Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Nyani my brother, taaluma ya sheria ni zaidi ya lugha...
Hata taaluma ya lugha ni zaidi ya lugha. So what's your point here?
Mtu anadhani anajua lugha basi anajua sheria,
Ni nani huyo anayedhani kujua lugha ndo kujua sheria?
basi ingekua mtu akisomea lugha anakua ni mwanasheria.
Hoja ya kitoto kabisa hii. Kwani hata wewe kwa vile unajua kusoma na kuandika kwa lugha ya Kiswahili hakukufanyi uwe mtaalamu wa lugha ya Kiswahili. Kujua kutoa na kujumlisha hakukufanyi uwe mwanahisabati. So again, what's your point?
Kwanini wachaguliwe baadhi tu kua wanasheria tena ngazi kwa ngazi?
Kwa nini wachaguliwe baadhi tu kuwa makomandoo, wahasibu, mafundi umeme, na kadhalika? Mbona una maswali ya kitoto sana wewe. Maana hujajibu hata hoja moja katika nukuuu uliyoinukuu na badala yake unauliza maswali ya jumla jumla tu. Come one now.
Kitu gani kinachowafanya walimu wa vyuoni wakaona fulani amefuzu? Ni lugha?
Mimi sijui maana sijafika wala kusoma chuo chochote. Niambie wewe msomi.
Tuchukue mfano kidogo, neno contract mtu anaweza kulitafsiri kama lilivyo kwa lugha yoyote ila ni wangapi wanaojua kua contract ni zaidi ya makubaliano ya watu wawili wenye akili timamu nk?
Contract ni zaidi makubaliano ya watu wawili wenye akili timamu tu? Kwa hiyo kwa mwanasheria contract ni nini na kwa mbeba maboksi kama mimi ni nini?
Wangapi unakuta anakuonyesha contract ambayo haifai kuitwa contract ilihali yeye anaita contract as agreement?
Sijui ni wangapi maana sijawahi kukutana na hata mmoja wa hivyo. Wewe umewahi?
Umeninukuu lakini hujajibu swali langu hata moja. Kwa nini? Kama umejibu naomba nionyeshe ulipojibu.
Kwa nini ni vigumu kuelewa kama mimi siyo mwanasheria? Kigumu ni nini? Ni lugha? Wanasheria wana nini cha zaidi katika akili yao hadi waweze kuwa na uwezo wa kutafsiri sheria ambao sisi wengine tusio wanasheria hatuna?
Wewe ni mwanasheria? Na kwani mwanasheria naye hawezi kufikiri kuwa anao uwezo au anajua kitu wakati kumbe hajui? Au mtu akiwa mwanasheria basi anageuka kuwa 'breed' tofauti na sisi mere mortals?
Hebu nipe mfano wa jambo ambalo ni gumu kwa 'layman' kama mimi kulielewa. Nipe mfano mmoja tu.
Sijaona popote ulipojibu.