Wanasema simjali mama yangu ila kiukweli sioni athari yake kwangu

Wanasema simjali mama yangu ila kiukweli sioni athari yake kwangu

Ni ngumu kumpa attention mtu ambaye hamna bond tangu mwanzo,binafsi nimekulia kwa watu yaani mama yangu namuona kama watu wengine.
Hatujawahi hata kukumbatiana yeye ndo naona ukaribu unakuja kuja labda kwa sababu nampa visenti mwisho wa mwezi ila huo ukaribu haukuwepo tangiapo.
We kijana unaumri wa miaka mingap Kwanza maana ushauri unaendana na umri
 
Kuna kitu zaidi ya kumuita mtu mama au baba ndo mana kuna watu wanaweza kufanya chochote kwa ajili ya mtu aliyemlea lakini si baba au mama mzazi aliyemtelekeza

Whatever the case hakikisha unatengeneza bond na wanao kuna mda utahitaji ukaribu wao zaidizaid watakutumia hela tu kama wanazo but not their love tusifarijiane kwamba mama ni mama you get what you give hii ni natural law
 
Umesema kweli bro mimi ni mmoja kati ya watu ninao experience hii hali kupitia mzazi wangu mmoja, nikiwa mtoto nilikua na upendo mkubwa sana kwa wazazi wawili ila hapa katikati ilitokea hali iliyovunja sana moyo wangu iliyosababishwa na mzazi mmoja ikapelekea hisia zangu za upendo kwake zipungue kwa kiasi kikubwa.

Hali kama hii ya kujikuta nimesahau kusalimiana nae hata kwa simu kwa wiki hata 3 huwa inatokea mara kwa mara muda mwingine unajishtukia na roho inauma inabidi ndo umtafute na kumtumia zawadi yoyote ili kuendelea kuonyesha upendo kwake lakini kiuhalisia upendo umeshapungua.

Sababu ni zilezile moyo wa mtu umeumbwa kumpenda anaeufanyia wema na kupunguza mapenzi kwa anaemuumiza/aliemuumiza.

Pole Sana Mkûu

Hiyo Hali Ipo Kwa Watu wengi Sana.
Kûna Watu wananipigiaga simu wakikueleza mambo Yao utabaki kuhuzunika.

MTU anakazi nzuri, anawahudumia Wazazi wake Vizuri lakini Hana love nao. Yaani hafanyi Kwa mapenzi. Yeye mwenyewe anatamani angeishi na Wazazi wake Kwa Upendo kama Watu Wengine.

Yeye hakulelewa na Baba na Mama, walimuacha Kwa Bibi.

Jamaa hata akienda Kwa Wazazi wake anakosa Stori na vibe la kuwa Sasa yupo na Mzee au bi Mkubwa
 
Hawawezi kukuelewa.

Alafu hata awe Karibu naye watazungumza kitu gàni?
Kumsaidia atamsaidia lakini itakuwa kama anavyosaidia Watu Back.
Nashangaa watu humu wanavyobishana,alafu mimi sikutelekezwa wala nini ni kwamba alinichukua mamdogo wangu tangu nikiwa na miaka mitano nikasoma huko mpaka nikamaliza secondary,mama yangu simchukii ila namuona kama watu wengine na amezoea hali hiyo,tofauti yake na wengine ni kwamba yeye nampa matunzo kama mama yangu ila huo ukaribu haupo.
 
Unaweza kuwa unampigia simu sioni tatizo .

Ila kuhusu BOND (connection) inaweza kuwa haipo maana Mama yako hakushiriki Sana katika makuzi yako.

Kwakuwa kupiga simu sio gharama waweza kuwa unampigia simu

Hata ukifanikiwa kupata chochote uwe unampa.

Maana umri aliokuwa nao mama yako kipindi wewe Una miaka 8 ni tofauti na sasa.

Yawezekana ufahamu wake ulikuwa chini na sasa upo juu.

So try to be positive and plant a good seed that will grow to other people.

Kama alikutupa wewe usimtupe
Don't repeat the same mistakes.
 
Nashangaa watu humu wanavyobishana,alafu mimi sikutelekezwa wala nini ni kwamba alinichukua mamdogo wangu tangu nikiwa na miaka mitano nikasoma huko mpaka nikamaliza secondary,mama yangu simchukii ila namuona kama watu wengine na amezoea hali hiyo,tofauti yake na wengine ni kwamba yeye nampa matunzo kama mama yangu ila huo ukaribu haupo.

Sasa hiko kitu Kwa Watu waliolelewa na Baba na Mama hawakielewi.

Alafu Watu àmbao hawajalelewa na Baba na Mama mapenzi hayawasumbui.

Ukimuacha akikufungia vioo ndîo intolee hiyo. NI zaidi ya makauzu
 
We kijana unaumri wa miaka mingap Kwanza maana ushauri unaendana na umri
Mi sio kijana mwenzio,nina heshima zangu na maisha yangu naongea kitu ambacho nina uzoefu nacho siongei kwa hisia.
 
Mi sio kijana mwenzio,nina heshima zangu na maisha yangu naongea kitu ambacho nina uzoefu nacho siongei kwa hisia.
Una heshima yeyote mwenye heshima awezi chukulia kawahida chanzo cha heshima wew mkubwa hovyo
 
Sasa hiko kitu Kwa Watu waliolelewa na Baba na Mama hawakielewi.

Alafu Watu àmbao hawajalelewa na Baba na Mama mapenzi hayawasumbui.

