Wanasheria wa Serikali Wakwama Mahakama ya Kimataifa. Bilioni 300 Kuchotwa

Nimesoma huku nikipatwa na uchungu mkali Sana moyoni

Pesa zote hzo zinakwenda kuliwa na wahuni
 
Yaani Bilioni 300 ambazo ni sawa na pesa ya kujenga km 250 za Lami tunaenda kuwalipa Matapeli wa Indiana Resources ambao Wanashulikiana na Mafisadi wa Serikalini.

Daa inauma Sana aisee
---

Mapendekezo au hoja mbili kati ya tatu ilizowasilishwa na Tanzania kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) yamepigwa chini.

Serikali iliwasilisha hoja hizo baada ya ICSID, Julai 2023 kutoa hukumu, hivyo walitaka Mahakama hiyo kufuta hukumu inayoelekeza kulipa fidia ya Dola 109 milioni za Marekani (Sh272 bilioni) kampuni ya Indiana Resources (IDA).

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa ya ICSID hela hiyo imefikia Dola za Marekani 112.9 milioni (Sh282 bilioni) pamoja na gharama za ziada za Dola 4.2 milioni (Sh10.5 bilioni) ambayo ni jumla ya zaidi ya Sh292 bilioni.

Kwa mujibu wa hukumu hiyo riba ya Dola za Marekani milioni moja (Sh2.5 bilioni) itaongezeka kila mwezi hadi Tanzania itakapolipa kiasi hicho au Indiana itakapozuia mali ya Tanzania itakayoendana na thamani ya madai hayo.

Desemba 2023, Mwanasheria Mkuu wa Tanzania alitoa barua ya uthibitisho kwa ICSID kwamba Tanzania ingelipa bila masharti na bila kubatilishwa kiasi chote cha fedha hiyo ndani ya siku 45 baada ya uamuzi wa mwisho wa kubatilisha. Hata hiyo ni takribani miezi miwili sasa tangu hilo litokee.

Mapitio ya Tanzania kubatilisha kesi yatafanywa Machi 15, 2024 na wadai kujibu Aprili 26, 2024. Kisha kila upande utakuwa na majibu yao mtawalia.

Mei 24, 2024 na Juni 21, 2024 kutakuwa na mkutano wa pamoja wa wiki tatu kabla ya tarehe ya mwisho ya maamuzi.

Mwananchi
Mama anaupiga mwingiiii...

Magufuli mzalendo kawakomesha mabeberu...

Na bado.
 
Daah, mabeberu sio watu. Wanatupiga kwa kutumia upumbavu wa viongozi wetu.
Ambacho nakihisi hapo ni kwamba hao wanasheria wa tanzania wameahidiwa donge nono na watapewa donge nono baada ya hayo malipo haramu kufanyika kutokana na kushindwa hiyo kesi, maana hata kushindwa kesi inawezanijawa ni sehemu ya dili zilezile
 
Shamba la Kizimkazi halina mwenyewe wacha wajipigie tu kwani nini bana

..hayo makesi na mafaini yamesababishwa na ujuaji wa Magufuli, Kabudi, na Kilangi.

..Lissu alionya bungeni kuhusu suala hili lakini akawa anabezwa ati ni mwanasheria wa hovyo anayeogopa kushtakiwa.

..Zaidi kwasababu ya kupaza sauti watawala wakajaribu kumuua.

..Ukweli unabaki kwamba hii ni hasara ambayo imetokana na kiburi cha watawala wetu.
 
Ambacho nakihisi hapo ni kwamba hao wanasheria wa tanzania wameahidiwa donge nono na watapewa donge nono baada ya hayo malipo haramu kufanyika kutokana na kushindwa hiyo kesi, maana hata kushindwa kesi inawezanijawa ni sehemu ya dili zilezile

..wanasheria wa bongo hawajasajiliwa kutetea kesi ktk hizo mahakama.

..kesi ikishakwenda nje Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Tz anatafuta mawakili wa kututetea ktk mahakama za nchi ambako kesi inaendeshwa.

..baada ya hapo kunakuwa na mpambano baina ya mawakili wetu na mawakili wa waliotushtaki.

..tusilaumu wanasheria wetu ktk hili. Kilichotuponza ni kuvunja mikataba bila kufuata utaratibu.
 
Viongozi wa kiafrica wa starve watu wao kwa kuwapa hawa matapeli wa dunia rasilimali zetu , huku hawa hawa matapeli yakilindwa na sheria zao .poor dark continent
 
Sio kweli!

