Wanaosema kujenga ni kuzika pesa

Wanaosema kujenga ni kuzika pesa

Inategemea unajenga ili iweje[emoji849]

Ukijua asset na liability hutoumiza kichwa

Ukijenga nyumba uje ukae tu halafu uje uiuze 2050 miaka ya kati hapo umekupa pesa gani zaidi ya malazi yako binafsi na familia.

Ila kuna wanaojenga na kuzipangisha miaka yote inawapa pesa na still wakitaka kuuza wanapiga mkwanja mzuri hawa ndio wanmekula matunda ya pesa vizuri

Uchaguzi ni wako
 
Wewe hujui kitu kuhusu uwekezaji kwenye nyumba.

Nimeanza kupangisha nyumba yangu mwaka 2014 kodi laki 5.

Hapa katikati nikapunguza hadi laki 4.5 kwa ushawishi tu wa madalali kwamba vyuma vimekaza, kwahiyo wapangaji hawafiki bei.

Kwakuwa zama za vyuma kukaza zimepita, mzigo unarudi palepale kwa 500k!

Hakuna maintenance ya aina hiyo uliyosema kwenye nyumba kwa mwaka.

Maintenance ya nyumba sio kama service ya gari!
Hahahahaha jamaa hawaelewi hawa

Wanadhani ni gari la mkweche

Sometimes unaweza kuta nyumba iko poa tu mtu anaiweza ishi bila shida labda rangi tu ndio imefuba sasa mwenye nyumba mwenye kiherehere atataka apake tena rangi na kukarabati hiki nakile wala havina ulazima atajikuta anaingia cost za kijinga
 
Wanaosema kujenga ni kuzika pesa utawakuta wanatoa mifano ya kina Bakhresa, Mo Dewji hivi kwa akili yako kuna tajiri hana nyumba?

Hivi unasemaje kujenga ni kuzika pesa wakati bei ya nyumba inapanda kila siku? Hivi mtu aliyejenga nyumba Kariakoo miaka ya 1970s kwa shs laki 1 alafu amekuja kuiuza hiyo nyumba mwaka 2021 kwa billioni 5 utamwambiaje kwamba alizika pesa?
Wengi wao ni wale wa sizitaki mbichi hizi.
Wasikuumize kichwa mkuu.
 
Mimi naongea facts, siongei blah blah.
Nimerithi nyumba na ardhi. Nyumba ni headache na nimekatazwa na ukoo kuiuza.
Nyumba inaleta heshima kwa utamaduni wetu.

Kama heshima kwa jamii ingeweza kuwekwa thamani yake kifedha labda.
Ila huwezi.

Viwanja vina thamani inayokua. Hata by looking at the population increase. Mapori mengi ya miaka 15 iliyopita Sasa ni miji.

Nyumba haiongezeki thamani. Huo ni ukweli wa kimahesabu siyo hadithi njoo .
Huwezi kupigiana hesabu za nyumba ukanipa faida above interest rate ya Benki kuu.

Ukitaka tupigiane mahesabu hapa.
Unaweza vipi tenganisha nyumba na kiwanja bro.

Kiwanja kikiwa na nyumba thamani yake ni ya juu kuliko kiwanja kitupu.

Nyumba ina add value ya kiwanja
 
Unaweza vipi tenganisha nyumba na kiwanja bro.

Kiwanja kikiwa na nyumba thamani yake ni ya juu kuliko kiwanja kitupu.

Nyumba ina add value ya kiwanja
Kutokuweza kwako kutenganisha nyumba na kiwanja, ndio kunakoleta utofauti kati yetu.
Je, ni bora kuwa na nyumba mbili za milioni 80.
Au nyumba moja ya milioni 40 na viwanja vinne?
 
Unajenga kama Biashara au Unajenga kama Prestige au unajenga kujihifadhi ?

Kazi ya pesa ni matumizi unaweza kujenga ili mtaani wakutambue kwamba nyumba ya fulani (wewe hizo sifa unalala usingizi mnono na smile kubwaaa) kwahio hio kwako ni price worth paying; it makes you feel good...

Pili kama unajenga kama biashara it depends, sio kila nyumba italipa na sio kila location ipo sawa..., unaweza ukajenga kitu cha value kubwa kwenye eneo duni.... (location matters) kuna sehemu unaweza ukajenga ukabakia kufuga buibui...

Tatu watu wanaocheza hii game (ina kanuni zake) wanatumia hio nyumba wanayojenga kama mtaji wa kufanya mambo mengine, moja hawatumii pesa yao cash (either wanachukua loan au rent za wapangaji wengine ndio zinawajengea hio nyumba) wanaanza kidogo kidogo kila nyumba zikiisha wanazichulia mortgage and on and on and on.... kwahio wanapanda property ladder....

