Wanasema simjali mama yangu ila kiukweli sioni athari yake kwangu

We kijana unaumri wa miaka mingap Kwanza maana ushauri unaendana na umri
 
Kuna kitu zaidi ya kumuita mtu mama au baba ndo mana kuna watu wanaweza kufanya chochote kwa ajili ya mtu aliyemlea lakini si baba au mama mzazi aliyemtelekeza

Whatever the case hakikisha unatengeneza bond na wanao kuna mda utahitaji ukaribu wao zaidizaid watakutumia hela tu kama wanazo but not their love tusifarijiane kwamba mama ni mama you get what you give hii ni natural law
 

Pole Sana Mkûu

Hiyo Hali Ipo Kwa Watu wengi Sana.
Kûna Watu wananipigiaga simu wakikueleza mambo Yao utabaki kuhuzunika.

MTU anakazi nzuri, anawahudumia Wazazi wake Vizuri lakini Hana love nao. Yaani hafanyi Kwa mapenzi. Yeye mwenyewe anatamani angeishi na Wazazi wake Kwa Upendo kama Watu Wengine.

Yeye hakulelewa na Baba na Mama, walimuacha Kwa Bibi.

Jamaa hata akienda Kwa Wazazi wake anakosa Stori na vibe la kuwa Sasa yupo na Mzee au bi Mkubwa
 
Hawawezi kukuelewa.

Alafu hata awe Karibu naye watazungumza kitu gàni?
Kumsaidia atamsaidia lakini itakuwa kama anavyosaidia Watu Back.
Nashangaa watu humu wanavyobishana,alafu mimi sikutelekezwa wala nini ni kwamba alinichukua mamdogo wangu tangu nikiwa na miaka mitano nikasoma huko mpaka nikamaliza secondary,mama yangu simchukii ila namuona kama watu wengine na amezoea hali hiyo,tofauti yake na wengine ni kwamba yeye nampa matunzo kama mama yangu ila huo ukaribu haupo.
 
Unaweza kuwa unampigia simu sioni tatizo .

Ila kuhusu BOND (connection) inaweza kuwa haipo maana Mama yako hakushiriki Sana katika makuzi yako.

Kwakuwa kupiga simu sio gharama waweza kuwa unampigia simu

Hata ukifanikiwa kupata chochote uwe unampa.

Maana umri aliokuwa nao mama yako kipindi wewe Una miaka 8 ni tofauti na sasa.

Yawezekana ufahamu wake ulikuwa chini na sasa upo juu.

So try to be positive and plant a good seed that will grow to other people.

Kama alikutupa wewe usimtupe
Don't repeat the same mistakes.
 

Sasa hiko kitu Kwa Watu waliolelewa na Baba na Mama hawakielewi.

Alafu Watu àmbao hawajalelewa na Baba na Mama mapenzi hayawasumbui.

Ukimuacha akikufungia vioo ndîo intolee hiyo. NI zaidi ya makauzu
 
We kijana unaumri wa miaka mingap Kwanza maana ushauri unaendana na umri
Mi sio kijana mwenzio,nina heshima zangu na maisha yangu naongea kitu ambacho nina uzoefu nacho siongei kwa hisia.
 
Mi sio kijana mwenzio,nina heshima zangu na maisha yangu naongea kitu ambacho nina uzoefu nacho siongei kwa hisia.
Una heshima yeyote mwenye heshima awezi chukulia kawahida chanzo cha heshima wew mkubwa hovyo
 
Sasa hiko kitu Kwa Watu waliolelewa na Baba na Mama hawakielewi.

Alafu Watu àmbao hawajalelewa na Baba na Mama mapenzi hayawasumbui.

Ukimuacha akikufungia vioo ndîo intolee hiyo. NI zaidi ya makauzu
Aseee we jamaa ni hatari na nusu,unajua hata mimi niko hivyo sijawahi kusumbuliwa na mapenzi utavyonipeleka ndivyo nitakupeleka.Umehit mulemule.
 
Hali hii inaathiri sana,Mimi niliachwa na mama nikiwa na mwaka 1 na miezi 8,ukweli Huwa sioni umuhimu wake kwangu ,analalamika sana ila moyo wangu ni mzito sana kwake, ninawapenda kaka zangu kuliko mama, Kiufupi hakuna bondi kabisa Kwa mama yangu,sijui nifanye nini mimi!!!


Nilichojifunza ni kuwa upendo unatengenezwa ,kuzaa tu haikufanyi watoto wakupendea
 
Una heshima yeyote mwenye heshima awezi chukulia kawahida chanzo cha heshima wew mkubwa hovyo
We shida yako ni nini mbona unahitaji nijue kwamba we ni empty set unaendeshwa na mihemko,ebu achana na mimi
Huna hadhi ya kubishana na mimi,kajifunze kwanza kuandika.
 
Achana na maneno ya ndugu, watachosema haijalishi. Bila shinikizo kutoka nje jitahidi sana umjali mzazi wako haijalishi yeye alitenda nini ila kuna sababu ya wewe kulichagua tumbo lake.

Muoneshe upendo bila ku prove something kwa watu, matunda yake utayashuhudia.
 
Iwe itakavyokua huyo bado ni mama mzazi.huwezi kupata mwingine zaidi yake...kuwaacha wadogo wa kiume kwa baba na akaondoka na wakike...isiwe na wala si sababu.hujui kilichojiri wakati huo...kuwa naye katibu kadri uwezavyo...
 
Nataman uvae viatu vyangu sijawah muona mama ang TOKA NIZALIWE inasemekana alivyo nizaa hakuish muda mrefu alifarik aseee kuna hal flan ya maumiv ,,,NATAMAN HUYO MAMA AKO AWE MAMA ANGU,,
 
Mama anatakiwa afanye jitihada si wewe, baada ya kuondoka kwa kipindi hiko alidhaninnini kitatokea?

Kuna wakati wazazi wa kitanzania lazima wabebe responsibility ya matendo yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…