Wanasheria wa Serikali Wakwama Mahakama ya Kimataifa. Bilioni 300 Kuchotwa

Kwa mwanasheria mkuu aliyepo sasa hivi kwenye serikali hii ni kizungumkuti maana yeye ni kubambika kesi kwa wananchi wanaohoji kuhusu masuala mbalimbali yenye maslahi ya taifa.

Ni bora ang'olewe awekwe mwingine ambaye hawezi kuwa 'compromised'
 
Kwa mwanasheria mkuu aliyepo sasa hivi kwenye serikali hii ni kizungumkuti maana yeye ni kubambika kesi kwa wananchi wanaohoji kuhusu masuala mbalimbali yenye maslahi ya taifa.

Ni bora ang'olewe awekwe mwingine ambaye hawezi kuwa 'compromised'

..ktk hili suala sio Mwanasheria Mkuu kuwa "compromised."

..labda tuseme Mwanasheria Mkuu kuwa "compromised" kwa kushindwa kumshauri Rais [magufuli]asifanye maamuzi ya kibabe, yatayoitia nchi hasara.

..Magufuli aliwahi kusababisha hasara ya sh bilioni 15 baada ya mahakama kuu Mwanza kutoa hukumu kwamba alivunja kituo cha mafuta bila kufuata sheria na kwa kukiuka ushauri aliopewa.

..Kwa maoni yangu tatizo lilikuwa ni Magufuli na tabia zake za kibabe.
 
Hata huyu aliyepo sasa hivi kuna madudu na rais atakayekuja atakuja kupindua meza kurejesha maslahi ya nchi sio wenye uwezo wa kipesa na watakaoathirika kutokana na maamuzi hayo kwa manufaa ya nchi watafungua kesi nao kwa kushauriwa na wanasheria hawa hawa kwamba fanyeni hivi ili mlipwe kwa hiyo sio sawa kumlaumu hayati JPM
 

..unatakiwa kupindua meza kwa kutumia akili sio kukurupuka.

..Magufuli alikuwa tatizo tangu akiwa Waziri wa ujenzi.

..kuna kesi ya kuvunja kituo cha mafuta Mwanza hasara yake bil 15.

..kuna kesi ya kuvunja mkataba wa ujenzi kibabe iliyopelekea ndege yetu bombardier kukamatwa Canada.

..Kuna jamaa amewahi kuandika hapa JF kwamba mikataba yote ya madini aliyoikuta Magufuli ilikuwa na kipengele cha kuijadili upya baada ya kipindi fulani.

..Kama madai hayo ni ya kweli basi kulikuwa hakuna ulazima wa Magufuli kufanya vurugu alizofanya.
 
Alikuwa na uthubutu kukataa ujinga kwa ajili ya wananchi kwa gharama zozote zitakazojitokeza. Kama kulipa lipeni kwa sababu ya viongozi wasio wazalendo walilitumbukiza taifa kwenye mikataaba yenye nia OVU na kwa faida ya watu wachache hasa baadhi ya viongozi wasio waaminifu.
 

..kiongozi anaposema kwa "gharama zozote" inabidi zitoke mfukoni kwake, na sio zitokane na kodi za wananchi.
 
.. Etwege na genge lake walikuwa wanashangilia eti hatujashtakiwa miga!!

Mjinga huyo dogo, yaani kwa kuivaa kichwa kichwa mikataba ya hatari vile tungeachwa? Au alidhani hayo makampuni ya kimataifa yangemuogopa yule mlevi wa madaraka?
 
Waliotuingiza kwenye hasara kama hi inatakiwa washtakiwe huu ni upuuzi hiyo pesa tunalipa sisi wananchi.
Hapa ndipo tatizo la siasa zetu lilipo. Hakuna atakayekubali jina lake kutajwa kuwa alihusika na kuandaa mkataba uliozaa janga hili. Hasa alieweka sahihi kuidhinisha jambo hilo angetolewa hadharani tukamfahamu au tukawafahamu.
 
Hapa kuna shida, unajiuliza nchi nzima inaingia mkataba bila ufahamu wa namna ya kuusitisha?
 
Hapa nikitamka kwamba kwa hali ilipofikia haitakuwa sahihi mzigo huu kwa kuanzia akabebeshwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali? La sivyo tuonyeshwe aliishauri nini serikali. Kama ushauri alitoa kupinga swala hilo na serikali haikuzingatia ushauri huo, kwanini basi hakujiuzulu?
 
Uthubutu ni sahihi lakini ingetakiwa kuwepo mchakato wa kuhakikisha kuwa maamuzi yanafanyika kwa maslahi mapana ya Taifa letu.
 
Kavipi kizimkaz apewe mwalabu afu io ela tukalipe ao machalii wa IDA
 
Hapa kuna shida, unajiuliza nchi nzima inaingia mkataba bila ufahamu wa namna ya kuusitisha?

..umesahau kwamba Rais wa Tz ni mungu-mtu?

..mtu akishakuwa Rais wa Tz mara moja anatunukiwa PhD na anakuwa na maarifa ktk kila jambo kuliko raia wote.
 
Mifumo ya mahakama ya kiupendeleo inawafanya mawakili wetu wasiwe vichwa. Huwa wanashinda kesi kwa maagizo ya juu. Sasa wakienda huku, vichwa chali...
 
..msimlaumu Samia ktk suala hili.

..kesi tuliyoshindwa imetokana na maamuzi ya Magufuli, akishauriwa na Prof.Kabudi, na Prof.Kilangi.
Mahakama zao

Walalamikaji wao?

What else .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…