Wanasema simjali mama yangu ila kiukweli sioni athari yake kwangu

Wanasema simjali mama yangu ila kiukweli sioni athari yake kwangu

Wakuu kwema.
Naombeni ushauri kwenye hili suala.
Mama yangu mzazi na ndugu wengine wanalalamika kwamba simjali mama yangu.

Kiukweli sio kwamba namchukia ila najisahau kumjulia hali.

Mama aliondoka nyumbani na watoto wa kike , akatuacha wakiume kama watatu pamoja na baba, wakati huo nilikuwa na miaka 8,
Nimeishi na baba peke yake hadi alipooa mwanamke mngine.
Mama wa kambo huyo ameishi kutunyanyasa sana hadi mzee alipomtimua nikiwa na miaka 17.

Nilipofika form 3 tukapata mawasiliano ya mama tukawa tunawasiliana naye ila yeye hakuwahi kututafuta , tukampotezea.

Sasa niko chuo nina miaka 24 , wanalalamika kwamba simjali mama yangu
Mama huwa naye analalamika japokuwa hajawahi kunipigia hata kunijiulia hali , ila nikimchek ni lawama.
Kiukweli sio kwamba simpendi ila namchukulia kawaida tu.
Sasa wakuu katika hali kama hii ushauri wenu ni upi
Ni mama yako jitahidi kumpa attention. Haujui nini kiliwatenganisha na mshua, kwaiyo usiweke akilini kwa sababu huo ni ugomvi wa wazazi. Suala la lawama ni kawaida kwa wanawake ndivyo walivyoumbwa.
 
Huo ni Mtazamo wako..ondoa hizo Negativity

Naongea kitu ambacho Ninakijua wewe unaongea assumptions.

Kuzaa na Kupenda hakuna uhûsiano.

Asilimia kûbwa ya Watoto àmbao hawajalelewa na Wazazi waô wanamuelewa mtoa Mada anachokisema.
Ninyi Wengine mnafanya assumptions na kuwafundisha unafiki, waigize
 
Mkuu mamako anatafuta kupendwa sehemu ambayo hakupanda upendo.
Usiingie kwenye mtego wa kutaka kuonesha kuwa yeye ni muhimu sana kwenye maisha yako.Alichopanda anayo haki ya kuvuna.
Hakikisha msingi wa maisha yako hautegemei hisia za watu wengine.
Amua na kufanya unachoona ni sahihi kwako na hauvunji sheria za nchi.
Una uzoefu na iyo hali anayo pitia au niubutu wa akili yako kumshauri mambo usiyo weza au kuyapitia
 
Hujawahi kubeba kiumbe tumboni huwezi kuelewa..Mwanamke Pekee aliebahatika kuitwa Mama ndio anaelewa ata nielezeje ni kama napoteza mda tu

Hakuna kitu Kama hicho.
Wàpo Wanawake maelfu wametelekeza Watoto, Wengine wameua Kwa Kutoa Mimba na kutupa vichanga alafu unasema kitu gàni l.
Wadanganye wasiojua jinsi binadamu alivyo.

Mama au Baba huwa na uchungu na Mtoto aliyemzaa na kumlea na siô vinginevyo.
Tenà aliyelea anakuwa na uchungu zaidi ya Yule aliyezaa.

Kubeba Mimba hata Wanyama wanabeba,

Upendo na uchungu msingi wake Mkûu siô kuzaa Bali Malezi, Muda uliotumika kumkuza Mtoto ndîo unafanya thamani na Mzazi kuona uchungu Kwa Mtoto.

Fikra potofu Kabisa.
 
Back
Top Bottom