Wasomi wa nchi hii ndio mambumbumbu mbugila mbugila. Inategemea usomi wake unampea ulaji kupitia wapi, ndiko atakapokuwa anaelewea

Yote aliyoyafanya Makonda na nguvu aliyokuwa nayo kipindi kile mpaka mkasema anatumwa na mwamba, SAA HII anatumwa na nani?
Tena ni majangili kabisa shenzi zao
 
Siku zote tunasema utawala wa CCM umefitinika duniani na mbinguni wao wanafikiri tunawabeza!
Ni utawala uliojaa;
Uovu
Ufisadi
gilba
uongo
utapeli!
 
Sio kweli!

Wasomi wa nchi hii ndio mambumbumbu mbugila mbugila. Inategemea usomi wake unampea ulaji kupitia wapi, ndiko atakapokuwa anaelewea

Yote aliyoyafanya Makonda na nguvu aliyokuwa nayo kipindi kile mpaka mkasema anatumwa na mwamba, SAA HII anatumwa na nani?
Mkuu inakuwa ngumu sana kujadili mada kwa kurukaruka. Twende na mada kama ilivyoletwa na hayo mengine yatakuwa na mada tofauti
 
Kesi ambazo serikali imewahi kuwa nazo, labda tuanzie awamu ya pili mpaka sasa, kuna ambazo serikali imewahi kushinda?
  • Na zile ilizoshindwa, kuna lolote lilifanyika kuzuia kesi kama hizo zisitokee tena?
  • Kama kuna ukanjanja uliosababisha kuwa kesi, kutokea serikalini, hao makanjanja waliotusababishia hayo, wako wapi? Ni kina nani? Nini kimefanyika dhidi yao?

Zile kesi tulizoshinda, kuna lolote tumejifunza? Nimesikia Accacia waliilipa serikali tsh 900bn, je ni kweli?
  • Kesi zilizofufuliwa awamu hii, zinaendana na matatizo ya kutengeneza kama umeme, inflation etc
  • Kwa mujibu wa Mpina, serikali inapaswa kuanza kulipwa fidia kwa mujibu wa mkataba kutokana na ucheleweshwaji wa bwawa la Nyerere, nini kinaendelea?

Kesi za awamu ya 5 ni zipi na status zake zikoje?
 
Yaani Bilioni 300 ambazo ni sawa na pesa ya kujenga km 250 za Lami tunaenda kuwalipa Matapeli wa Indiana Resources ambao Wanashulikiana na Mafisadi wa Serikalini.

Daa inauma Sana aisee
---

Mapendekezo au hoja mbili kati ya tatu ilizowasilishwa na Tanzania kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) yamepigwa chini.

Serikali iliwasilisha hoja hizo baada ya ICSID, Julai 2023 kutoa hukumu, hivyo walitaka Mahakama hiyo kufuta hukumu inayoelekeza kulipa fidia ya Dola 109 milioni za Marekani (Sh272 bilioni) kampuni ya Indiana Resources (IDA).

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa ya ICSID hela hiyo imefikia Dola za Marekani 112.9 milioni (Sh282 bilioni) pamoja na gharama za ziada za Dola 4.2 milioni (Sh10.5 bilioni) ambayo ni jumla ya zaidi ya Sh292 bilioni.

Kwa mujibu wa hukumu hiyo riba ya Dola za Marekani milioni moja (Sh2.5 bilioni) itaongezeka kila mwezi hadi Tanzania itakapolipa kiasi hicho au Indiana itakapozuia mali ya Tanzania itakayoendana na thamani ya madai hayo.

Desemba 2023, Mwanasheria Mkuu wa Tanzania alitoa barua ya uthibitisho kwa ICSID kwamba Tanzania ingelipa bila masharti na bila kubatilishwa kiasi chote cha fedha hiyo ndani ya siku 45 baada ya uamuzi wa mwisho wa kubatilisha. Hata hiyo ni takribani miezi miwili sasa tangu hilo litokee.

Mapitio ya Tanzania kubatilisha kesi yatafanywa Machi 15, 2024 na wadai kujibu Aprili 26, 2024. Kisha kila upande utakuwa na majibu yao mtawalia.

Mei 24, 2024 na Juni 21, 2024 kutakuwa na mkutano wa pamoja wa wiki tatu kabla ya tarehe ya mwisho ya maamuzi.

Mwananchi

View: https://www.instagram.com/p/C3H2iL2Igja/?igsh=czIwZXllcDBmaWl4
 
Back
Top Bottom