Wanaosema Rais Magufuli hajui Kiingereza leo amewasuta

Of course hapa tunazungumzia waliosoma kwa lugha ya kiingereza. Wewe unadhani tunazungumzia waliosoma kwa lugha ya kinyanzutuzu? Unawezaje kuandika thesis za kuanzia masters mpaka Phd bila kujua lugha? Arguments na mambo mengine yote utaelezea kwa kutumia vidole? Vitabu na machapisho utakayosoma utaelewaje? BTW hata najaribu kumwelezea mtu asiyejua hata lectures huwa zinatolewaje.
 
Mbona sioni mahali aliposutwa mtu.Tanzania hasa Dar hakuna Corona.Mnahangaika nini.Mimi nilijifukiza nikiwa std 2 sasa ni mtu mzima kuna cha kunifundisha hapo.HAKUNA CORONA TANZANIA.WOOOOTE TULALE MBELR
Za kuambiwa changanya na zako alijisemea JK.

Maana, Waswahili walisema, mficha maradhi, mauti humfichua.
 
Dada Joy je?
Aje naye aseme anajua kiingereza halafu maneno hayo ayaseme kwa kiingereza.
Aseme " Mimi najua kiingereza maana kuanzia form one Hadi PhD nimesoma kwa kiingereza hata sesis zangu nimeziandika kwa kiingereza"
 
Huu utumwa wa kuona sifa kujua lugha za watu kama bado tunaendelea nao mpaka sasa tutachelewa Sana kupata maendeleo tunayoyataka.

Hakuna nchi iliyoendelea inatukuza lugha ya Nchi nyingine.
 
Hapa hatujadili broken english. Hapa tunajadili mtu anayeelewa kiingereza na kufanya mazungumzo hata kwa kutumia broken english! Umeelewa? Uliona ile clip Magufuli alipofanya ziara Uganda akaulizwa swali rahisi kabisa kwa kiingereza akabakia ametoa macho kama popo na akashindwa kuelewa ameulizwa nini mpaka Museveni akamsaidia? Mambo ya broken english ni wasomi au marais wengi wanazungumza lakini pamoja na kuwa broken english lakini wanazungumza kitu kinacho-make sense!
 

Unataka kuniambia Hasikii English ?
 
Labda wewe ndo hujui,Tena acha kabisa kusema Watanzania wengi wasomi hawajui Kiingeza au Inernational Language.Sema mimi sijui,na unanesha kweli hujui.
 
Huu utumwa wa kuona sifa kujua lugha za watu kama bado tunaendelea nao mpaka sasa tutachelewa Sana kupata maendeleo tunayoyataka.

Hakuna nchi iliyoendelea inatukuza lugha ya Nchi nyingine.
Utumwa ni pale unasoma o level, a level mpaka PhD ulitumia English lakini hauijui English [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sasa kwanini anajitetea anajua wakati kutokujua si tatizo? Kiingereza ni lugha kama zilivyo zingine hivyo asijisikie vibaya kutokukimudu.
 
Utumwa ni pale unasoma o level, a level mpaka PhD ulitumia English lakini hauijui English [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Yaani ni sawa wewe ni mpare halafu aje mtu akucheke kwakua hujui kimasai.
 
Nakumbuka niliangalia maadhimisho kama haya mwaka 2016 kwenye runinga. Akatoa shukran kwa kuchaguliwa. Kama kawaida anaongea Kiswahili na kuchomekea Kiingereza. Akasema, ' kati ya wote, mmenichagua mimi, who I am?', basi umati wote ukirudia ile ' who I am?' Na kicheko juu!
Kweli Magufuli hajui kiingereza!
 
Hili kamwambie mwenyewe, maana hotuba ya leo inakupinga.
 
..aliyemshauri Raisi kuzungumzia hayo ni nani?

..Jpm amekuwa madarakani huu ni mwaka wa 6, hivi anahitaji kujieleza na kujitetea kwamba anaimudu lugha ya Kiingereza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…