Thus kuifanya hii kama biashara kuna kanuni zake kama biashara nyingine na issue sio kujenga tu, bali unajenga wapi na kwa value gani na kwa kutumia gharama zipi (loan interest rates) wenzetu ulaya interest rates unapata single digit kwa urahisi sana....
 
Dar es salaam Tz kama unafanya biashara yako ya nyumba sehemu yenye biashara usingesema hailipi.
Wewe huna nyumba ya kukodisha. La sivyo usingesema hivyo.
Mimi naona hasara tupu. Na hapo nimerithi, yaani sijatumia hela kuijenga na nimewekewa nadhiri nisiiuze.
 
Hahahahaha jamaa hawaelewi hawa

Wanadhani ni gari la mkweche

Sometimes unaweza kuta nyumba iko poa tu mtu anaiweza ishi bila shida labda rangi tu ndio imefuba sasa mwenye nyumba mwenye kiherehere atataka apake tena rangi na kukarabati hiki nakile wala havina ulazima atajikuta anaingia cost za kijinga
Nakwambia wewe huna property.
Nyumba ina maintainances zinazotakiwa kwa muda fulani based on matumizi fulani ili ziishi muda mrefu.
Asilimia 90 ya nyumba za Dar es salaam zilizojengwa mwaka 2000 zimetitia. Baraza lipo level moja na ardhi.
Kisa, ni watu wenye mawazo kama yako.
Unaishi miaka hii bado unaongea maneno kama hayo ?
 
Wewe huna nyumba ya kukodisha. La sivyo usingesema hivyo.
Mimi naona hasara tupu. Na hapo nimerithi, yaani sijatumia hela kuijenga na nimewekewa nadhiri nisiiuze.
Okey, hapo nimekuelewa.

Kiufupi nyumba za kukodisha zinategemeana sana na umezijenga eneo gani kama ilivyo biashara nyingine zinavyohitaji kujua soko lako lilipo.

Unaweza ukawa na banda la m10 au kontena sehemu likakupa faida kubwa kuliko nyumba yenye thamani ya m100 sehemu isiyo sahihi.
 
Sawa, ila kwa mjadala huu nyumba inaleta heshima kama ilivyo gari.
Uzuri wake nyumba inabebwa na kiwanja (location).
Kiwanja kikiwa location mbaya, unakipata kwa bei ya kutupa, kiwanja kitapanda tu thamani, hata kikiwa kijijini subiri 10-20 years.
Kwa kijana anayeanza kazi, mimi nitamshauri akamate viwanja viwili vitatu kabla ya kujenga hata kama ni viwanja vya vijijini halafu ajenge.
Viwanja akae navyo tu hata 20 years au awe na shamba tu hata kwa 20 years.
Hii ni bahati ya kuwa mtanzania.
 
Ni sahihi kuwa na viwanja maana hata ukisema ujenge huwezi jenga bila kiwanja, na hata usipojenga kitapanda thamani kama ulivyosema. Ila nyumba ya kuishi ni lazima na muhimu sana na pamoja na heshima ni usalama wa familia yako, unapopata nafasi JENGA kisha baada ya hapo nunua hivyo viwanja hata usiponunua sawa.
 
Mimi naongea facts, siongei blah blah.
Nimerithi nyumba na ardhi. Nyumba ni headache na nimekatazwa na ukoo kuiuza.
Nyumba inaleta heshima kwa utamaduni wetu.

Kama heshima kwa jamii ingeweza kuwekwa thamani yake kifedha labda.
Ila huwezi.

Viwanja vina thamani inayokua. Hata by looking at the population increase. Mapori mengi ya miaka 15 iliyopita Sasa ni miji.

Nyumba haiongezeki thamani. Huo ni ukweli wa kimahesabu siyo hadithi njoo .
Huwezi kupigiana hesabu za nyumba ukanipa faida above interest rate ya Benki kuu.

Ukitaka tupigiane mahesabu hapa.
For ur point my friend assume ardhi ya kuuza imeisha mfano wa Kenya na nchi nying...... Kat ya ww muuza ardhi na landlord (mmiliki wa nyumba za kupangsha) nan atakuwa na consistancy income/cashflow....
 
Ardhi ya kuiuza unamaanisha nini?
Ardhi ni asset kama zilivyo assets nyingine.
Hata Nondo (steel) ni asset kubwa sana, Shaba, aluminium etc...
Ndiyo maana maskini anauza skrepa, tajiri ananunua.
Ardhi ya kuiuza ikiisha maana yake wewe una hela.
Usipotaka kupangisha, Bei itashuka.
 
Back
Top Bottom