Katika soma yangu nimekutana na hii aya. Naona inapishana na baiolojia niliyosoma miaka ile ya sekondari.
Quran 23:14
Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyoganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu mbora wa waumbaji
English translation:
Then We made the sperm drop into a clinging clot, and We made the clot into a lump [of flesh], and We made [from] the lump, bones, and We covered the bones with flesh; then We developed him into another creation. So blessed is Allah, the best of creators.
Ukisoma tafsiri ya kiingereza na kiswahili unaelewa kwamba sperm inaingia kwenye damu iliyoganda. Nikatafuta wataalamu wa tafsiri kuhusu hiyo clot.
Prof Haanein Muhammad Makhloof, on page 508 of his Dictionary of the meanings of words of the Quran says that the Arabic word alaq translated into English as "clot" means frozen blood.
Maswali yangu
1. Sperm inaingia kwenye damu iliyoganda?
2. Damu iliyoganda inaishi ndani ya tumbo la mwanamke?
3. Quran haifahamu kuhusu yai la mwanamke?
4. Sperm peke yake inaweza kuumbwa ikawa mtu?
5. Kauli kwamba tukamfanya kiumbe mwingine inamaanisha nini?
battawi FaizaFoxy Mokiti adriz Kisai
Watu kama wewe,wakati yesu anafanya miujiza ndio wale waliomuita mchawi.kwa sababu wamejaa roho za chuki na ujinga ndani yao.
Na sio wote wanaosoma huwa wanaona na na kukielewa sawia kile kilichondikwa.
na ndio maana katika iyo aya Qur'an 24:14 uliyoinukuu(kwa kiswahili) hakuna palipoandikwa kuwa "manii inaingia katika damu iliyoganda" kama papo nioneshe.
katika hilo tayari umezusha na umeifanya kuwa hoja yako ya msingi.
Kwa hiyo hapa tunajadili uzushi.
Nachokushauri,somo au mada moja katika dini hizi mbili haiandikwi kwenye mstari au aya au kitabu kimoja, ndio maana biblia ni mkusanyiko wa vitabu vingi na Qur'an ni mkusanyiko wa vitabu vingi vile vile.
Kwa hiyo huwezi kuijua dini hata iyo yako kwa ku-google google tu.maana hata wajinga huwa wanaposti google.
Kwenye dini yoyote watu wanahoji na kitafsri maandishi.ndio maana Kuna "mafundisho" na "madrasa"
Kama kweli unania ya kuijua dini fulani jitoe kujifunza kwa wenye elimu nayo,hata mapadri na mashehe wamasome wakaelimika ndio maana huji kuwaona wakilumbana katika dini zao.
Maana DINI NI IMANI. yaani kuamini vinavyoonekana,visivyoonekana kwa macho ya nyama na kuamini vinavyowezekana na visivyowezekana kibinadamu.kwa hiyo katika Imani ya mtu hakuna jambo la ajabu kwake,
Ndio maana hata yesu "alitembea juu ya maji ,kwa nyayo zake" kitu ambacho kisayansi mtu kutembea juu ya maji haiwezekani,LAKINI KWA IMANI(dini).
Kwa hiyo kulinganisha dini na sayansi,KWA AYA MOJA" vitu ambavyo watu wanajifunza maisha yao yote kwa muda na gharama pia kwa na bado hawajavimaliza,kama sio chuki ni UJUHA.
Punguza kuteseka juu ya Imani za watu,ishi kwa Imani yako
ELIMU NI BAHARI.(Usitangulize kebehi,dharau kama kweli una nia ya kujifunza).
Wapo watu wana elemu katika wakristo na waislam ila hawatoi majibu wakishagundua nia ya mtoa mada,/hoja.wanaamua kukaa kimya,
KWA MAANA KUKAA KIMYA KIHENGA NA KIIMANI NI HEKIMA.
NA PIA KUKAA KIMYA NI JIBU KWA MPUMBAVU,(basi tusiwafanye wenye maarifa watukalie kimya).
Uwe na hekima katika kujifunza kwako.