Ukimuacha akikufungia vioo ndîo intolee hiyo. NI zaidi ya makauzu
Aseee we jamaa ni hatari na nusu,unajua hata mimi niko hivyo sijawahi kusumbuliwa na mapenzi utavyonipeleka ndivyo nitakupeleka.Umehit mulemule.
 
Hali hii inaathiri sana,Mimi niliachwa na mama nikiwa na mwaka 1 na miezi 8,ukweli Huwa sioni umuhimu wake kwangu ,analalamika sana ila moyo wangu ni mzito sana kwake, ninawapenda kaka zangu kuliko mama, Kiufupi hakuna bondi kabisa Kwa mama yangu,sijui nifanye nini mimi!!!

Nilichojifunza ni kuwa upendo unatengenezwa ,kuzaa tu haikufanyi watoto wakupendea
 
Una heshima yeyote mwenye heshima awezi chukulia kawahida chanzo cha heshima wew mkubwa hovyo
We shida yako ni nini mbona unahitaji nijue kwamba we ni empty set unaendeshwa na mihemko,ebu achana na mimi
Huna hadhi ya kubishana na mimi,kajifunze kwanza kuandika.
 
Wakuu kwema.
Naombeni ushauri kwenye hili suala.
Mama yangu mzazi na ndugu wengine wanalalamika kwamba simjali mama yangu.

Kiukweli sio kwamba namchukia ila najisahau kumjulia hali.

Mama aliondoka nyumbani na watoto wa kike , akatuacha wakiume kama watatu pamoja na baba, wakati huo nilikuwa na miaka 8,
Nimeishi na baba peke yake hadi alipooa mwanamke mngine.
Mama wa kambo huyo ameishi kutunyanyasa sana hadi mzee alipomtimua nikiwa na miaka 17.

Nilipofika form 3 tukapata mawasiliano ya mama tukawa tunawasiliana naye ila yeye hakuwahi kututafuta , tukampotezea.

Sasa niko chuo nina miaka 24 , wanalalamika kwamba simjali mama yangu
Mama huwa naye analalamika japokuwa hajawahi kunipigia hata kunijiulia hali , ila nikimchek ni lawama.
Kiukweli sio kwamba simpendi ila namchukulia kawaida tu.
Sasa wakuu katika hali kama hii ushauri wenu ni upi
Achana na maneno ya ndugu, watachosema haijalishi. Bila shinikizo kutoka nje jitahidi sana umjali mzazi wako haijalishi yeye alitenda nini ila kuna sababu ya wewe kulichagua tumbo lake.

Muoneshe upendo bila ku prove something kwa watu, matunda yake utayashuhudia.
 
Wakuu kwema.
Naombeni ushauri kwenye hili suala.
Mama yangu mzazi na ndugu wengine wanalalamika kwamba simjali mama yangu.

Kiukweli sio kwamba namchukia ila najisahau kumjulia hali.

Mama aliondoka nyumbani na watoto wa kike , akatuacha wakiume kama watatu pamoja na baba, wakati huo nilikuwa na miaka 8,
Nimeishi na baba peke yake hadi alipooa mwanamke mngine.
Mama wa kambo huyo ameishi kutunyanyasa sana hadi mzee alipomtimua nikiwa na miaka 17.

Nilipofika form 3 tukapata mawasiliano ya mama tukawa tunawasiliana naye ila yeye hakuwahi kututafuta , tukampotezea.

Sasa niko chuo nina miaka 24 , wanalalamika kwamba simjali mama yangu
Mama huwa naye analalamika japokuwa hajawahi kunipigia hata kunijiulia hali , ila nikimchek ni lawama.
Kiukweli sio kwamba simpendi ila namchukulia kawaida tu.
Sasa wakuu katika hali kama hii ushauri wenu ni upi
Iwe itakavyokua huyo bado ni mama mzazi.huwezi kupata mwingine zaidi yake...kuwaacha wadogo wa kiume kwa baba na akaondoka na wakike...isiwe na wala si sababu.hujui kilichojiri wakati huo...kuwa naye katibu kadri uwezavyo...
 
Nataman uvae viatu vyangu sijawah muona mama ang TOKA NIZALIWE inasemekana alivyo nizaa hakuish muda mrefu alifarik aseee kuna hal flan ya maumiv ,,,NATAMAN HUYO MAMA AKO AWE MAMA ANGU,,
 
Wakuu kwema.
Naombeni ushauri kwenye hili suala.
Mama yangu mzazi na ndugu wengine wanalalamika kwamba simjali mama yangu.

Kiukweli sio kwamba namchukia ila najisahau kumjulia hali.

Mama aliondoka nyumbani na watoto wa kike , akatuacha wakiume kama watatu pamoja na baba, wakati huo nilikuwa na miaka 8,
Nimeishi na baba peke yake hadi alipooa mwanamke mngine.
Mama wa kambo huyo ameishi kutunyanyasa sana hadi mzee alipomtimua nikiwa na miaka 17.

Nilipofika form 3 tukapata mawasiliano ya mama tukawa tunawasiliana naye ila yeye hakuwahi kututafuta , tukampotezea.

Sasa niko chuo nina miaka 24 , wanalalamika kwamba simjali mama yangu
Mama huwa naye analalamika japokuwa hajawahi kunipigia hata kunijiulia hali , ila nikimchek ni lawama.
Kiukweli sio kwamba simpendi ila namchukulia kawaida tu.
Sasa wakuu katika hali kama hii ushauri wenu ni upi
Mama anatakiwa afanye jitihada si wewe, baada ya kuondoka kwa kipindi hiko alidhaninnini kitatokea?

Kuna wakati wazazi wa kitanzania lazima wabebe responsibility ya matendo yao
 
Back
Top Bottom