkuchika
2.Makongoro Nyerere
3 .Mtaka
 
Kama ni hivyo wasiompenda wamkatae Samia kwenye sanduku la kura. Ila Tume ya Uchaguzi nayo ndiyo hivyo tena!!!
 
Makamu wa rais na urais miaka 10, ishaisha tunahitaji mwingine
 
Kumbuka hakuchaguliwa na wananchi, alikaimu na huenda wenye chama wakaamua kuweka mtu wa kuchaguliwa na wananchi.

Mambo ya Biden kama nayaona
SSH hajakaimu nafasi ya Urais. Yeye ni Rais kamili baada ya kifo cha JPM.
 
Mm sikumchagua. Wamama wabaki kuongoza vikoba
Kwenye karatasi la kura mwaka 2020 kulikuwa na picha ya JPM kama mgombea urais na picha ya SSH kama mgombea mwenza ambaye anakuwa Makamu wa Rais; iwapo Rais anafariki akiwa madarakani yeye ndiye anakuwa Rais. Kwa hiyo kama ulimchagua JPM siku hiyo automatically ulimchagua SSH.
 
Kwani mlipomchagua kuwa Makamu wa Rais hamkufahamu kuwa yeye ndiye angekuwa Rais just in case Rais aliyeko madarakani atafariki? Au huo uanamke ndiyo mnaufahamu leo?
Siku daraja la busisi linafunguliwa nilikuwepo pale. Aisei niliiona baadhi ya watu hawakufirahi kazi kukamilika, walidhani halitamalizika ili iwe kete yao ya kumkataa Mama. Wale ambao walidhani bila Magufuli Kila kitu kingekwama Sasa hivi wameishiwa punzi, ndio maana wanajikita kwenye vitu vya hovyo vidogo vya utaratibu , utekaji sijui nini. Wanasahau kuwa akina Azori, saanane walipotea wakati w Magufuli.

CCM haijawahi kuwa fair kwenye chaguzi zoote tangu wakati wa Nyerere wa kuchagua ndiyo au hapana hadi kuengua wagombea, na wakati wote huo wanaCCM waliimba hiyenahiyena CCM nambari one.

Kama lowasa, kama wanadhani mgombea wa CCM ni dhaifu basi mgombea wao aende upinzani akachuane na mgombea dhaifu wa CCM badala ya kupoteza muda wao kumjadili mgombea wa CCM ambae amepitishwa na Mkutano Mkuu kama kawaida yao. Mkutano mkuu wanayo nguvu ya kumchagua hata chizi kama wakitaka kuwa mgombea wao. Magufuli alichaguliw kuwa mgombea kwa njia hii, alikuwa hategemei kuwa atachaguliwa.
 
Umpime wewe ukiwa kama nani?nenda kapimwe mkojo kwanza nyambaff
Magufuli aliteuliwa kuwa mgombea kwa mizengwe ya CCM na wajumbe wa mkutano Mkuu kumpitisha ingawa alikuwa hana sifa hata Moja ya kupitishwa. Bila mizengwe ile Lowasa angekuwa Rais, na bila mizengwe Ya CCM Membe angekuwa Rais.

Mnachokitafuta mtakipata CCM ni ileile ya mizengwe.
 
Hii comment yako ina ukweli kwa asilimia 100 anayepinga atakuwa ni miongoni mwa hao wanufaika wa serikali yake dhaifu.
Kuna watu ambao wako radhi Rais awe hata kichaa lakini wa kabila, dhehebu au Kanda yao.
 
Wagombea wenye nia wanatakiwa wapewe ratiba ya kuchukua form watakuja wenyewe. Acheni woga tangazeni tatehe ya kuchukua form. Chama dume kinaogopa kutoa form hii ni maajabu. 😂😂😂😂
 
Hakuna anayepinga wewe ,fuateni taratibu ,ruhusuni wagombea wachukue fomu then wapite kwenye mchujo kama Late JK Nyerere alivyosema ,ukitaka urais inabidi ujadiliwe ,waone kama unakidhi na siyo tu unampitisha kisa ni KABILA lako.
Kama membe angeruhusiwa kuchukua fomu na kushindanishwa na Magufuli hali ingekuwa mbaya kwa Magufuli. Tulieni msubiri 2030 au nendeni mgambee kupitia kwenye vyama vingine Kama CHAUMMA kama kweli sifa mnazo.
 
Gharama zipo juu lakini umeme umefika kila mahali, ni suala la muda tu gharama hizo zitashuka. Kuwa mpole punguza kulialia.

Uchumi unakua sana kwa taarifa yako, viwanda vilivyoanzishwa kwa miaka hii minne ni vingi kwani nchi imeweza kufunguka. Umeme umefika kila kona, usafiri unakuwa wa kisasa zaidi kadri barabara zinavyozidi kujengwa.
 
Tumia akili wewe unajua kwa nini gharama azishushwi ...? Labda ilo bwawa wapewe mafisadi kina rostam azizi ndiyo watashushq tena kidogo tu sababu ni kuoinda biashara zao za gesi waliyo tuibia kifisadi chini ya kikwete
 
Sikia mpumbavu huku
 

Attachments

  • Duh kiongozi kama huyu mchapa kazi kumpata tena ni mitano tena 🫣.mp4
    947.9 KB
Sikia mpumbavu huku
Kwa taarifa yako Samia ndani ya miaka minne amefanya mengi makubwa kuliko marehemu JPM aliyofanya kwa miaka mitano.

Tatizo lako hutembei huko mikoani unaishia kulialia tu kwenye mitandao ya kijamii ukiwa unaishi mijini.

Samia anamalizia SGR
Anamalizia ujenzi wa viwanja vya ndege
Anamalizia miradi ya umeme wa REA
Kaongeza uwekezaji wa bandari na hivi sasa mapato ni mara mbili kulinganisha na awamu ya marehemu.

Anafanya mengi sana lakini tatizo letu ni mahaba ya upofu kwa marehemu JPM pia tunasumbuliwa na kumuona Samia akiwa ni mwanamke wa kizanzibari.

Tazama mbali zaidi ya huo unyonge wa mawazoni mwako, utaelewa Samia anafanya nini muda huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…